Wakazi wa Mbweni Mpiji hatuna imani na Paul Makonda

fishseller

Member
Jun 13, 2012
30
19
Kwa kipindi kirefu sasa, wakazi wa Mbweni Mpiji iliyoko manispaa ya Kinondoni tumekuwa na matatizo mbalimbali ambayo serikali ya wilaya na mkoa wameshindwa kushirikiana na wananchi ili kusaidia kutatua matatizo hayo.

Mojawapo ya matatizo matatu tuliyonayo yaliyodumu kwa kipindi kirefu ni magari makubwa yanayotumika kusomba mchanga kutoka mto Mpiji na kupita kwa kasi kwenye makazi ya watu na kusababisha ajali.

Pia magari hayo yamepelekea kwa mmonyoko mkubwa wa ardhi na uharibifu wa miundombinu kwenye maeneo mengi ya Mbweni Mpiji. Miundombinu hiyo inajengwa kwa kutumia pesa za walipa kodi wan chi hii.

Baada ya tangazo la kuzuia magari hayo kusomba mchanga kutolewa na serikali mapema mwaka jana, magari ya polisi yalianza kufanya doria usiku na mchana ili kuzuia magari hayo yasiendelea kusomba mchanga huyo.
Hata hivyo, wakazi wa Mpiji tunasikitika kuwa polisi hao wametumia mwanya huo kuomba rushwa kutoka kwa madreva na wamaili wa malori na kuwaruhusu kuendelea na shughuli za uharibifu wa mazingira.

Baadhi ya madreva wamesikika wakitamba kuwa hakuna mtu wa kuwafanya chochote kwakuwa malori mengi yanamilikiwa na watu wenye nafasi kubwa serikalini na hakuna mtu yoyote anayeweza kuwagusa.

Tatizo la pili ni magendo kutoka Zanzibar kupitia bandari bubu ya Mbweni Maputo.

Kambi ya jeshi iliweka kizuizi ili magendo isipitie lakini wanaofanya biashara hiyo walibadilisha njia na kutumia njia nyingine ambayo polisi wanaofanya doria wamekuwa wakiwasubiri, kupokea rushwa na kuyaruhusu magari hayo kuendelea na safari.

Baadhi ya maafisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania wamekuwa wakishirikiana na askari polisi kupokea rushwa kutoka kwa wafanyabiashara hao.

Jambo lingine linalowasikitisha wakazi wa Maputo ni kwamba bandari inayotumika kupitisha magendo ipo mita chache kutoka chuo cha Usalama wa Taifa ambako wanafunzi na wakufunzi wanaiona biashara haramu ikiendelea bila wao kufanya chochote.

Tunasikitika kuona kuwa katika zama hizi za rais Magufuli ambaye alitoa ahadi kwa wapiga kura kwamba mambo haya hayawezi kuendelea kutokea nchi lakini yanaendelea kufanyika wakati watu wenye mamlaka ya kuzuia uharifu huu wakishirikiana na waarifu.

Mheshimiwa Makonda alipata sifa kubwa wakati akiwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kutokana na utendaji wake mzuri lakini matatizo haya aliyafumbia macho mbali na ukweli kwamba alikuwa na taarifa.

Tatu, Mbweni Mpiji ni eneo la mji mpya ambapo viwanja vyote waligawiwa kwa wananchi baada ya kupimwa na serikali. Hata hivyo, maeneo mengi bado hayajaunganishwa na maji ya Dawasco. Baadhi ya watu waliounganishiwa maji walilazimika kuchanga mpaka milioni 10 ili Dawasco iweze kuwapelekea maji kwenye maeneo yao.

Eneo hili lina kaya za kutosha kwa Dawasco kuwekeza fedha kwa kuunganisha maji bila kuwachangisha wananchi kwani kuna uhakika wa wateja. Ni aibu kwa shirika ambalo linatakiwa kujiendesha kibiashara kuwachangisha watu ili kuwapatia huduma ya msingi kama maji.

Wengi wetu tuna matumaini makubwa na uongozi mpya wa mkoa wa Dar es Salaam na kasi ya Mheshimiwa Makonda lakini wasiwasi wetu ni kwamba kama alishindwa kutatua matatizo haya akiwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, ataweza kufanya nini kipya kwenye nafasi yake ya sasa?
 
Mkuu fishseller,

Tuache kulalamika na kulaumu. Wewe umechukua hatua gani baada ya kuona magendo, uliwahi kunakili japo namba za gari za hao polisi na TRA?

Masuala ya serikali za mitaa ni manispaa,je uliwahi kumuona diwani wako au meya
Maelezo yako yamelenga tu kumchafua makonda
 
Mkuu fishseller,tuache kulalamika na kulaumu,wewe umechukua hatua gani baada ya kuona magendo,uliwahi kunakili japo namba za gari za hao polisi na tra?
Masuala ya serikali za mitaa ni manispaa,je uliwahi kumuona diwani wako au meya
Maelezo yako yamelenga tu kumchafua makonda
wewe kweli ni mlungo.kaishakuwambia kuwa hicho ni kilio cha muda mlefu.

swissme
 
Ni aibu kwa serikali hii baadhi ya maeneo ya Dar kutokuwa na maji ya uhakika kutoka DAWASCO. Huwa najiuliza shida ni nini?

Yaani vyanzo vya maji tunavyo vingi sana, huwezi kulinganisha na km kule arabuni au hata china ambao wana recycle hata maji ya chooni( yanayotumika kusafishia barabara)
 
Kuna bwege anapigwa na majogoo yake ya kuchi, eti kayatoa Mwanza..... kila kitu cha kisukuma ni kitendea kazi shambani, hayo majogoo ayape majembe yakalime
hahahaha bujibuji wape vidonge vyake.

swissme
 
Sasa kama ni kilio cha mda mrefu kwa nini anamlaumu makonda wakati makonda kapewa mkoa juzi tu,lakini pia inaweza kuwa kilio cha mda mrefu lakini ukawa unalia nyumbani kwako bila kufikisha tarifa mahala popote.
makonda anatakiwa kusikiliza mambo kama hayo sio mambo ya kitoto.wewe na jamaa zako majanga tu.

swissme
 
Yuko wap matonya original ombaomba no.1 tanzania
Huyo ni marehemu kwa sasa, ni mtu aliyefanikiwa kuandaa warithi wake makundi kwa makundi. Inawezekana tabia hiyo inatokana na dhiki ambayo jamii imeikumba kutokana na umasikini.

Kwa taarifa iliyotolewa wiki hii inayoishia leo, watu hao hawatakiwi kuwepo katika maeneo yao ya kuombea kuanzia kesho.

Hayo ni maagizo kutoka kwa Kiranja wa Mkoa.
 
Bandari bubu zipo kibao ....serikali za mitaa wanajua vyema ....polisi na TRA wanajua vyema ....ni wakati JWTZ wawe wakali na mipaka yetu ....hizi njia za panya zinaweza kupitisha hata silaha haramu kama wanaweza kupitisha bidhaa za kawaida kwa kificho.....Makonda kama mdau wa JF naamini ataifanyia kazi taarifa ya mdau huyu ....
 
Sasa kama ni kilio cha mda mrefu kwa nini anamlaumu makonda wakati makonda kapewa mkoa juzi tu,lakini pia inaweza kuwa kilio cha mda mrefu lakini ukawa unalia nyumbani kwako bila kufikisha tarifa mahala popote.
chai tayari lumumba nini?
 
Ina summary jamaa mdau ameandika nini maana ni ndefu hatare halafu wengine hatujanywa chai.
 
Hongera sana mtoa hoja, ila kunavichefuchefu humu bila kusoma maada na kuielewa anachangia kisha anachangia asicho jua. .
Mtu ana pose anaposema kilio cha muda mrefu maana yake, walisha fuatilia na hakuna jibu. .mlitaka aandike mpaka walipokuwa wakienda kwa MAKONDA.
 
Mimi sio mkazi wa Mbweni mpiji ila cha kushangaza ni mji mpya lakini watu wameziba njia halisi za kupitia magari na kujenga ukuta, ,Kaka yetu Makonda ukiwa katika kushughulikia tatizo la maji iende sambamba na waliojenga kuta kwenye mitaa kwenye njia za magari na watembea kwa miguu, nguvu ja pesa. ..
Sio muda mrefu mpiji itakuwa kama Manzese
 
wewe kweli ni mlungo.kaishakuwambia kuwa hicho ni kilio cha muda mlefu.

swissme
Kilio cha muda mrefu nini maana yake kama raia wenyewe hawaisaidii serikali yao kuipatia taarifa sahihi za kihalifu,
Na ukilichunguza hili kwa kina mwisho wa siku utakuta asilimia kubwa ya wa kazi wa eneo husika ndio watendaji kazi wa uharamia huu aidha kwa kuwa vibarua nk.
Tafakari na chukua hatua Acha kulalamika!
 
makonda anatakiwa kusikiliza mambo kama hayo sio mambo ya kitoto.wewe na jamaa zako majanga tu.

swissme
Mleta Mada kaishamhukumu makonda, hakumpa taarifa, ni kama vile ana kamkataba fulani ka uchafuzi Kwa makonda.
Kama sivyo ataje ni lini waliitisha mkutano na watendaji wa serikali na kuwakabidhi taarifa hii anayoitoa humu JF.
Au hata nakala ya barua kutoka kwa serikali ya mtaa au au kitongoji kwenda ofisi ya Ocd wilaya au ngazi yoyote ya juu kiserikali?
 
Back
Top Bottom