Wakili Albert Msando,kulikuwa na haja kweli?

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,524
2,000
Nikiri kuwa tangu jana kumekuwa na mjadala juu ya alichokisema Wakili Msomi Albert Msando pale Serena Hotel. Moderators, naomba msiutoe wala kuunganisha uzi huu.Ni kwasabu una mtazamo tofauti.

Wakili Msando, ulitangaza kuwa kutakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari pale Serena Hotel. Siku ilipotimu,waandishi na wasio waandishi wakaja kukusikiliza. Ukajitokeza kama Wakili wa akina-Zitto Kabwe. Ukatoa taarifa. Naiona Taarifa yako kama taarifa tata kwakuwa ina mchanganyiko usio rasmi na ambao haukutegemewa.

Kwanza, taarifa yako imebeba 'taarifa kwa umma'. Kwamba, Zitto Kabwe na wenzake,badala ya kujibu tuhuma zao 11 walizopewa na chama chao, wao wameamua kukata rufani kwenda Baraza Kuu la CHADEMA.

Pili, taarifa yako imebeba 'rufani'. Umeainisha sababu kuu mbili za rufani ya akina-Zitto. Ukazikoeza sababu hizo kwa kutaja vifungu mbalimbali vya Katiba ya CHADEMA.

Tatu, taarifa yako inabeba 'utetezi'. Baada ya kuainisha sababu za rufani na vifungu vyake,ukaenda mbele zaidi na kuwsilisha utetezi wa Zitto juu ya tuhuma zinazomkabili. Kuna mahali umesema: 'ZITTO HAUSIKI'. Eti kwakuwa hajatajwa moja kwa moja na Waraka. Kimsingi, huu ni utetezi.

Nne, taarifa yako ikabeba 'kanusho' . Tena ni kanusho lililotokana na habari za sikia-sema (hearsay). Ukakanusha kuhusu kuhusika kwa Zitto kwa vurugu za Kigoma. Kwamba, hausiki na kupigwa mawe Dr.Slaa,Katibu Mkuu wa CHADEMA. Wakili Msomi mwenzangu MsandoAlberto, hujui uzito wa sikia-sema? Wewe ulikuwepo Kigoma wakati Dr.Slaa anapigwa mawe? Kuwa makini Wakili Msomi.

Tano, taarifa yako imebeba 'malalamiko'. Mwanzo hadi mwisho wa taarifa yako ya Serena ni kulalamika tu. Umelalamikia utaratibu,sababu,maneno yasemwayo na kadhalika.

Je, kulikuwa kweli na haja ya kuitisha mkutano Serena na kutoa 'mchanganyiko' huu? Wakili msomi wenzangu MsandoAlberto, tafadhali washauri wateja wako wafuate taratibu za chama chao. Acheni sarakasi zisizo na tija. Mnaweza kuwa mna hoja.Lakini, mnaweza kuiharibu kwakuwa mnapoitolea hapastahili. Kwa hili la sasa, si umma wala vyombo vya habari vinavyoweza kuwa msaada wenu. Msaada pekee mlionao ni Katiba yenu.

Si busara kutoa kila mchakato wa ndani ya chama nje. Msipokuwa makini,mtachokwa na kuhukumiwa kwa jazba na hasira ya viongozi wenu. Watasema:'liwalo na liwe' . Msifike huko. Hakuna haja ya mambo hayo!
 
usungilo

JF-Expert Member
Aug 9, 2012
527
500
Mimi naamini Zitto anahusika kuihujumu CHADEMA.! Yeye kila jambo anakimbilia kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Hata rumours yeye anataka kuzijibu! Kuna mambo mengine ni kuyapeleka kimya kimya mpaka matokeo ndo yataleta majibu ya ukweli.! @zito jaribu kukaa kimya vinginevyo utaendelea kulaumiwa kuhusu kuhujumu chama.
 
Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,110
2,000
Ushahidi upo unaoonyesha kwamba Zitto alishiriki kuandaa huo waraka, asubiri atakapokuwa mbele ya CC ndio atakaposhtushwa kwa mara nyingine.
 
Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,110
2,000
Mkuu kama ni kweli hili basi ni habari njema mnoo kwangu mie ndg yako! Mungu akutie nguvu.

Toa hofu, kama wanafikiri tundu lissu kuandaa mashtaka vague namna ile ni makosa ya kiufundi, watatoka mbele ya pilato siku hiyo nguo zimelowa.

Juzi tundu lissu amesema wazi zaidi, kwamba Zitto Kabwe alikuwa nyuma ya mkakati wa kukichora chama chake na rangi ya ugaidi, upo ushahidi upo, lakini hiyo haijafanywa kama sababu ya kumshughurikia.
 
Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,413
2,000
Mie nashauri urgent measures zichukuliwe haraka kwani kama makosa tayari wanajua walikosea na kama kotimuliwa pia wanajua wanatimuliwa,wanachofanya hapa ni timing,wanadelay mambo ili wapate nafasi ya kuendelea kudestabilise na kuharibu composure ya chama kwa ujumla kwani wao wanajua hawana tena cha kupoteza,washaamua liwalo na liwe ...nashauri waondolewe haraka kama ni saga bora lihamie mahakamani kuliko kuwaacha waendelee kuwa ndani ya chama
 
BigMan

JF-Expert Member
Feb 19, 2007
1,096
1,195
Mimi naamini zito anahusika kuihujumu chadema.! Yeye kila jambo anakimbilia kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Hata rumours yeye anataka kuzijibu! Kuna mambo mengine ni kuyapeleka kimya kimya mpaka matokeo ndo yataleta majibu ya ukweli.! @zito jaribu kukaa kimya vinginevyo utaendelea kulaumiwa kuhusu kuhujumu chama.

kuna tatizo kubwa ya idadi kubwa ya jamii yetu sasa hivi kuzichukuwa fununu kama ukweli na nyingi zimekuwa zikipitishiwa katika vyombo vya habari,hivyo ukizushiwa kitu chochote na ukanyamaza kimya basi jamii inaamini ni kweli.Kwa mtazamo wangu anachofanya ZZK ni sahihi vinginevyo akinyamaza kimya itaonekana ni kweli,mfano mpaka sasa kupitia mikutano ya waandishi wa habari ya viongozi wa chadema kuhusiana na sakata hilo,tayari baadhi ya wanachama wa chama hicho wanaamini ni kweli sasa yeye kama mwanasiasa ina muathiri ni lazima ajibu kupitia njia ile ile na sasa inatakiwa kufanya naye mikutano ya hadhara.Lakini mimi kwa mtazamo wangu ingekuwa vyema kwa kamati kuu ya chadema baada ya kufikia maamuzi ya kumvua madaraka isingetoa ama kuitisha press conference mpaka pale hatua ya mwisho kabisa itakapofikiwa
 
Issue ya Zitto ni fununu? Hajalimwa barua? hajajibu?
 
BigMan

JF-Expert Member
Feb 19, 2007
1,096
1,195
Issue ya Zitto ni fununu? Hajalimwa barua? hajajibu?

Twende katika pande mbili za mgogoro huo,soma vizuri majibu ya wakili wake na ukiwa katikati ya pande mbili hizo utabaini bado ni fununu haijarishi kama barua zimetoka ama laa,lugha rahisi bado ni tuhuma na ndiyo maana kwa mtazamo wangu nikasema kamati kuu ingekaa kimya hadi mwisho wa jambo hilo.
 
Albert Msando

Verified Member
Nov 2, 2010
1,019
0
Wakili Msomi Petro,

Kwanza nashukuru kwa maswali yako na pia kuepusha Uzi huu na hayo mengine huko.

1. Taarifa ya jana haikuwa rufaa. Ni taarifa ya nia ya Zitto kukata Rufaa Baraza Kuu dhidi ya adhabu ya kuvuliwa nafasi zake za uongozi. Ni taarifa ya nia na sababu za nia hizo. Sababu kwa nini ameamua kukata Rufaa sio utetezi.

2. Sikia-sema ya yaliyotokea kigoma umechanganya Wakili. Nilichosema ni kwamba Zitto hausiki na matukio hayo. Sijasema kwamba Matukio hayo hayakutokea kwa sababu sikuwa kigoma. Vile vile basi nisiseme yametokea kwa sababu sikuwepo pia.

3. Kwa ilipofikia Zitto atasubiri barua ya maamuzi rasmi ya Kamati Kuu ili aweze kuchukua hatua kwa mujibu wa Kanuni. Pia atasubiri maamuzi ya Kamati Kuu baada ya utetezi wake kwa nini asivuliwe uanachama.

Ahsante.
 
kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,728

Kwa hiyo kwa hiki ulichokiandika unamaanisha hata wakati ule Nyerere alitakiwa asubiri hadi mwisho ndipo aje kuwakamata akina Tamim, Macgee, Rugangira, Maganga na wale wengine waliokuwa wamepanga Kumpindua je kusubiri huku kungemuokoa yeye kutoPinduliwa?
 
Mwangendage

Member
Jan 11, 2012
69
70
Kwa hiyo kwa hiki ulichokiandika unamaanisha hata wakati ule Nyerere alitakiwa asubiri hadi mwisho ndipo aje kuwakamata akina Tamim, Macgee, Rugangira, Maganga na wale wengine waliokuwa wamepanga Kumpindua je kusubiri huku kungemuokoa yeye kutoPinduliwa?
Kuhusisha issue ya akina Zitto Chadema na Uhaini uliotokea wakati nyerere akiwa rais ni utovu wa nidhamu
 
kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,728
2,000
Wakili Msomi Petro,

Kwanza nashukuru kwa maswali yako na pia kuepusha Uzi huu na hayo mengine huko.

1. Taarifa ya jana haikuwa rufaa. Ni taarifa ya nia ya Zitto kukata Rufaa Baraza Kuu dhidi ya adhabu ya kuvuliwa nafasi zake za uongozi. Ni taarifa ya nia na sababu za nia hizo. Sababu kwa nini ameamua kukata Rufaa sio utetezi.

2. Sikia-sema ya yaliyotokea kigoma umechanganya Wakili. Nilichosema ni kwamba Zitto hausiki na matukio hayo. Sijasema kwamba Matukio hayo hayakutokea kwa sababu sikuwa kigoma. Vile vile basi nisiseme yametokea kwa sababu sikuwepo pia.

3. Kwa ilipofikia Zitto atasubiri barua ya maamuzi rasmi ya Kamati Kuu ili aweze kuchukua hatua kwa mujibu wa Kanuni. Pia atasubiri maamuzi ya Kamati Kuu baada ya utetezi wake kwa nini asivuliwe uanachama.

Ahsante.

1.Hapo nilipoweka BLUE nafikri bado unaendelea kuonyesha upeo mdogo, unaposema Zitto hausiki sijui kama una ushahidi juu ya hii kauli yako kwani tukumbuke matukio ya fujo hizi na katika mabango yaliyobebwa na wale vijana Hatuja ona jina la Mwigamba wala Kitila sasa tujiulize why? na je kuna tamko lolote kutoka ndani ya Chama (CDM) lililosema Zitto anahusika? kama hakuna tamko inakuwaje wewe na mteja wako uje na kanusho?

2. Wewe tunasikia ni wakili wa Zitto, Mwigamba na Kitila Mkumbo lakini katika maelezo yako ya jana umejikita zaidi kumtetea Zitto napenda kujua ni kwa nini unamtetea Zitto pekee na haukutoa maelezo yeyote juu ya Mwigamba na Kitila au unapanga siku nyingine kuita waandishi kwa ajili ya kuelezea juu ya hawa wengine?

3. Mwigamba alikuwepo kilichonishangaza alichoongea ni tofauti na dhumuni la mkutano ule ambao nafikiri wewe ndio ulikuwa kinara wake na kutofikiria hilo Mwigamba akapoteza dhima nzima ya kikao kile.
 
kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,728
2,000
Kuhusisha issue ya akina Zitto Chadema na Uhaini uliotokea wakati nyerere akiwa rais ni utovu wa nidhamu

Tambua uhaini ni sehemu yeyote iwe kwenye vyama vya siasa, na hata katika familia unaweza kuta watoto wanampindua baba yao na kumuua na kurithi mali hayo pia ni mapinduzi.
 
Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,524
2,000
Wakili Msomi Petro,

Kwanza nashukuru kwa maswali yako na pia kuepusha Uzi huu na hayo mengine huko.

1. Taarifa ya jana haikuwa rufaa. Ni taarifa ya nia ya Zitto kukata Rufaa Baraza Kuu dhidi ya adhabu ya kuvuliwa nafasi zake za uongozi. Ni taarifa ya nia na sababu za nia hizo. Sababu kwa nini ameamua kukata Rufaa sio utetezi.

2. Sikia-sema ya yaliyotokea kigoma umechanganya Wakili. Nilichosema ni kwamba Zitto hausiki na matukio hayo. Sijasema kwamba Matukio hayo hayakutokea kwa sababu sikuwa kigoma. Vile vile basi nisiseme yametokea kwa sababu sikuwepo pia.

3. Kwa ilipofikia Zitto atasubiri barua ya maamuzi rasmi ya Kamati Kuu ili aweze kuchukua hatua kwa mujibu wa Kanuni. Pia atasubiri maamuzi ya Kamati Kuu baada ya utetezi wake kwa nini asivuliwe uanachama.

Ahsante.
Maswali yangu bado yapo pale pale Wakili Msomi mwenzangu MsandoAlberto.Kwanza, kulikuwa na haja kweli ya mkutano ule? Pili, kwanini umechanganya mambo mengi yasiyoendana pamoja?
 
Last edited by a moderator:

Ben Saanane

Verified Member
Jan 18, 2007
14,594
2,000
Wakili Msomi Petro,

Kwanza nashukuru kwa maswali yako na pia kuepusha Uzi huu na hayo mengine huko.

1. Taarifa ya jana haikuwa rufaa. Ni taarifa ya nia ya Zitto kukata Rufaa Baraza Kuu dhidi ya adhabu ya kuvuliwa nafasi zake za uongozi. Ni taarifa ya nia na sababu za nia hizo. Sababu kwa nini ameamua kukata Rufaa sio utetezi.

2. Sikia-sema ya yaliyotokea kigoma umechanganya Wakili. Nilichosema ni kwamba Zitto hausiki na matukio hayo. Sijasema kwamba Matukio hayo hayakutokea kwa sababu sikuwa kigoma. Vile vile basi nisiseme yametokea kwa sababu sikuwepo pia.

3. Kwa ilipofikia Zitto atasubiri barua ya maamuzi rasmi ya Kamati Kuu ili aweze kuchukua hatua kwa mujibu wa Kanuni. Pia atasubiri maamuzi ya Kamati Kuu baada ya utetezi wake kwa nini asivuliwe uanachama.

Ahsante.

Barua gani rasmi kutoka kamati kuu?
 
Hivi Msando jana ulikuwa unaongea na waandishi wa habari kama nani? Kama Msemaji wa MMs au kama Mwanasheria? Mi huwa najua wanasheria ni kwa ajiri ya mambo ya Kimahakama, mahakama ilihamia serena?

Alafu swala zima la fee, nani anasettle?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom