MKUNGA
JF-Expert Member
- Dec 10, 2009
- 441
- 72
Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, Stanslaus Boniface Makulilo (44) Jembe, amefariki ghafla usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Dk. Eliezer Feleshi, alithibitisha taarifa za kifo hicho jana asubuhi alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima. Dk. Feleshi alisema kuwa ofisi yake na taifa kwa ujumla limepata pigo kubwa kwa kuondokewa na gwiji wa uendeshaji wa mashtaka, hususan ya jinai hapa nchini. Aliongeza kuwa mchango wa marehemu katika uendeshaji wa kesi hautasahaulika na utaenziwa.
Dk. Feleshi alieleza kuwa Jumamosi jioni, Boniface, ambaye pia alikuwa Msimamizi wa Uendeshaji wa Kesi zenye Maslahi kwa Umma, alifika Dar es Salaam akitokea Moshi, ambako alikwenda kutoa mafunzo kwa maofisa wa Idara ya Uhamiaji kuhusu uendeshaji wa mashtaka. Alikuwa mwenye afya njema na alirejea nyumbani kwake Kinondoni. Hata hivyo, usiku hali yake ilibadilika ghafla na alikimbizwa Hospitali ya Regency kwa matibabu.
"Baada ya kufikishwa hospitalini hapo, alifariki dunia. Kwa sasa siwezi kusema chanzo cha kifo hicho hadi tutakapopata taarifa rasmi za madaktari. Msiba upo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mtaa wa Sinza Load Kitalu Na. 4, na utaratibu wa mazishi utajulikana leo," alisema Dk. Feleshi.
Dk. Feleshi alimuelezea Boniface kama mmoja wa mawakili wa serikali waliokuwa wakijitoa kwa moyo wao wote kuitumikia nchi bila woga. Alihusika katika kesi kubwa kama mauaji ya watu waliokuwa wakichunwa ngozi mkoani Mbeya, wizi wa fedha za EPA, na matumizi mabaya ya ofisi ya umma.
Miongoni mwa kesi alizoshughulikia kwa zaidi ya miaka mitano ni kesi ya wizi wa Sh. bilioni 1.8 ya EPA, iliyomkabili Kada wa CCM Rajabu Maranda na Farijala Hussein, ambao walihukumiwa kifungo cha miaka mitano Mei 23 mwaka jana. Pia alisimamia kesi ya rushwa ya Sh. milioni 10 iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa mtangazaji wa TBC, Jerry Murro, ambaye alishinda kesi hiyo mwaka jana.
Alishiriki pia katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na mfanyabiashara Jayankumar Patel (Jeetu Patel) dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, DPP na Reginald Mengi, akitaka kufutiwa kesi zake nne za EPA. Boniface alimwakilisha AG na DPP na alishinda kesi hiyo.
Kesi nyingine kubwa alizokuwa akizisimamia hadi mauti zilikuwa kesi ya mauaji ya Ubungo Mataa inayoendeshwa na Jaji Projestus Rugazia, rufaa ya kupinga hukumu ya mfanyabiashara Naeem Gile kuhusu Richmond, na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayowakabili Basil Mramba, Daniel Yona, na Gray Mgonja.
Boniface alizaliwa Februari 21, 1968. Ameacha mke na watoto watatu. Alitimu shahada ya kwanza ya sheria mwaka 1995 na shahada ya pili mwaka 2008 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Julai 1, 1995, aliajiriwa rasmi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama Wakili wa Serikali. Oktoba 1, 2006, alipandishwa cheo na kuwa Wakili wa Serikali Mwandamizi, kisha Oktoba 1, 2007, akawa Wakili Kiongozi wa Serikali.
Kati ya 2003 na 2007, alikuwa Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Mkoa wa Mbeya. Mei 2007 hadi Oktoba 2010, alihudumu kama Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Kanda ya Mwanza. Novemba 2009 hadi Novemba 2010, alikuwa Mwanasheria Mfawidhi wa Serikali mkoani Dar es Salaam.
Kutokana na utendaji wake mzuri, Desemba 2010 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Uendeshaji Mashtaka na Msimamizi wa Kesi zenye Maslahi kwa Umma, hadi mauti yalipomkuta.
Bwana alitoa, na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima, Jumatatu, Mei 28, 2012.