change we need
Member
- Aug 10, 2011
- 81
- 9
Nasikitika sana na hali ya mafuriko yanayotokea katika jiji la Dar,hii si mara ya kwanza au ya pili hali hii kutokea lakini baada ya mafuriko wananchi husahau na kuendelea na shughuli zao kama hakuna kitu kilichotokea. Ajabu na la kushangaza zaidi baada ya muda viongozi wa serikali na chama huja na kuongea blabla basi mambo yanaisha. Najiuliza kwanini wakazi wa Dar hawaombi suala la miundombinu ya jiji katika kupeleka maji machafu na maji ya mvua? wameridhika na hali hii? jiji linaendesha miradi mingi tu ya maghorofa makubwa na marefu mbona hakuna hata mwananchi anayelalamika kuhusu miundombinu ya maji? Je Dar wakazi wake wamezoea kuishi na uchafu au harufu mbaya kila kona huku wakiwaangalia watawala wetu na viongozi waliowapa dhamana wakiwa kwenye magari ya viyoyozi raha mstarehe? Dar nani kawaloga?