StudentTeacher
JF-Expert Member
- Jan 30, 2019
- 3,679
- 3,719
Ni kweli kwamba mamlaka ziliwekwa na Mungu lakini "wenye mamlaka" hata shetani anaweza kupenyeza wa kwake.Sidhani kama kila mtu humu anamfahamu huyo Mwakasege, au kila mtu anafuatilia mafundisho yake. lakini bila shaka ninge pingana naye vile vile, kwa muktadha huo. Unaposema cheo/madaraka ndio kinalindwa/hilindwa hata sielewi na haileti maana kabisa, Nikikuuliza unakilinda cheo dhidi ya nani? Kama uliomba lidhaa ya wananchi uwaongoze wakakubali, na ukawa kiongozi wao, kwanini ukilinde hicho cheo au hayao madaraka? umepewa dhamana uitumikie siyo mali yako binafsi hadi uilinde. Cheo ukiteuliwa, pia nidhamana umepewa ili utumike kwenye nafasi hiyo, au madaraka umekabidhiwa uyatumikie kwa nafasi hiyo, sasa unayalinda dhidi ya nani, aliyekuteua asikunyang'anye au WANANCHI AMBAO HAWAKURIDHIA UTEUZI WAKO WASIKUNYANG'ANYE?
Unalinda cheo au madaraka? kwanini? kama yametoka kwa mungu kwanini usitegemee ulinzi wa huko mbinguni? au Mungu alikileta bila ulinzi sasa wewe unakianzishia ulinzi kidumu mwilini mwako?
Any way labda ungeeleza zaidi huyo mtumishi Mwakasege alimaanisha nini kulinda cheo au madaraka ningekuelewa, lakini sielewi kwa uchache wa maelezo yako, hainipi maana ya kunifanya nielewe.