Wakili Mwabukusi kachukua point zote kuhusu mkataba wa DP World

Nauliza tu, naona kuna watu ghafla bin vu ameanza kutumia neno watanganyika sana katika kipindi hichi cha karibuni. Masuali yangu ni hivi kwani tanganyika bado ipo? Kama ipo ni nani raisi wa tanganyika? liko wapi bunge la tanganyika? ni wapi panapopitishwa bajeti ya tanganyika? ni wapi inakopepea bendera ya tanganyika? Ni lini ilikuwa mara ya mwisho kuimbwa wimbo wa taifa wa tanganyika katika shuhuli za kiserikali? mbali ya vitambulisho vya utanzania, watanganyika wenyewe viko wapi vitambulisho vya watanganyika?
Zanzibar bado ipo, wana raisi wao, wana bunge lao linaitwa baraza la wawakilishi, baraza la wawakilishi linapitisha bajeti ya nchi ya zanzibar, wimbo wao wa taifa huimbwa kila pale raisi wao anapohudhuria shuhuli za kiserikali, wazanzibari wana vitambulisho official vya utaifa wa zanzibar na pia wanavyo vitambulisho vya utaifa wa tanzania.

Nadhani kabla ya kuanzisha makelele ya utanganyika jambo la mwanzo nahisi ni kudai kurudishwa na kutambulika kisheria nchi ya tanganyika. Mnaweza kufanya hivi kwa kuwapa tafu lile kundi la wazanzibari walioichukua kesi ya muungano kwenye mahakama ya kimataifa kutaka mabadiliko ya muungano wa zanzibar na tanganyika.

Ni mawazo yangu tu.
 
Jamaa amewakomboa wanyakyusa na kwasasa nimewaweka kwenye kundi la wanamume, huyu jamaa binafsi nikifika mbeya nitafika ofisini kwake nipige naye story mbili tatu.
 
Back
Top Bottom