Wakati tunafurahia usomaji wa namba na Majipu, nchi inakwenda huku...

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,997
20,329
Wakati tunafurahia usomaji wa namba kile kiitwacho utumbuaji wa "Majipu", plate number ninayoisoma mimi inasomeka hivi;
Yield ya bonds za serikali ambayo ni risk free investment kwa mujibu wa BOT imefikia 19.7586% leo.

Access Bank wamepandisha interest rates kwenye fixed deposit accounts hadi 17% (yaani ukiweka fedha wanakupa riba ya hadi asilimia 17 kwa mwaka).

Namaanisha ukiwa na fixed akaunt wanakupa riba ya 17% ya pesa uliyoweka.
Kwahiyo mabilionea wetu kati yao mmoja akienda bank kutoa mil 500 tu ai fix bank halafu kwa mwaka wanampa riba ya 17%. Bilionea huyu anaweza kuishi mwaka mzima kwa kula riba ya bank tuuuu asifanye kazi yoyote.

Hii inamaana gani katika uchumi usiodhibitiwa kijasusi? Inamaanisha tutarajie benki kutoza riba kubwa katika mikopo na hivyo kuathiri hasa wananchi wa kipato cha chini wanaokenua meno mpaka geno la 32 badala yake itawanufaisha wenye nazo wanaowaimbisha nyimbo za majipu maana watapata faida kubwa kwa kuweka fedha benki.

Bank inajiuliza kama nikikoposha serikali inanilipa 20% riba je Yericko nimkopeshe kwa riba ya %? kwasababu Yericko ni mtu na ni subject to risks tofauti na govt ndio mana wanatoza 24% sasa nani atafanya biashara kwa riba juu kiasi hicho.

Pengo la wasionacho ambao ni 86% ya watanzania wote, Wataendelea kudhibitiwa na Kundi dogo la 14% ya Watanzania wote, hawa ndio ambao wanadhibiti Uchumi na siasa ya nchi kwa gharama ya Watanzania 86% wanaoishi kwenye mstari wa umasikini.
Tuendelee kuisoma namba, bahati nzuri ukienda benki haupeleki kadi ya chama!

Nini kifanyike ni kujiuliza kwanini serikali inapandisha TBs rates kiasi hicho? jibu nikwamba haina hela na inafanya hivyo ili kupata pesa kuendesha majukumu yake. hivyo cha kufanya ni serikali ipunguze kukopa ndani kwa mfano kama serikali ikikopa kwa kuuza TBs at rate ya less than 5% bank zitakopesha private sector kwa less than 10%. hivyo private sector itakua kwa kasi kwani mikopo inalipika
 
Yericko uzuri wako watu wengi wanajua huwa unatabia ya kuzungumza Mambo usio na weledi nayo na ndio Mbinu uliyoamua kutumia kujifunza nasi bila ya hiyana tutakufunza.

Kwny nchi yoyote ambayo Inflation rate ipo juu njia ya kudhibiti mfumuko huo
1) Kupunguza Goverment Expenditure (na hilo linafanyika)
2) Kuongeza Riba kwny Bank ili ku discourage Drawing na ku incourage savings ili kupunguza mzunguko wa Fedha kwa muda.
 
Wakati tunafurahia usomaji wa namba kile kiitwacho utumbuaji wa "Majipu", plate number ninayoisoma mimi inasomeka hivi;

Yield ya bonds za serikali ambayo ni risk free investment kwa mujibu wa BOT imefikia 19.7586% leo.

Access Bank wamepandisha interest rates kwenye fixed deposit accounts hadi 17% (yaani ukiweka fedha wanakupa riba ya hadi asilimia 17 kwa mwaka)

amemaanisha ukiwa na fixed akaunt wanakupa riba ya 17% ya pesa uliyoweka.

Kwahiyo mabilionea wetu kati yao mmoja akienda bank kutoa mil 500 tu ai fix bank halafu kwa mwaka wanampa riba ya 17%. Bilionea huyu anaweza kuishi mwaka mzima kwa kula riba ya bank tuuuu asifanye kazi yoyote.

Hii inamaana gani katika uchumi usiodhibitiwa kijasusi? Inamaanisha tutarajie benki kutoza riba kubwa katika mikopo na hivyo kuathiri hasa wananchi wa kipato cha chini wanaokenua meno mpaka geno la 32 badala yake itawanufaisha wenye nazo waowaimbisha nyimbo za majipu maana watapata faida kubwa kwa kuweka fedha benki.

Pengo la wasionacho ambao ni 86% ya watanzania wote, Wataendelea kudhibitiwa na Kundi dogo la 14% ya Watanzania wote, hawa ndilo ambao ndio wanadhibiti Uchumi na siasa ya nchi kwa gharama ya Watanzania 86 wanaoishi kwenye mstari wa umasikini.

Tuendelee kuisoma namba, bahati nzuri ukienda benki haupeleki kadi ya chama!
Mkuu awali ya yote nimefurahi kukuona jukwaani
 
Yericko uzuri wako watu wengi wanajua huwa unatabia ya kuzungumza Mambo usio na weledi nayo na ndio Mbinu uliyoamua kutumia kujifunza nasi bila ya hiyana tutakufunza.

Kwny nchi yoyote ambayo Inflation rate ipo juu njia ya kudhibiti mfumuko huo
1) Kupunguza Goverment Expenditure (na hilo linafanyika)
2) Kuongeza Riba kwny Bank ili ku discourage Drawing na ku incourage savings ili kupunguza mzunguko wa Fedha kwa muda.

Mkuu labda hujui mada hii, hapo faida anapata yule anayeweka pesa, laki mtu anayekopa (masikini wa tz) ni majanga, maana mkopo inaweza kuwa rejesho lake 18-20%......matajiri walio 14% ya Watz wanaodhibiti siasa ya nchi hii ndio wanaonufaika
 
Toa ushauri wa kitaalamu nini serikali ifanye kuepukana na hilo.
Kazi ya upinzani ni kutoa mawazo mbadala pale serikali inapokwama.!
Huyu ni fundi ujenzi, unapoanza kumwambia atoe ushauri kuhusu masuala ya kiuchumi utakuwa unamuonea kama yule Mtangazaji wa BBC, Zuhura Yunus alivyomuonea Lowassa kuhusu dhana ya Mabadiliko!

Usishangae ukifahamu hata mada ameokota tu mitaani na kuileta hapa!

Hizo rates niza kuokota mitaani kama ilivyo mada!

Kama unataka jibu sahihi muulize, atatumia mbinu gani kupaka rangi nyumba ya ghorofa!
 
Asante Yerico Nyerere,kumbe riba ya mkopo itaongezeka sasa kama nitaenda kukopa benki yangu pendwa ya n.m.b!basi nimestisha kwenda!
 
Mkuu labda hujui mada hii, hapo faida anapata yule anayeweka pesa, laki mtu anayekopa (masikini wa tz) ni majanga, maana mkopo inaweza kuwa rejesho lake 18-20%......matajiri 14% wanaokula na kusaza ccm ndio wanaonufaika

Yericko kilichofanyika hapo ni muongozo wa kanuni za Uchumi usilete blabla za Siasa hufanyika Dunia nzima.
Halafu acha kukariri kuwa anaekopa ni Maskini tu na anae weka pesa ni tajiri. Hivi karibuni NBC ilifanya tafrija fupi ya kumkopesha Mohamed Enteprise jumla ya Bill 100 huyo nae ni maskini?
Maskini anaumizwa zaid na Inflation rate kubwa kuliko riba. Ndio sababu serikal imechukua hatua hizo! au ulitaka bei za bidhaa ziendelee kupaa Ili upate hoja ya kuanzishia thread?
Masuala ya kiuchumi hujibiwa kiuchumi wewe leta mbadala wa kufanyika kukabiliana na Inflation mbali ya kubana matumizi ya serikal na kupandisha interest rate hatua ambazo ndio zinachukuliwa na serikali kwa sasa
 
Majipu unaweza kutumbua ya mwenzio lakini kujitumbua ni ngumu hasa likiwa limeota pabaya, mpaka limekua kansa
 
Yote haya ni kwasabu nchi hii wajinga wengi!

Mijitu imekuwa ni mijinga ikisikia neno CCM haitumii hata akili kuangali hali ya nchi ikojee inashabikia tu CCM utadhani inashabikia soka.
Mijinga Nadhani ni ile inayosoma andiko la yeriko kwa dakika mbili, inaanza kutukana bila kwanza kujiridhisha kama andiko hilo lina UKWELI?
 
Badala ya kuvizia wapi serikali itakosea ni vyema wapinzani kutoa solutions kwenye issues za msingi ili waaminike ....nchi ilipofikia maamuzi magumu yoyote lazima yawe na negative impact kwa walalahoi hata kama ingekuwa ni chadema wamechukua nchi .....huwezi kurudisha nchi iliyooza kwenye mstari alafu mambo yakawa sawa tu ghafla ....
 
Back
Top Bottom