Wakatae marafiki wenye Shobo ( Mamluki )

Wakatae marafiki wenye Shobo ( Mamluki )

Ubinadamu ni kazi sana kuna wengine utawasaidia wakiwa na shida wakipata kidogo tu wanaanza dharau.
 
Urafiki wa kutafutana kwa matukio ukatae , wakati wote chimbuko la urafiki wako na mtu litokane na utu na sio mtu akushobokee mambo yako yakiwa Super, Yesu mwenyewe aliwakemea wanafunzi wake waliokuwa wanamtafuta ili wapate mikate.

Wapo aina ya watu kwenye maisha watatakakuwa na ukaribu na wewe ukiwa na nafasi fulani au uwezo fulani watu wa aina hii tambua utawapoteza usipokuwa na hiyo nafasi au huo uwezo they are not loyal to you.
UHALISIA WA MAISHA UKO HIVI.
Mnajua sasa iv watu wako busy sana na kutafuta maisha (maokoto) sio rahisi mtu akupigie pigie simu kila muda bila sababu ya msingi et akusalimie tu.
Lazima kuwe na jambo la msingi la kukutafuta moja wapo kama ivyo mtu amekwama anahitaji msaada kutoka kwako. Mimi kwa upande wangu naona sio mbaya labda kama hupendi kumsaidia hio ndio utaona kero. Mimi binafsi mtu akinitafuta anahitaji msaada kwanza naona amekumbuka uwepo wangu na umuhimu wangu kwake.
 
Marafiki status viewers.
Au wale waku add friend facebook
😆😆😆
 
Back
Top Bottom