Wakazi Wa USA river wasikitishwa na uzembe wa polisi

mgeni wenu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
3,664
1,730
Kwa nyakati tofauti Wakazi wa Arumeru Mashariki wameskitishwa kwa Watuhumiwa wa Mauaji ya Mwenyekiti wa CHADEMA kutoroka polisi,mzee mmoja kada maarufu wa CCM aliyejitambulisha kwa jina moja la Maeda akitokea Magadirisho amelaani kitendo cha polisi kuwaachia watuhumiwa na baadae kutangaza kuwa wametoroka,amesema kitendo hicho kinakiweka chama cha mapinduzi mahala pabaya maana toka mwanzo wauaji walilalamikiwa kuwa ni wafuasi wa CCM,na nivizuri wakamatwe na wahukumiwe mara moja maana polisi wanajua walipo alisema
Juhudu za kumtafuta mbunge wa jimbo hilo Joshua Nassari hazikuzaa matunda baada ya simu yake kuita bila kupokelewa
 
Kwani waliomtuma kuuwa si viongozi wa ccm!, we ulitegemea nini hapo, ccm ndo walivyo na nikawaida yao kufanya njama hizo.
 
Mkuu hilo siyo swala la wakazi wa USA linagusa nchi nzima na linatuachia maswali mengi kuhusu Jeshi letu na Polisi na vyombo vya usalama pia.
 
Hawa wameachiwa kwa kazi maalum. Kampeni za udiwani Arusha zinaanza leo rasmi.

Hawa wametumwa kutishia ama kuua kabisa tena. They got none to loose. Kwa wanaomjua Sam (mmoja wa aletoroka) watakubaliana na hili.
 
hii nchi yaani polisi ni kama polisher ya ccm na wala si walinda haki na amani ya nci inasikitisha sana kuendelea kunyanyasa wananchi tukisema tunapolisi kumbe ccm polisher
 
Wale wametoroshwa maana wangemtaja mhusika ingekuwa noma yaani hasi hapo serikali inahusika

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Kwa nyakati tofauti Wakazi wa Arumeru Mashariki wameskitishwa kwa Watuhumiwa wa Mauaji ya Mwenyekiti wa CHADEMA kutoroka polisi,mzee mmoja kada maarufu wa CCM aliyejitambulisha kwa jina moja la Maeda akitokea Magadirisho amelaani kitendo cha polisi kuwaachia watuhumiwa na baadae kutangaza kuwa wametoroka,amesema kitendo hicho kinakiweka chama cha mapinduzi mahala pabaya maana toka mwanzo wauaji walilalamikiwa kuwa ni wafuasi wa CCM,na nivizuri wakamatwe na wahukumiwe mara moja maana polisi wanajua walipo alisema
Juhudu za kumtafuta mbunge wa jimbo hilo Joshua Nassari hazikuzaa matunda baada ya simu yake kuita bila kupokelewa
Haya mambo hayana tofauti na Muvi nyingine za polisi za siku za nyuma. Tujiulize ile muvi ya Kova na yule chizi Mkenya, kuhusiana na sakata la kutekwa kwa Dr Ulimboka, imeishia wapi? Tujiulize Tume zote zilizoundwa, kuanzia mauaji ya wale watu watatu Arusha, kwenye maandamano ya CDM mwaka jana. Tume ya Ally Zona aliyeuawa pale Msamvu-Morogoro, Tume ya Mwangosi, zote hizo, majibu yake yako wapi? Ni dhahiri ni vigumu Tume hizo kutoa majibu, kwa kuwa yaliyogundulika kwenye uchunguzi wa Tume hizo, kama taarifa hizo zitatolewa hadharani zitawavua nguo watawala!!
 
Ni vigumu sana sisi wananchi kurudisha imani kwa jeshi letu la POLISI sababu wanatumika vibaya kwa maslahi ya kisiasa na kuacha kusimamia usalama wa raia kwa haki. Kuna haja ya kufanya restructuring ya jeshi zima la polisi ili liweze kutekeleza majukumu yake kama inavyopaswa.
 
Back
Top Bottom