Shida inakuja kutafsiri neno "kutia" , neno la kawaida na kugeuzwa kuwa na maana moja tu. Utasikia mtu akinena "niwekee chai kwenye kikombe " ambapo kimantiki haiyumkini, kuweka kiuhalisia ni sehemu tambarare , je kikombe / bilauri havina shimo ? Kwa nini tusirudie kusema " nitilie maji mwenye bilauri / kikombe ?"