Wakaka mna nini lakini?

Wakaka mna nini lakini?

Meridah Tough

Senior Member
Joined
Nov 27, 2017
Posts
136
Reaction score
365
Dah!
Hapa duniani kuna mengi sana.

Kwa heshima naomba nitangulize salamu kwa jukwaa hili pendwa. Kwa kweli mkasa ambao umenipata, nitapenda kuuongelea ili iwe funzo kwa wadada wengine wadogo ambao wanapata changamoto hizi ndogondogo.

Hivi karibuni baada ya kuachwa na mwenzangu ambaye tulidumu muda sana katika mapenzi, tukipita changamoto mbalimbali hususan za kiuchumi, nafikiri mwenzangu alipata mtu mwingine. Nami kwa kuwa nilishachoka kuwa mpiganaji wa kulinda penzi letu, nikaona sawa tu, aende nipate pumziko kwingine, pengine hatukuandikiwa. Baada ya kama miezi 3, tukaanza mahusiano na kijana mwingine mtu mzima kidogo.

Kwa kweli, alinijali sana na kunipenda sana. Lakini katika maongezi ni kama tulikuwa watu wawili tofauti. Wakati mimi nikimwambia mategemeo yangu katika mahusiano yetu ni kutulia na kutokuwa na dramas, mwenzangu alikuwa anaongea kana kwamba tuna urafiki wa sex tu na and nothing. Sikuwa na pupa kujua nini alimaanisha.

Kwa bahati mbaya mwenzangu alipata changamoto fulani mambo ya msiba, hivyo akalazimika kubeba majukumu katika familia yao kipindi hiko cha Covid 19. Alinishirikisha nami bila hiyana nikaona nimsaidie jambo ambalo lilimshangaza sana kwani hakutegemea kama ningeweza kujitoa kiasi kile tena katika kipindi cha Covid 19.

Baada ya hapo, upendo uliongezeka ikawa too much sasa kwa uapande wake jambo ambalo mimi nikaanza kupata wasiwasi. Wasiwasi wangu ukazidi pale ambapo jamaa akaanza tabia za kuonyesha dalili zote za kutaka niwe nampatia pesa. Ingawa anafanya masihara lakini ni yale masihara ya kweli. Mara nina ndoto za kufanya hivi nitafutie pesa, mara nataka kile in the future kitatusaidia but kitakaa kwangu and so many dramas.

Kwa kweli maisha ya namna hiyo, nikaanza kupoteza interest naye. Sababu ninaamini kusaidiana kupo na ni jambo la kawaida katika maisha either ya mapenzi ama la, lakini mtu anapomchukulia mwenzake aliyemsaidia kama kitega uchumi, kwa kweli, kwanza inasikitisha lakini pili itakufanya upoteze trust kwa mtu. Hii ni kwa ke na me.

Mpaka sasa nina mwezi sina interest kabisa ya kumtafuta mwenzangu. Sina interest naye kabisa naona hata yeye amegundua hivyo na ndio maana hanitafuti.

Mwenye kuona funzo na aone.
 
Mbona umeandika nyuzi mbilimbili maudhui yaleyale.Umebadilisha title kidogo tu.
 
Noma sana tatizo wanawake huwaga mkimsaidia mtu Mnawekaa sana moyonii yani kinawaumaa balaa hata kama Ni mumeoo...!! Kama jamaa aliona pesa unazo kwa kuwa ulijionesha sasa why asikushauri mambo mazurii Japo hapo kuna mwisho mbayaa wa vilioo na kusaga menoo
 
Wamekukosea hao wawili unatujumlisha wote!..
Hi tabia ikome leo waambie na wenzako!

Mbona tupo wakaka tumetulia na hatuna mbwembwe kabisa!
 
Yaani wanawake nyie nomaaa sanaaa
Kwa hiyo ile ya yeye kukuchukulia kama mtu wakugegedana nae tuu wala haikukubugudhi ukaona poa tuu na ukaendelea....ila hili la kumsaidia mihela umeona hapana wacha nijiweke pembeni 🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Itakuwa jamaa alikuwa anagegeda vizuri na this speaks volumes kuhusu wanawake na mihela yao
 
Noma sana tatizo wanawake huwaga mkimsaidia mtu Mnawekaa sana moyonii yani kinawaumaa balaa hata kama Ni mumeoo...!! Kama jamaa aliona pesa unazo kwa kuwa ulijionesha sasa why asikushauri mambo mazurii Japo hapo kuna mwisho mbayaa wa vilioo na kusaga menoo

Yaani usijaribu ata siku moja mkeo akusaidie mihela....utakuja kujuta maana itakumbushiwa hiyo mpaka ukome.
Mara mie akukooeshe umrudishie lakini sio eti akupe alafu ndio iwe ntolee...utalia huko mbeleni.
 
Hajaliwa kimasihara kweli huyu..!???
 
Yaani usijaribu ata siku moja mkeo akusaidie mihela....utakuja kujuta maana itakumbushiwa hiyo mpaka ukome.
Mara mie akukooeshe umrudishie lakini sio eti akupe alafu ndio iwe ntolee...utalia huko mbeleni.
Mkuu achaa tuu mimi sijamuoa bado lakini naona kabisaa hizo isharaa...!! Ana kiwanja nikawaza akiuze tufanye maarifa lakini baada ya kuwa na mambo ya kukumbushia pesa alizowahi toa na pengine kusema nimrudishie lakini baada ya muda ananiomba msamaha ni mara kibao tu.. Nimejifunza yani huwaga siulizii tema kuhusu mali zake wala pesa kama sina bora nikope aisee...
 
Kama vipi nataka kwenda nawe kama vipi nataka toka nawe na kama vipi twende wote tamashani.......
 
msaada wa mwanamke ni wakuogopa sana, ukiupokea tarajia matangazo na masimango, mbona nyie mnatufanyaga vitega uchumi na tunatoa tu wala hatujali, we ungemsaidia tu.
 
Back
Top Bottom