Wakati jamii inapotuangamiza undani wetu

Nov 2, 2023
60
50
Jamii imekuwa ni mwongozo wetu kwenye kuishi, hisia zetu mawazo na kufikiria mara zote yanatokana na jinsi jamii ilivyotutafsiria maisha. Kinachotokea ni tunakuwa zao la jamii inavyotaka na kukosa uhuru wetu binafsi kwa hofu unaweza kuwa na changamoto kutokana na mifumo yetu tulivyojiwekea.

Tunaongelea kuhusu tunavyo aminishwa fedha na kufikiri kuwa kipaombele kwetu na ni vitu vinavyoenda njia moja kutuathiri. Tujiulize kwanini tumeishia kuipa fedha umuhimu wa kwanza na kufikiri kwetu tunakoshairiwa na kunakoleta fedha na si kitu kingine.

Kwaufupi inaonekana tunahofu sana na wakati, hatutaki kukutana na changamoto yoyote wala tatizo tunaikimbilia fedha kwakuwa yunajua inaweza kutufanya tutulize tamaa zetu na tusahau mafunzo ya muhimu yatayotufanya kukua kwa kuelewa uhalisia wa maisha kwa changamoto zake kwa jinsi kila mtu alivyo.

Iwapo tutakuwa na jamii inayoamini fedha zaidi ya kwanza kuweza kupata uelewa wa kujitambua binafsi kwa kujionyesha kwa uwezo wa ulichonacho kinachoelezea maana kubwa ya ukweli wa kufurahia matendo ya kuishi kwako ni lazima utakuwa nnje ya ubora wako na utakuwa mtumwa wa kufikiri sana kuhusu fedha kuliko thamani yako binafsi.

Wazo la kuishi kwa kushauriana kufikiri sana kila kona ni tumegeuza maisha ni tatizo kubwa la kutatua wakati si kweli. Tunahisi tunatatizo kubwa tunalotakiwa tufikiri sana kuliepuka na kukosa muda wa akili yetu kupumua na kuweza kufanya kazi yake kwa ufasaha. Muda wote tunahofu na maisha kwakuwa tunahisi hatuto endana na jamii yetu inavyotaka, tunaonekana tumepotea na kujisahau kabisa thamani yako binafsi bila kuweka ushindani ndani yako.

Haya yote ni msukumo wa jamii kutufanya tushindwe kupata muda wa kujitambua undani wetu na kutuweka bize kwenye mchezo wake. Simanishi fedha si muhimu hapana bali matendo yako yalete fedha na si fedha ndio ikupangie matendo. Na hili hutokea pale tu utapotambua mwenyewe thamani ya matendo yako yanayoleta uhai kwenye mwili na akili yako nakuona mwanga wa maisha.

Na kufikiri sana hakutoenda kutufanya tujitambue zaidi ya kuchanganyikiwa zaidi. Na tunafikiri sana kwakuwa tunataka tuenee sehemu ambazo si saizi yetu kwa msukumo tu wa kuonekana kwenye jamii wakati tungeweka nguvu na ujuzi wetu kwenye vitu vyenye kutoa thamani zetu za ndani kimatendo tungekuwa na wakati mzuri sana wakuishi bila mkazo.

Nb: Hatuwezi kuepuka matatizo na kuteseka kwa kufikiri sana na kuwa na fedha ya kutosha. Kila mtu unahitajika kujielewa wewe kwanza kabla ya kukimbilia chochote kukutafsiri. Kuanzia hapo itakuwa nirahisi kujionyesha wewe halisi uliyejitambua na kuepuka mitego ya jamii inavyotaka kukutengeneza inavyotaka.
 
Dunia kila kona watu wanafuata mfumo wa jamii fulani haswa ambao wameleta fedha...Hata maendeleo nayo wanaona ni kama kufikia jamii fulani..
 
Dunia kila kona watu wanafuata mfumo wa jamii fulani haswa ambao wameleta fedha...Hata maendeleo nayo wanaona ni kama kufikia jamii fulani..
Haimanishi kila mtu akiwa anaumwa na wewe umwe makusudi hata kama umeshajua ugonjwa. Maisha ni yako peke yako unajukumu nayo mwenyewe kuyaishi kama ulimwengu ulivyokupendelea sio kama watu wengine walivyokuwekea kuzuizi. Maisha ni mara moja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom