mtafuta-maisha
JF-Expert Member
- Nov 5, 2016
- 1,982
- 2,934
Hii story inaanzia hapa Wakala wa kifo alivyowatesa polisi katika kesi ya aina yake
Siku iliyofuata ripoti ya daktari ya kiuchunguzi kuhusu ule mwili wa kijana uliokutwa hotelini inaletwa kwa Lawson, na yule kijana kupitia alama za vidole vyake na kumbukumbu za mpangilio wa meno yake kinywani anagundulika kuwa jina lake ni Carlos Perez aliyekuwa na umri wa miaka 19 aliyekuwa akiishi na baba yake nje kidogo ya mji wa Florida.
Baada ya hiyo taarifa Kachero Lawson na Borne wanaamua kuendesha gari mwendo wa masaa matatu mpaka nyumbani kwa Perez kumtaarifu baba yake Bwana William Perez juu ya kifo chake. Wanapofika wanagonga mlango na baba yake ndiye anafungua mlango ambapo wanampa taarifa juu ya kifo cha mwanaye.
Carlos Perez alikuwa akiishi na baba yake William Perez aliyekuwa na umri wa miaka 56. Baba na mwana walikuwa na ukaribu sana na walipendana sana, Perez alipenda sana masuala ya kazi za mikono hivyo alikuwa anapenda sana kuunda na kubuni vitu mbalimbali. Tarehe 26 mwezi wa 8 mwaka 2003, Perez hakurudi nyumbani kutoka kwenye mamlaka ya ajira ambako alikuwa amepata kazi ya kibarua cha muda. Baba yake anapata wasiwasi kwakuwa Perez hakuwa na tabia ya kutorudi ama kuchelewa nyumbani. Baba yake anaamua kutoa taarifa polisi juu ya kupotea kwa kijana wake. Aliwataarifu polisi kwamba Perez uwa anawahi nyumbani na siku zote uwa wanakula chakula cha usiku pamoja lakini siku hiyo hakutokea, watu wote pale kituoni walimwambia kwamba ni kijana wa miaka 19, na haya anayofanya ya kuondoka kutorudi nyumbani hufanywa na vijana wengi wakiwa kwenye umri huo ila baba yake Perez aliwajibu hapana Perez hayuko hivyo na hawezi kufanya hivyo.
Hakumuona mwanae tena mpaka baada ya siku tatu ndipo analetewa taarifa juu ya mwili wa mwanae kukutwa hotelini akiwa kauawa. Lakini makachero hao walikuwa na maswali ambayo walitaka kuona kama yanaweza kujibiwa na baba yake Perez. Perez alikuwa akiishi Fortl Lauderdale nje ya Florida mbali kabisa na Melbourne, sasa swali imekuaje amekutwa hotelini Melbourne.
Borne alimuuliza William kama mwanaye alikuwa akifahamiana na mtu yoyote Melbourne ambaye huenda alikuwa na uhasama naye na angependa kumdhuru. William alijibu kuwa anashangaa imekuaje mwanaye amekutwa Melbourne wakati anafanya kazi eneo hilo hilo na wala hana gari.
Makachero waliamua kuondoka na kuelekea kwenye makao ya polisi ya Fort Lauderdale ili kuzungumza na kachero mpelelezi wa kesi za mauaji wa eneo hilo ajulikanaye kama Mike Shorkwel. Wakiwa katika mazungumzo wakamwambia kuwa wanachunguza kesi inayohusisha mauaji ya kijana mmoja na hapo ndipo Mike alipowaonyesha picha za mwili wa marehemu ambao anahisi aliyemuua Perez ndiye aliyemuua huyo pia. Mike aliwaeleza kwamba kuna kesi ambayo anaifanyia upelelezi juu ya mauaji ya kijana mmoja katika namna inayofanana na mazingira ya mauaji ya Perez. Picha hizo zilikuwa zinatishana mwili wa marehemu ulikuwa umeharibiwa vibaya na umetapakaa damu. Majeraha ya kukatwa katwa na mazingira ya mauaji ya kijana huyo yalikuwa yanashabihiana na mauaji ya Perez.
Anawaeleza kuwa tarehe 9 mwezi wa 10 mwaka 2002 mwaka mmoja kabla ya mauaji ya Perez, Mike alipokea simu ikimtaarifu kuwa kuna tukio la mauaji katika eneo hilo la Fort Lauderdale. Mike anakimbia mara moja mpaka eneo la tukio na anakutana na mauaji ya kutisha. Marehemu alikuwa na majeraha ya kukatwa katwa kwa kisu shingoni, miguu na mikono ilikuwa imefungwa kwa kamba, mwili ulikuwa hauna nguo na pia ilionyesha kuwa alikuwa amelawitiwa kabla ya kuuawa. Marehemu anatambuliwa kupitia alama za vidolekuwa ni mwanafunzi wa chuo aliyejulikana kama Keese Gloth aliyekuwa na umri wa miaka 24.
Kwa mazingira yalivyokuwa maeneo yale Mike alijua moja kwa moja kuwa tukio hilo halikuwa la uvamizi au wizi, bali lilikuwa tukio linaloonekana ni la kulipiza kisasi kutokana na ugomvi au kutoelewana baina ya muuaji na aliyeuawa. Aliamini ya kwamba muuaji alikuwa anafahamiana na Keese kwa jinsi alivyomtesa na kumwingilia ilionekana dhahiri muaji alikuwa ana lengo la kumuua kwa mateso na maumivu makali. Pia muaji alisafisha eneo lote hivyo Mike na wenzake walikosa ushahidi na hivyo kushindwa kuendelea na kesi, ikabaki ikiwa haina muelekeo kwa muda wote huo mpaka alipokutana na akina Lawson na kumwambia juu ya mauaji ya Perez.
Kachero Lawson aliomba picha za za eneo la mauaji ya Keese, akazitandaza kwenye meza pamoja na picha za eneo la mauaji ya Perez, William na Lilian. Kwa kutazama matukio hayo waligundua jinsi muaji alivyofunga marehemu kunashabihiana, namna alivyowakata kata majeraha yanashabihiana na pia jinsia ambavyo aliweza kusafisha na kuondoka pasipo kuacha ushahidi kunashabihiana. Hawakuwa na shaka mpaka sasa kuwa wote wanamtafuta muaji katili ambaye huenda alianza kutekereza mauaji mwaka mmoja uliopita kwa kuanza na mauaji ya Keese Gloth.
Wiki mbili baadae.
Kachero Lawson na Borne wanaamua kuelekea kwenye eneo ambapo Perez alikuwa akifanya kibarua kabla ya kupotea na mwili wake kupatikana hotelini akiwa ameuawa. Wakiwa kwenye huo mtaa walikuwa na picha Perez na walikuwa wakimuuliza kila waliyemuona kama amewahi kumuona Perez kwa kumuonyesha picha na majibu waliokuwa wakipewa ni kwamba hawakuwahi kumuona. Walitumia muda mrefu wakiwauliza watu lakini mpaka inafika muda wa mchana juhudi zao hazikuwa zimezaa matunda na walikuwa wameanza kukata tama.
Lakini wakati Lawson akitazama sehemu za maegesho ya magari aliona gari ambalo linashabihiana na lile gari aliloona kwenye ile video aliyotumiwa ambapo gari la namna hiyo linalodaiwa lilijazwa mafuta kwenye kituo cha kujazia mafuta kwa kutumia kadi ya benki iliyoporwa baada ya mauaji ya William na James. Japokuwa ile video haikuwa na ubora wa kueleweka kuona kila kitu lakini james aliweza kugundua aina ya gari na alikuwa ana hakika ya kwamba lile gari lililokuwa pale kwenye maegesho ni sawa kabisa na lile gari aliloliona kwenye kile kipande cha video.
Lawson alimuonyesha Borne na kumwambia vipi ikiwa hilo gari ndilo lile linaloonekana kwenye kile kipande cha video. Borne alimwambia twende tukalikague huenda tukapata kitu na wote walielekea pale lilipokuwa lile gari. Borne alifika na kuanza kulipiga picha na kwa kulitazama kwa karibu lilikuwa sawa kabisa na lile gari waliloona kwenye kile kipande cha video. Lawson aliamua kuchukua namba ya gari kwa lengo la kuituma kitengo cha polisi kinachohusika na usajiri wa magari ili apate kujua mmiliki wa lile gari alikuwa nani. Lakini kwa muda waliotumia kuwa pale kwenye gari waligundua watu eneo hilo mmoja baada ya mwingine walikuwa wakiondoka eneno hilo.
Kwa kuhofia kuwa wanaweza kukosa mashahidi ambao huenda wana habari muhimu ya kuwambia ilibidi wasitishe kwanza zoezi la gari na kuendela kuhoji atu mbalimbali ambao walikuwa wakifanya kazi eneo ambalo Perez alikuwa akifanya kibarua lakini baada ya kuhoji kila mfanyakazi pale zoezi lililochukua masaa kadhaa na kutofanikiwa kupata taarifa yoyote muhimu ya kuweza kuwasaidia, waliporudi eneo walipoacha gari walipigwa butwaa kukuta lile gari limeondolewa na halipo tena eneno hilo.
Lakini bahati nzuri taarifa ilirudi kutoka katika kitengo cha kusajiri magari kwamba ile namba ya gari haikuwa imesajiliwa kwa gari bali kwa mtu binafsi ambaye anajulikana kama Henry Lee Jones. Polisi walirudi kwenye eneo ambapo Perez alikuwa akifanyia kazi na ndipo baada ya kuwatajia jina la Jones waligundua kwamba Perez na Jones wote walikuwa wamepangiwa kufanya kazi katika eneo la ujenzi hivyo ina maana walikuwa wanafanya kazi pamoja katika ofisi hizo. Na walipoomba kutazama kitabu cha maudhulio waligundua kuwa Jones alikhudhuria kazini siku ambayo Perez aliuawa.
Lawson ana Borne wanarudi ofisini na kuingiza jina la Jones kwenye mfumo wa kumbukumbu wa polisi ndipo wanapata taarifa ya kuvutia, kwamba kuna gari dogo jeupe ambalo linamilikiwa na Jones lilisimamishwa mara kadhaa na askari wa barabarani maeneo ya Tennessee na Mississippi na pia lilisimamishwa maeneo ya Melbourne Florida tarehe 25 mwezi wa nane 2003. Hii tarehe gari hilo liliposimamishwa mara kadhaa ilikuwa ni baada ya mauaji ya William na Lilian lakini ilikuwa ni kabla ya mauaji ya Perez.
Mauaji ya William na Lilian yalitokea tarehe 22 mwezi wa 8 2003 huko Brlett Tennessee, siku tatu kabla ya hilo gari jeupe kuonekana na kusimamishwa huko Tennessee, hapo hapo tena gari hilo likasimamishwa na askari maeneo ya Melbourne siku mbili kabla ya mwili wa Perez kugundulika katika hoteli hapo Melbourne. Hii haikuwa bahati mbaya polisi walikuwa na uhakika kuwa kuna jambo la uhusika wa moja kwa moja kwa mtu aliyekuwa akitumia hilo gari.
Na jambo la kufurahisha ni kwamba gari liliposimamishwa Melbourne, askari alimkamata muendeshaji wa hilo gari na muda huo alikuwa bado akiwa katika himaya ya polisi lakini mtu huyo hakuwa Henry Jones, bali aliyekuwa akiendesha gari alikuwa Yung. Polisi aliyesimamisha gari ajulikanaye kama kachero Carlos alibahatika kuzungumza na Jones lakini alimuachia aondoke na magari yake kwakuwa hakuona sababu ya kumkamata baada ya kugundua kuwa hakuwa na kosa lolote wala hakukuwa na taarifa yoyote toka polisi kuwa alikuwa ana tuhuma zozote.
Lawson na Borne wanaamua wakazungumze na Yung ambaye kwa muda huo alikuwa bado kashikiliwa na polisi, na wanafanikiwa kuandaa mahojiano naye. Katika mahojiano na Yung alionyesha kuwa na kiburi sana. Aliwajibu makachero kuwa mwenye gari hamfahamu yeye alilipwa kuendesha gari kutoka Tennesse mpaka Fort Louderle hakuuliza maswali mengi yeye alikuwa anatekeleza alicholipwa kufanya basi.
Wakiwa wamekata tama, katika kile chumba cha mahojiano alikuwemo kachero Carlos ambaye ndiye alihusika katika kumkamata Yung, Carlos anamambia unawezaje kufanya ulivyofanya Yung. Yung anauliza kufanya nini. Lawson anadakia uliwezaje kumtazama yule mama Mzee na mrembo kwenye macho yake kasha ukakata koromeo kwa kisu chako.
Hapo ndipo Yung alibadrika ghafla na kuanza kutetemeka kasha kusema “Sikumuumiza yule mama, naapa haikuwa mimi niliyemtendea vile.”
Carlos anamuuliza nini hasa kilitokea, Yung anamjibu haikuwa mimi na hapo ndipo anaanza kuwapa kisa jinsi mauaji yale yalivyotokea
bonyeza link iliyopo hapo chini subiri sekunde tano bonyeza next kuendelea kusoma sehemu inayofuata
Earn money on short links. Make short links and earn the biggest money - shorte.st