Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Hi kidogo inatia mashaka na inaleta sintofahamu hasa kwa mahakama zetu na ofisi ya DPP, mtuhumiwa alihojiwa mbele ya wakili wake kuhusu makosa ya mtandao na kufungwa kwa maelezo. Lakini anatikishwa mahakamani kwa makosa ya kukwepa Kodi na kutakatisha fedha, je hizo fedha ametakatisha lini na kwanini hakuhojiwa kuhusu tuhuma hizo?
DPP Hadi anaandika hizi charge alisoma Nini Kama siyo maelezo ya mtuhumiwa? Kama maelezo ya mtuhumiwa hayana kipengele Cha kukwepa Kodi wala kutakatisha fedha kuna umuhimu gani wa watuhumiwa kuendelea kuhojiwa? Kwanini wasiwe wanakamatwa na DPP anawafungulia mashtaka anayohisi yanampendeza?
Kwa upande wa mahakama, watu wamejazwa magerezani kwa kunyimwa dhamana lakini bado tu mahakama haitaki kushtuka kutoka usingizini, watu wanateseka bila hata hatia huko magerezani kisa tu yupo mtu mmoja ambaye ofisi yake imeshindwa kusimamia haki na kuwalaza watu ndani huku yeye akilipwa mshahara na Kodi za wananchi.
Ifike mahali wasomi wetu mtambue kiwango kilekile mnachotumia kuwatesa waliowasomesha ndicho mtakachoteswa nacho ninyi na vizazi vyenu.
Mnamweka mtoto wa watu ndani huku mama yake mgonjwa akiwa anaangaika mkiamini kwamba mtafanikiwa ila mnachuma laana. Ipo siku damu na machozi ya Hawa mnaowatesa zitasimama Kati yetu ndipo mtatambua Bora kuishi bila kazi kuliko kutumia kazi yako kuwanyanyasa wengine.
Unahojiwa uraia unafunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi sijui utakatishaji fedha kweli? Kwamba utakatishaji fedha mliuona kwenye pasipoti yake au kwenye cheti chake Cha kuzaliwa?
No no no no no no no no, kuna watu wanatumika sivyo.