Wakati wa binadamu si wakati wa Mungu

Wakati wa binadamu si wakati wa Mungu

Joined
May 3, 2019
Posts
53
Reaction score
145
WAKATI WA BINADAMU SI WAKATI WA MUNGU.

Leo 12:15pm,20/10/2019.

Mwaka 2008 aliyekuwa mgombea Urais wa Ghana kupitia chama cha NDC,Prof John Atta Mills alipatwa na upofu ghafla akiwa kwenye kampeni na kuwahishwa kwenye Matibabu nchini Afrika ya Kusini.

Kesho yake Magazeti nchini Ghana yakaandika Mgombea mwenye kupendwa sana na watu kupitia chama cha NDC afariki dunia nchini Afrika ya Kusini ilihali ndio kwanza Mgombea huyo alikuwa katua Afrika ya Kusini na ndio anaingia kwenye chumba maalum kwa ajili ya upasuaji wa jicho moja.

-Unabii wa T.b Joshua kwa Prof John Atta Mills.

Mtumishi wa Mungu,T.b Joshua akiwa ziarani nchini Ghana kwa ajili ya mikutano ya injili miaka ya 1998,alialikwa na Profesa John Atta Mills kwa ajili ya chakula cha jioni nyumbani kwake,wakati huo Profesa John Atta Mills alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ghana.

Mtumishi wa Mungu T.b Joshua alikubali mwaliko wa Profesa John Atta Mills,alifika kwenye chakula cha jioni nyumbani kwa Profesa John Atta Mills na kushiriki chakula cha jioni pamoja na familia ya Profesa John Atta Mills.

Baada ya Chakula T.b Joshua alishukuru na alimwambia Profesa John Atta Mills kwamba atakuwa Rais wa Ghana lakini atagombea mara ya kwanza atashindwa,atagombea mara ya pili atashindwa lakini mara ya tatu atakuwa Rais wa Ghana.

Profesa John Atta Mills alijibu kuwa yeye ni Mhadhiri tu wa Chuo Kikuu cha Ghana hata siasa siijui lakini je watu watakubali kumchagua Mgombea aliyeshindwa mara mbili!? Mtumishi wa Mungu T.b Joshua alimsisitiza atakuwa Rais wa Ghana na baada ya hapo Mtumishi wa Mungu T.b Joshua aliaga na kuondoka,hiyo ilikuwa ni mwaka 1998.

-Hospitalini Afrika ya Kusini.

Madaktari wa Afrika ya Kusini wakamfanyia upasuaji wa jicho moja lakini kesho yake ilisababisha jicho la pili kuleta shida na madaktari wakashauri kufanyiwa operation kwa jicho lake la pili.Profesa na watu wake waliomsindikiza waliingiwa na hofu kuweza kumpoteza Mgombea wao ambaye alikuwa anaelekea kushinda uchaguzi huo wa mwaka 2008.

-Simu yapigwa kwa T.b Joshua.

Profesa John Atta Mills alikumbuka unabii wa T.b Joshua wa mwaka 1998 alipomualika kwa chakula cha jioni nyumbani kwake na kumtabiria kuwa atakuwa Rais wa Ghana.

Hallo Mtumishi wa Mungu,Mimi ni Profesa John Atta Mills tulikutana miaka kumi na mbili iliyopita nilipokualika nyumbani kwangu kwa ajili ya chakula cha jioni na baada ya Chakula uliniambia nitakuwa Rais wa Ghana nitakapogombea mara ya tatu baada kugombea mara mbili na kushindwa,

Hivi sasa ninavyoongea nipo hospitalini Afrika ya Kusini kufanya upasuaji wa macho yangu baada ya kupata itilafu,nimefanya jicho moja na sasa nataka kufanya upasuaji wa jicho la pili.

T.b Joshua alimjibu,Usiku wa kuamkia leo uliota ndoto,je unaikumbuka ndoto uliyoota,Profesa John Atta Mills alifikiria kidogo na kuikumbuka ndoto alioota,na haraka akamjibu T.b Joshua,nimeikumbuka ndoto hiyo,nilikuwa natembea pembeni ya barabara nimeshika mkongojo na mtu akiniongoza,T.b Joshua akamjibu ndivyo utakavyokuwa kama utafanya upasuaji wa jicho la pili,tuombe pamoja na baada ya maombi njoo moja kwa moja Lagos,Nigeria kwa ajili ya maombi.

Wazo la kutoka hospitali likaleta mtafaruku baina ya watu alioongozana nao kuelekea hospitalini hapo Afrika ya kusini,lakini hatimaye walifanikiwa kutoka hospitalini Afrika ya kusini na kupanda ndege kuelekea Synagogue Church of All Nations linaloongozwa na Mtumishi wa Mungu T.b Joshua pale Lagos,Nigeria.

-Profesa John Atta Mills na watu wake watua Lagos,Nigeria.

Uwanja wa ndege wa Lagos alikuwepo T.b Joshua mwenyewe kumpokea mgeni,baada ya kumpokea,Prof John Atta Mills alimwambia T.b Joshua,Je nitakuwa Rais kipofu wa Ghana,kama ni hivyo mi basi urais siutani na sina haja nao! T.b Joshua alimwambia si ahadi yangu wewe kuwa Rais bali ni ahadi ya Mungu wewe kuwa Rais nami niliisema tu,twende kwenye maombi kwani hakuna gumu lolote lisilowezaka kwake yeye Bwana wetu Yesu Kristu.

Maombi yalichukua siku nzima jicho la pili lililoshauriwa kufanyika upasuaji likaona kabisa na hatimaye jicho lililofanyika upasuaji likapona kabisa,na akachagua kupumzika kanisani hapo kwa wiki nzima.

-Wiki ya mwisho ya Uchaguzi nchini Ghana 2008.

Profesa John Atta Mills anarudi akiwa mzima wa afya,akiwa anaona vyema na habari hiyo ilijaza watu katika mkutano wake wa kwanza baada ya kurudi kutoka kwenye matibabu ya Macho,Kampeni zake katika wiki hiyo moja ya mwisho zilivuta umati mkubwa wa Watu na hatimaye siku ya Uchaguzi Wananchi wa Ghana wakamchagua Profesa John Atta Mills kuwa Rais wa Ghana na unabii wa T.b Joshua ukatimia.

Ndugu zangu wakati wa Mwanadamu si wakati wa Mungu na awazayo Mwanadamu siyo awazayo Mungu,Kusudi la Mungu kwa mtu mwenye haki halitakatizwa na binadamu yeyote .Ahsante Mwenyezi Mungu kwa ajili ya neno lako ambalo ni kweli,Ahsante kwa Watumishi wako wakiwa kama nuru na mwanga hapa duniani,Ahsante kwa kuibariki Afrika,Ahsante kwa kuibariki Tanzania,Ahsante kwa kumlinda na kumbariki Rais wetu John Pombe Magufuli.

Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755078854.
 
Chakubanga Kwa sasa ungeacha kwanza haya ya Ghana, kwa sasa hebu tutoeni wasiwasi sisi tusio na connection! Ni nini kinaendelea mkuu? Achana na mambo ya 1998, hebu tusaidieni jamani na sisi
 
Back
Top Bottom