MkenyaMzalendo
Senior Member
- Sep 12, 2010
- 171
- 16
Kama ungetaka huduma za wakili, kuchorewa mkataba ama ushauri wowote, tafatheri tuma ujumbe na utahudumiwa.
Kama ungetaka huduma za wakili, kuchorewa mkataba ama ushauri wowote, tafatheri tuma ujumbe na utahudumiwa.
Kama unataka huduma za wakili, kuandikiwa mikataba au ushauri wowote wa kisheria, tafadhali tutumie ujumbe ili tukuhudumie.
Samahani, ni nini maana ya hio sentensi ; maana umerudia niliyoyasema, ama labda ulikuwa unasahihisha kiswahili changu kibovu? lol
Kama ungetaka huduma za wakili, kuchorewa mkataba ama ushauri wowote, tafatheri tuma ujumbe na utahudumiwa.
Nilikuwa naweka sawa kiswahili ili tangazo lako lisomeke na kueleweka vema. Pia kumbuka kuwa wakili ni mtaalamu na kama ni mzuri sana anaitwa ''mahiri'' ingesomeka wakili mahiri. Shupavu hutumika katika mambo yanayohusu ushujaa kama ''askari shupavu' ingawa pia anaweza kuwa askari mahiri na shupavu, kwa maana ya kuwa ni askari mtaalamu na shujaa.
Lengo lilikuwa kuweka tangazo la wakili mahiri lisomeke na kueleweka vema. Ahsante kwa kuuliza.
Are you registered with the Tanganyika Law Society? Are you registered with the Judiciary and your name is in the roll of Advocates at the High Court? Whats your Roll No? If yes i will PM you. If not please dont lie to us the Tanzanians.
Sidhani haswa nia yako ni ya kunipatia kazi, bali ni kufanya uchunguzi na kisha baadaye kunichukiza kwa watanzania wenzako. Unajua vizuri ya kwamba mfumo wa EAC unakubalisha ma-professionals wa nchi husika kufanya kazi katika nchi zote washiriki. Tz kama kawaida wamejikokota kutekeleza mkataba uliopo ili mtu kama mimi tuwahudumie WaTz (Kenya na Rwanda wametekeleza huo Mkataba na Uganda pia wameahidi kufanya hivyo hivi karibuni).
Ningependa kukujulisha ya kuwa sasa hivi waKenya wengi wanatoa huduma za wakili kwa watu wa nchi za ngambo (Marekani, Uingereza na Australia) kupitia mtandao, na wanaingiza hela tosha. Hebu tazama hii link
Search Jobs on Elance
Kwa nini tusiwahudimie Wenzetu kutoka Tz kwa mtandao?
You must be an ambulance chaser! this is not allowed in Tanzania.Hebu nipe contacts zako nipate kukushughulikia.
karibu sana mkuu, tanzania imejaaliwa ukarimu, na udhalimu pia.. cha maana tu ufuate taratibu... ila hiyo ya sie kununua ardhi kenya nadhani umepotoka, tunayo plenty pande ya huku bongoNa pia mkumbuke kwa sasa hivi mimi nalenga wale watu ambao labda wanafanya biashara Kenya, ama wangetaka kufanya biashara na Mkenya, kununua ardhi huko, nk, na wangetaka hizi huduma kwa bei mwananchi wa kawaida anaweza kumudu.
karibu sana mkuu, tanzania imejaaliwa ukarimu, na udhalimu pia.. cha maana tu ufuate taratibu... ila hiyo ya sie kununua ardhi kenya nadhani umepotoka, tunayo plenty pande ya huku bongo
thanks sana mazee
Shukran pia kwa ukarimu wako. Kumbuka Kuna adhari za kujitwika mamlaka usiyopewa, na dukuduku zinaarifu kuwa WaTz hawajamteua msemaji wa wanabiashara wote na kumshauri atangaze kuwa WaTz WOTE watasusia kufanya biashara huko Kenya, haswa kununua ardhi na kujenga manyumba, kwa hivo nimesema ahsante kwa kujitolea kwako, ingawa nahisi maoni yako hayajakubaliwa na kila MTz.
Nimekutana na wabongo kadhaa wanaofanya kazi ya Real Estate ambayo imenoga sana hapa Nairobi
Ni kweli kabisa, wewe ni shupavu... endelea na mambo yakoShukran pia kwa ukarimu wako. Kumbuka Kuna adhari za kujitwika mamlaka usiyopewa, na dukuduku zinaarifu kuwa WaTz hawajamteua msemaji wa wanabiashara wote na kumshauri atangaze kuwa WaTz WOTE watasusia kufanya biashara huko Kenya, haswa kununua ardhi na kujenga manyumba, kwa hivo nimesema ahsante kwa kujitolea kwako, ingawa nahisi maoni yako hayajakubaliwa na kila MTz.
Nimekutana na wabongo kadhaa wanaofanya kazi ya Real Estate ambayo imenoga sana hapa Nairobi
Rules of Professional Conduct and Etiquette of the Tanganyika Law Society haziruhusu mambo ya advertisement! Huko Kenya kama mawakili mnajitangaza muishie huko huko!
Hehehehe.
Arguments kama hizi zinatumika sana katika juhudi za kukwepa competition, labda mawakili wa Tz wanafahamu mlo wao utakuwa hatarini wakiruhusu mawakili shupavu kama mimi kuhudumia WaTz. Wanataka kuendelea kutoa huduma duni kwa wananchi kwa bei ghali. Anyway, kama nilivyosema, huduma za wakili siku hizi zinapokewa kwa mtandao na hata kama Wana TZ law Society watadinda kuturuhusu tishirikiane nao, kuna njia mingi za ku-evade restrictions hizo za kipumbavu