SONGOKA
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 1,836
- 1,846
Ni wakati muafaka sasa, mwenye nia nzuri na hii nchi, mwenye kutaka kufichua udhalimu, mwenye malalamiko, mwenye kuchukia ufisadi, Mungu atupe nini?? Iambie dunia ijue, waeleze bila uoga, ukikosa kuitumia nafasi hii basi tutaendelea kuwa waathirika wa "nani amfunge paka kengere". CNN wapo, SKY news wapo, ABC wapo, CCTV wapo, Frach24 wapo, SABC wapo, hata Aljazeera pia watakuepo. Na mgeni lazima aje...WAPI wana harakati, wapi wana haki za binadamu, wapi kituo cha sharia (human legal rights center) wapi wana JF mnaochukia Ufisadi? wapi mama ananilea nkya, wapi mama kidjo bi simba,wapi deus kibamba, wapi jukwaa la katiba...tuwaeleze kuhusu radar, kuhusu Richmond, kuhusu meremeta, kuhusu kiwila, kuhusu mabwepande, kuhusu mwangosi, kuhusu ulimboka, kuhusu arusha, kuhusu fr evalist, kuhusu north mara, na kuhusu matokeo ya kidato cha nne, kuhusu wanachi tulivyokata tamaa....Wazungu kwa taarifa yenu ni "wambea sana" na hawa ignore any signal, ....Je TUTAITUMIA NAFASI HII HADIMU.