Wakati nasubiria uber, nawapatia huduma ya kutengeneza QR Code

Yaani mi nakupa hela unitengenezee tudoti doti.!!! Dunia imefika mbali naomba isimame nishuke.
Nadhani ungekuwa na uhitaji nayo ungelipa tu utengenezewe.. Jiulize kwanini hao kina mengi wanatoa hiyo pesa ya kutengenezewa vidotidoti kwaajili ya kuweka kwenye maji yake ya kilimanjaro na bakhresa nae analipa kwaajii ya kuweka kwenye bidhaa zake... Usishobokee usichokijua, samahan kwa kauli mbaya nakurekebisha tu
 
Hapana.. Sio lazima uende brella, hii utaipata hata ukiwa nyumbani kwako muhimu ututumie details zako unazotaka zionekane hapo kwenye QR Code. Barcode ndio inamlolongo mrefu hadi uende GSM
Ushanichanganya sasa, kwa nini sasa watu wahangaike na bar code na kwa gharama kubwa ilihali kuna hii yako kwa bei ya kutupa??
 
Nafurahi kwa swali zuri.. Wengi hutumia barcode baada ya kusajili biashara au bidhaa zao kwasababu huwezi kupata barcode bila kuwa na leseni ya biashara na tin number! Bidhaa nyingi huwekwa barcode kwaajili ya kuonyesha bei, eneo la kiwanda au tovuti ya kampuni inayomiliki bidhaa husika. Qr code huwekwa kwenye bidhaa kwaajili ya kuonyesha bei, location, details za mtengenezaji, tovuti ila pia unaweza kuweka vyote hivyo kwenye qr code moja ila kwenye barcode huwezi. Sababu kubwa ya kutumia barcode zaidi ni kwasababu huwezi kuitumia barcode kwenye bidhaa ambayo haijasajiliwa ndio maana wafanyabiashara wengi wanaitumia ili bidhaa zao ziwe na thamani zaidi na kuoneka halali zaidi. ila Qr code unaweza kuitumia bila hata kusajili bidhaa yako na huifadhi details nyingi zaidi ya barcode muhimu umpate mtaalamu wa mtandao akutengenezee.
 
Sasa umeeleweka mkuu. QR kwa sisi tunaoendesha mambo kinyemela.
 
Uzi wako umekaa kichoyo mkuu unahisi kila mtu ni msoni na muelewa wa mambo kwa haraka..

Hebu niambie mimi mfanya biashara nauza nguo za dukani nazinunua kutoka china,thailand sasa hiyo qr code inahudikaje dukani kwangu/kwenye biashara yangu na faida yake ni ipi??

Hebu niambie mimi mfanyabishara nina duka la kuuza simu na vifaa vya simu kama ,usb cable,adapter,flash memory card na charger hiyo qr code inafanyaje kazi kwenye duka langu namimi nitanufaika vipi na hiyo qr code.
 
Kama huitak acha kupost wivu wako hapa the poor have nothing but the chain of their poverty
Ushanichanganya sasa, kwa nini sasa watu wahangaike na bar code na kwa gharama kubwa ilihali kuna hii yako kwa bei ya kutupa??
 
Uzi wako umekaa kichoyo mkuu unahisi kila mtu ni msoni na muelewa wa mambo kwa haraka..

Hebu niambie mimi mfanya biashara nauza nguo za dukani nazinunua kutoka china,thailand sasa hiyo qr code inahudikaje dukani kwangu/kwenye biashara yangu na faida yake ni ipi??

Hebu niambie mimi mfanyabishara nina duka la kuuza simu na vifaa vya simu kama ,usb cable,adapter,flash memory card na charger hiyo qr code inafanyaje kazi kwenye duka langu namimi nitanufaika vipi na hiyo qr code.
Asante sana mkuu kwa swali zuri.. Jibu lako: Ukitaka kuwa na biashara iliyo hai kuna mambo kadhaa unapaswa kuzingatia ambayo ni kuwa na bidhaa bora, huduma nzuri lakini pia kuitangaza biashara yako.

Kwa mtu kama wewe mwenye duka la nguo au la simu tutakutengenezea business card yenye maelezo mafupi ya biashara yako na hapohapo kwenye card tutakuwekea qr code yako, faida yake ni kwamba hiyo qr code itabeba details halali za mmiliki wa biashara/ bidhaa ama duka lako.

Faida yake: Qr code italinda bidhaa zako, mfano una-heat transfer yakuprint macover ya simu au tshirt zako tutakutengenezea qr code ndogo tu ambayo utaiprint kwenye bidhaa zako kwahiyo yeyote atakaenunua tshirt zako ataweza kuprint majina yake anayotaka ila ukiscan hako ka-code kadogo kwenye hiyo tshirt itakuletea details zako wewe unaeziuza zikiwa plain! Kwahiyo mteja atakutafuta wewe kwa kupitia hiyo qr code na yeye anunue tshirt zake plain.

Qr code unaweza kuiscan kwa app za simu nyingi sana zinazopatikana playstore, kwahiyo ni rahisi sana kusoma details zake.
Karibu sana mkuu.
 
Nimekuelewa vizuri sana kiongozi swali dogo la nyongesa

Je ikitokea nimepunguza kitu au nmeongeza kitu kwenye bidhaa zangu hiyo qr code ntatakiwa kutengeneza nyingine?

Swali jingine la nyongesa
Ukienda super market ukinunua kitu yule muuzaji anapitisha ile bidhaa kwenye mashine fulani kisha inasoma ile mashine inasoma bei ya ile bidhaa je ile mashine inaitwaje?utofauti wake na qr code upoje na faida zakw ikiwezekana..
 
Hapana, hautotengeneza nyingine ila utarudi kwetu na tutabadilisha maelezo ya code yako.
Ile mashine inayosoma bei inaitwa barcode scanner, na code inayosomwa hapo ndio inaitwa BARCODE.

Tofauti ya BARCODE na QR CODE ni hii;

BARCODE
Ili kupata Barcode unatakiwa uwe umesajili biashara yako, uwe na leseni ya biashara na uwe na TIN namba. Lakini pia Barcode inabeba bei ya bidhaa pekeyake haibebi kitu kingine na pia unailipia kila mwaka (renew).

QR CODE
Code hii hutumika kuweka bei ya bidhaa, tovuti ya kampuni/duka la wanaozalisha au kuuza biadhaa, kuweka namba ya simu ya mmiliki wa bidhaa, kuwe jina la bidhaa au la mmiliki, kuweka maelezo ya bidhaa au kuweka eneo ipopatikana bidhaa. Utofauti wa code hii ni kwmba unaweza kuweka maelezo yoote haya kwenye hii code moja sio kama barcode unaweka bei tu, lakini pia code hii hailipiwi kila mwaka hulipiwa maramoja tu. Kupata code hii ni rahisi, uwe tu na bidhaa yako na kumtafuta mtaalamu wa kuitengeneza (wapo wachache sana labda uende kwenye kampuni ya GS1 ila ni gharama sana).

Code zote hizi ni halali kisheria ila wengi wanaitumia QR CODE bila kusajili biashara zao ili kuipa thamani bidhaa ama biashara yake kwasababu unaweza kuipata bila hata kusajili bishara yako. Lakini ni kinyume cha sheria maana bidhaa ikiwa haijapitia TBS kukaguliwa halafu mmiliki wa bidhaa ile akaja kwetu ili kupata code hiyo, kisha ile bidhaa ikaenda kuuzwa kwenye supermarket na kumletea mteja madhara basi tutakamatwa sisi tuliokutengenezea code ya kuipa thamani bidhaa yak wakati haikusajiliwa... code zote ni muhimu sababu huipa thamani biashara yako ila ni vyema ukaisajili kwanza ndio ukatafuta code hizi.

Karibu tena.
 
Shukurani kiongozi nimejifunza mambo mengi kwa niaba ya watanzania wenzangu wasio na uelewa wa mambo haya.
Naamini watapita hapa na watakua wateja wako wa moja kwa moja ama wateja kwa maana ya kuwatoa tongotongo
 
QR code kwenye business card ina faida gani?
Unapotengeneza business card ni unaitangaza na kuipa thamani biashara yako, lakini ukiongeza QR CODE kwenye card yako utaipa thamani zaidi biashara yako. Kwasababu asilimia kubwa ya wanaotumia code hizi ni wale waliosajili biashara zao na wengi wao wanamasoko makubwa, kwahiyo uatakapoitumia code hii utamvutia mteja zaidi na kumpa uhakika mkubwa wa uhalali wa biashara au bidhaa yako.

Karibu.
 
Shukurani kiongozi nimejifunza mambo mengi kwa niaba ya watanzania wenzangu wasio na uelewa wa mambo haya.
Naamini watapita hapa na watakua wateja wako wa moja kwa moja ama wateja kwa maana ya kuwatoa tongotongo
Shukrani pia.
 
Nipe elimu kwanza qr code ni kitu gani manake naonagaaa onaga
Natengeneza QR Code kwaajili ya kuitumia kwenye biashara yako au business card yako kwa bei nafuu kabisa ya offer sawa na bure! Faida ya QR Code kwa mfanyabiashara au mjasiriamali ni kwamba hufanya bidhaa yako au biashara yako kuwa ya thamani na yenye kupokelewa vizuri zaidi, pia QR Code huifadhi mawasiliano yako pamoja na maelezo ya bidhaa au biashara yako kwa kaalama kadogo tu ambacho hakitachukua nafasi kubwa mahali hapo utakapoiweka.

QR Code hutumika dunia nzima kwa wafanyabiashara wakubwa sana na wadogo pia, mfano.. Waangalie akina Deskjet kwenye packing za printer zao kuna QR Code, tecno, samsung, nokia na nyingine nyingi. Tanzania angalia bidhaa za kina Mh.Mengi (Kilimanjaro water), Mh.Bakhresa (Uhai) na Mh.Mo (Masafi) kwote huko utaona hii QR Code ikiweka ubora zaidi na thamani kubwa kwenye bidhaa zao zinazosambaa sehemu kubwa ya dunia.

Unasubiri nini?! Pata leo QR CODE yako uitumie milele hadi Mungu atakapokunyamazisha mwenyewe, ipate kwa bei nafuu kabisa ya Tzsh.30,000/= tu, karibu.. Asante.

Affiliate:
Niletee mteja mmoja wa QR CODE nikulipe Tsh.5000/= Hakuna kikomo cha kuleta wateja.
5000*10=50,000.. changamkia hii fursa, usione ndogo! Wengi walianza hivi ila sasa ni ma-agent wa makampuni makubwa na maisha yao ni safi.

Phone: +255 688 072 587

Hii ndio QR Code View attachment 766567
 
Nipe elimu kwanza qr code ni kitu gani manake naonagaaa onaga
Ni alama ndogo ya kielektroniki inayobeba bei ya bidhaa, huduma fulani, maelezo ya bidhaa yako au biashara yako. Code hii huilinda bidhaa yako kwenye suala zima la umiliki lakini pia huipa thamani biashara yako.

Mfano: Wewe unatengeneza fresh juice na kuzipaki kwenye chupa, juice zako zikawa nzuri wafanyabiashara wengine wakaanza kukuibia bidhaa yako kwa kununua kwa jumla kisha wanatoa lebo yako kwenye hizo juice wanabandika lebo zao ili nao wapate wateja... ili kusuluhisha hilo tutakutengenezea QR CODE ya bidhaa zako na tutaiprint kwenye chupa zinazobeba juice yako kwahiyo huyo anayeiba ataweza kubandua lebo yako tu lakini hatawaeza kutoa ile QR CODE kwasababu imeprintiwa kwenye chupa moja kwa moja na bidhaa ile ikipelekwa kwenye masoko makubwa lazima wascan zile code kwahiyo wataona details za mmiliki halali wa bidhaa ile na kumkata aliyebadili jina...

Ndiomaana code hizi hutumiwa sana na watu wenye biashara kubwa na masoko makubwa kuanzia supermarkets.. nk.

Vp nikitengeneza coupon za kiingilio kila mmoja kwa namba yake....akifika mlangoni anaskan anaingia. Itanicost ngapi
 
Back
Top Bottom