Wakenya wachukizwa na Ngugi kwa kuendeleza Ukabila huko Catalonia

joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
26,117
46,613
Ngugi should have spoken in Kiswahili when taking prize
Kitendo cha Prof. Ngugi wa Thiong'o kutumia lugha ya Gikuyu wakati akipokea tuzo huko Catalonia kimeendelea kushutumiwa na wakenya mbalimbali na kuelezewa kama sehemu ya kuendeleza ukabila ambao umekua ni tatizo kubwa na lakudumu linaloisumbua Kenya.

Jambo la kushangaza na kusikitisha ni kuona baafhi ya wakenya hapa JF walipongeza kitendo hicho hatari akichokifanya Prof. Ngugi ambaye ni miongoni mwa waasisi wa tatizo la ukabila linaloisumbua Kenya.
 
Emancipate yourself from mental slavery
 
akili ya wa kenya ni moja,akiwa Raila au Kitovu Gimanyara wote sawa ukabila tu
 
Ngugi should have spoken in Kiswahili when taking prize
Kitendo cha Prof. Ngugi wa Thiong'o kutumia lugha ya Gikuyu wakati akipokea tuzo huko Catalonia kimeendelea kushutumiwa na wakenya mbalimbali na kuelezewa kama sehemu ya kuendeleza ukabila ambao umekua ni tatizo kubwa na lakudumu linaloisumbua Kenya.

Jambo la kushangaza na kusikitisha ni kuona baafhi ya wakenya hapa JF walipongeza kitendo hicho hatari akichokifanya Prof. Ngugi ambaye ni miongoni mwa waasisi wa tatizo la ukabila linaloisumbua Kenya.
Wapumbavu in large numbers hua wanafanya vitu vya kipumbavu sana

Kikuyu ni lugha yake,aongee Kichina,Kizaramo,etc ni lugha its fvcking his business...

Ni personal choice acheni upumbavu....

Angeongea Kingereza msingeongea huu upumbavu....Kaongea Kikuyu then the whole dumb population goes ballistic!

Ukabila ni nini?

Ukabila ni kutokuongea Kiswahili?Ila kuongea Kingereza sio ukabila?Stupid people
 
Hao ni wakenya wenzako ndio wanaosema anaendeleza ukabila kwa kutumia Gikuyu katika International platforms, huko alipaswa kutumia International languages ikiwemo Kiswahili

Sasa unaweza kuona ni kwakiasi gani wakenya ukabila unavyojijenga?, kwa hiki kitendo alichokifanya Ngugi, tayari kimewagawa wakenya, wengi wameandika " Let's emphasize things that unite us", hii pekee ni sababu tosha ya wakenya kuacha kutumia lugha za makabila yenu katika maeneo ambako kuna watu kutoka makabila mbalimbali.

Lazima mkubali kwamba kuna baadhi ya mambo yakifanyika katika public areas yanawagawa watu, hata kama hayo mambo ni tamaduni au ni dini zetu. Lugha ni kitu muhimu Sana katika kuwaunganisha watu kama kikitumika vizuri. Lugha ni kichocheo muhimu sana cha ukabila kama ilivyo Kenya. Uchaguzi ni wenu, kukumbatia lugha zenu, au kuachana na Ukabila.
 
Wapumbavu in large numbers hua wanafanya vitu vya kipumbavu sana

Kikuyu ni lugha yake,aongee Kichina,Kizaramo,etc ni lugha its fvcking his business...

Ni personal choice acheni upumbavu....

Angeongea Kingereza msingeongea huu upumbavu....Kaongea Kikuyu then the whole dumb population goes ballistic!

Ukabila ni nini?

Ukabila ni kutokuongea Kiswahili?Ila kuongea Kingereza sio ukabila?Stupid people
Mimi nimependa tu alivosema, wakenya wachukizwa.. kisha povu lake akaliambatanisha na maoni ya mkenya mmoja.
 
Kuna articles Kama tano zote za Kenya zimelizungumzia hili kwa hasira Sana, ingia Google Search, weka heading ya hiyo article uone jinsi wakenya walivyochukizwa na Ngugi
 
Ngugi wa thiong'o vitabu zake nyingi ni kwa lugha ya kikuyu. Tuzo alipewa ni ya vitabu zake. Swahili pia lugha ya kabila ya waswahili, ingwa inatumikiwa kama lugha rasmi ya kenya na tanzania.

Mswahili,bajuni ama mijikenda?
 
Jaribu kusoma hiyo article uone jinsi anavyolaumiwa kwa kuendeleza ukabila Kenya. Hakuna tuzo ya Vitabu duniani, hiyo tuzo ya Catolania inatolewa kila mwaka kwa watu wenye kufanya juhudi za kuhifadhi utamaduni na urithi wa asili, yeye ni mtu wa 31 kupewa, japo kuna watu wanaipinga hiyo tuzo kwasababu hilo jimbo la Catolania linataka kujitenga kwa misingi ya ukabila.
 
Hio ni opinion ya huyo mjinga aliyeandika hio nakala akimkejeli Ngugi kwa kutumia lugha yake asili. Kiswahili sio lugha asili ya mtu yeyote isipokuwa waswahili wenyewe. Hata mimi nikitaka naweza kuandika nakala kwa gazeti nikimpongeza Ngugi kwa kutumia lugha yake ya mama. Opinion ya Mkenya mmoja au hata watano bado ni opinion tu. Kuna wakenya wengi tu wanaomsupport Ngugi hata Wakenya ambao sio Wakikuyu. Huu upuzi wa watu kujifanya eti Kiswahili ndio lugha pekee ya waafrika wa Afrika Mashariki lazima ikome. Lazima tuheshimu lugha zetu zote na hatuwezi kudharau lugha zetu za asili eti kwa sababu Watanzania wanadhani kuwa lugha hizo ni takataka. Sisi tunaheshimu lugha zote za kiafrika sio kiswahili tu. Halafu hio kiswahili hata sio ya kiafrika sana kwa sababu imesheheni maneno mengi ya kiarabu. Kiswahili chenyewe pengine asilimia arubaini ni maneno ya kiarabu. Sasa sijui ni nini inakufanya uchukie lugha yako ya asili halafu ukipende kiswahili ambacho ni nusu bantu nusu kiarabu. Hiyo ni hypocrisy.
 
Off point, tatizo lenu wakenya hampendi kujifunza kwa waliofanikiwa kutokana na kiburi chenu cha kujifanya mnajua kila kitu.

Hakuna ubishi kwamba Tanzania tumefanikiwa kutokomeza ukabila, Hakuna ubishi kwamba kwa kutumia lugha moja ya Kiswahili nchi nzima, ni miongoni mwa sababu kubwa katika kutokomeza ukabila, kwanini msiige hilo?.

Nani aliyesema Tanzania tunadharau lugha za asili?, humsikii Magufuli akizungumza baadhi ya maeneo, kama tungekua tunazidharau asingezungumza.

Huko vijijini huwa tunazungumza lugha zetu kwasababu zaidi ya 98% ya wakazi huko vijijini wanaelewa hiyo lugha, kwahiyo hakuna hatari ya watu kujitenga kutokana na "language barrier".

It is very uncivilized" kuzungumza lugha ambayo nusu ya watu waliopo hawaelewi hiyo lugha, hasa katika ofisi za serikali na public places. Hivi kweli unaingia ofisini au Hospitalini unakuta Daktari mkikuyu anazungumza Gikuyu na baadhi ya Nurses ambao ni wakikuyu, Daktari mjaluo anazungumza Kijaluo na Nurses wa kijaluo, eti kwasababu wanalinda Mila na desturi zao, Nonsense.

Kuhusu wanaoandika kumkashifu Prof. Ngugi, muhimu sio idadi ya watu wangapi wameandika, muhimu ni kilichoandikwa, ukisoma wote walioandika wanazungumzia umuhimu wa Lugha katika kuunganisha nchi.

Unapozungumza lugha inayoeleweka na watu wengi, kunasaidia kuunganisha jamii, lakini unapotumia lugha ya jamii moja na kuacha kundi kubwa, huko ni kutenga na kuigawa jamii husika.

Umuhimu wa Kiswahili ni
1)Ndio lugha inayoeleweka kwa watu wengi zaidi Kenya
2)Hakuna kabila lolote katika Afrika au Kenya ambalo linahodhi au kumiliki Kiswahili

Kwahiyo Kiswahili kinaunganisha watu wa Kenya na kinaeleweka kwa wakenya wengi bila kujali makabila yao.

Tumieni Kiswahili ili kuleta wakenya pamoja na kupambana na ukabila. Acheni kuendekeza ukabila kwa kisingizio cha kulinda mila na desturi, huo ni upumbavu na ni hatari Sana.
 
Back
Top Bottom