Wakiingia madarakani, wananchi tunageuka kuwa maadui zao, na wanajilinda dhidi yetu, kwanini?

Sidhani kama kila mtu humu anamfahamu huyo Mwakasege, au kila mtu anafuatilia mafundisho yake. lakini bila shaka ninge pingana naye vile vile, kwa muktadha huo. Unaposema cheo/madaraka ndio kinalindwa/hilindwa hata sielewi na haileti maana kabisa, Nikikuuliza unakilinda cheo dhidi ya nani? Kama uliomba lidhaa ya wananchi uwaongoze wakakubali, na ukawa kiongozi wao, kwanini ukilinde hicho cheo au hayao madaraka? umepewa dhamana uitumikie siyo mali yako binafsi hadi uilinde. Cheo ukiteuliwa, pia nidhamana umepewa ili utumike kwenye nafasi hiyo, au madaraka umekabidhiwa uyatumikie kwa nafasi hiyo, sasa unayalinda dhidi ya nani, aliyekuteua asikunyang'anye au WANANCHI AMBAO HAWAKURIDHIA UTEUZI WAKO WASIKUNYANG'ANYE?
Unalinda cheo au madaraka? kwanini? kama yametoka kwa mungu kwanini usitegemee ulinzi wa huko mbinguni? au Mungu alikileta bila ulinzi sasa wewe unakianzishia ulinzi kidumu mwilini mwako?
Any way labda ungeeleza zaidi huyo mtumishi Mwakasege alimaanisha nini kulinda cheo au madaraka ningekuelewa, lakini sielewi kwa uchache wa maelezo yako, hainipi maana ya kunifanya nielewe.
Ni kweli kwamba mamlaka ziliwekwa na Mungu lakini "wenye mamlaka" hata shetani anaweza kupenyeza wa kwake.
 
Ni kweli kwamba mamlaka ziliwekwa na Mungu lakini "wenye mamlaka" hata shetani anaweza kupenyeza wa kwake.
Hahaha huyu shetani ndiye anayewatishia maisha yao?! Kwanini wanatuogopa sisi, au tunafanana na huyo shetani? Hivyo kuwafanya wasitambue nani shetani miongoni mwetu?!
 
Hawa watawala waajabu sana, wanatoka miongoni mwetu, lakini wakiishaanza kutawala sisi ndiyo tunakuwa maaadui zao wanalindwa dhidi yetu.
Huu uadui huwa unaanza lini na kwanini iwe hivyo?!

Wanakuja kwetu wanalindwa kwa bunduki za moto, hawataki kuwa karibu na watawaliwa, eti wanahofia usalama wao.

Na hili linaendelea hata wakistaafu, au kuondoka madarakani. Ni lini tunawatisha, ni lini tunatisha hadi wajilinde dhidi yetu wananchi?!

Wengine wanateuliwa lakini nao wanalindwa kweli kweli, adui yao ni sisi hawa hawa kweli au ni mwingine?!

Humo barabarani wanapita kwa kasi hadi kutishia usalama wetu, huwa wanafukuzwa na nani, au wanamkimbia nani?!

Sisi hatulindwi na sisi ndio tunalipa kodi, wao wakianza kutawala kodi wanaacha kulipa, kila kitu bure hata ulinzi wao tunaulipia sisi, na ni sisi wabaya wao tunalipia usalama wao tusiwadhuru, huwa sielewi hili.

Huwa na jaribu kuelewa ni lini huwa tunaanza kuwa tishio kwao, au ni wakati gani.

Kwanini wanatuogopa?!

Huwa najiangalia kwenye kioo sitishi kihiivyo, na nikiwaangalia wananchi wenzangu hawatishi kiiivyo, lakini watawala wanatuogopa, kwanini?!.

Haka ka video ni nyongeza

Jiulize kwa nni ukiwa huna kitu kapuku unatembea kila kona na masaa yoyote kwa miguu, ila ukiwa na pesa don unaanza kuchukua na mabastora mara bodyguard pia badhi ya sehem hutaki kwenda, kwa uoga wa maisha yako au kwa kudhalau kuwa sio hadhi yako wakati zamani vilukuwa viwanja vyako?, tafakari pia
 
Jiulize kwa nni ukiwa huna kitu kapuku unatembea kila kona na masaa yoyote kwa miguu, ila ukiwa na pesa don unaanza kuchukua na mabastora mara bodyguard pia badhi ya sehem hutaki kwenda, kwa uoga wa maisha yako au kwa kudhalau kuwa sio hadhi yako wakati zamani vilukuwa viwanja vyako?, tafakari pia
Hawa hulinda pesa na mali zao. Status zao wanajipa hazina maana yoyote, kuja maeneo yetu wanaweza kuja na pesa zao na wakaondoka bila kudhurika. Kama wanaona sisi ni hatari kwa usalama na afya zao kwanini wanakuja huku?! Kwanini wasikae huko huko masaki kama huko ndio salama?!
 
Back
Top Bottom