BVR 2015
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 229
- 413
Wakazi wa mji mdogo wa Mikumi katika mkoa wa Morogoro,wametishwa na uongozi wa Serikali ya mji huo kuwa watakamatwa pale watakapobainika kuwa hawajachangia kiasi cha Tsh. 5,000/= kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.
Uongozi wa mji kupitia gari la matangazo walikuwa wanawatangazia wananchi popote wanapotembea waakikishe wawe wamebeba risiti walizolipia ili wasikamatwe na jeshi la akiba.
Katika kikao walichoketi viongozi, wakiwepo madiwani na mbunge wa jimbo la mikumi ndugu Londa,wananchi walihoji huo uhalali wa kutoa michango wakati kipindi cha kampeni walinadi sera kuwa elimu itakuwa ni bure, pia wananchi waliwauliza hao madiwani na mbunge je wao tayari wameshachangia huo ujenzi? na wamechangia kiasi gani? Jibu alilotoa mbunge ni kwamba hataki maswali ya kelele kelele.