Nasikitika sana kuhusu Bunge letu.
Yani Bunge limebaki kuitikia tu kila kinacholetwa na Serikali.
Leo hii tunawategemea watu binafsi kuliokoa Taifa letu dhidi ya uvamizi wa maharamia wanaokuja na vazi la kondoo.
Leo hii tunawategeme viongozi wachache wa Dini kufanya kazi ya Bunge.
Hivi Wabunge wote kweli hawakuliona hili?
Yaani Bandari zote za Bahari, Mito na Maziwa kamiliki kakampuni kamoja ka huko Dubai kweli ?
Kampuni ambayo tunaweza kuiajiri na tukailipa.
Hili Bunge tutaliamini vipi tena kesho ?
Binafsi nawashukuru sana SHURA YA MAIMAMU TANZANIA na BARAZA LA MAASKOFU TANZANIA kwa kusimamia kidete bila kupepesa macho na kulitetea Taifa letu kwa jasho na Damu.
Kama Mlinzi wetu Mkuu anakavulia madaraka yake kakampuni ka mji wa Dubai hakika ametukosea sana.
Tulimwamini sana na kumtegemea bila wasi wasi.
Sasa hivi tuna wasiwasi mkubwa sana na vyombo vyetu vya ulinzi wa raslimali zetu.