Je ni sahihi kwa watu kumzonga na kumzomea mwanamke kwa mavazi yake

Watu wote wote wanamzomea kwa jinsi alivyovaa afu ww unaona sawa. Km vp hebu na ww vaa kinguo km hicho uone km utaweza hata kutoka nje.
wanaozomea sio wote ni wanaume ! mbona wao wakivaa yale masuruali yao yanayodondokea magotini na kuonyesha ch..pi, hawazomewi....huu ni unyanyasaji wa wanawake.
 
wanaozomea sio wote ni wanaume ! mbona wao wakivaa yale masuruali yao yanayodondokea magotini na kuonyesha ch..pi, hawazomewi....huu ni unyanyasaji wa wanawake.

Ni unyanyasaji wa wazi kabisa. Mbaya zaidi hata baadhi ya wanawake hawaoni kama ni unyanyasaji na wanamlaumu mhanga kwa kujisababishia hiyo kadhia.

Waliosababisha hiyo kadhia ni hao wahuni labda aje mtu aniambie kuwa huyo mdada alikuwa anawakatia mauno na akawachukiza. Zaidi ya hapo kwenye mzani wangu wa haki lawama zinawaangukia hao wahuni (thugs) entirely. I don't condone sexual harassment by placing blaming on the victim. Let others do that. Me not, never.

Halafu hiki kisanga cha huyu mdada kimenikumbusha wakati ule wa maandamano ya Tahrir square kule Misri. Moja ya vilio vya wanawake kilikuwa serikali ya Mubarak ililea unyanyaswaji wa wanawake.

Kuna waandishi kadhaa wa kike wa vyombo vya habari vya kimataifa ambao walikuwa wala hawajavaa vibaya lakini walikuwa wanazongwa kama hivyo alivyozongwa huyo dada na kushikwa matiti, ******, kuonyeshwa ishara za ngono, na kufanyiwa mambo mengine yanayoendana na unyanyasaji wa kijinsia.

Walivyotendewa hao waandishi ndivyo ambavyo wanawake wa Misri 'walivyozoea' kutendewa na hawana popote pa kwenda kupata msaada wa kisheria zaidi ya wao wenyewe, ndugu zao, ama wasamaria wema kuwasaidia. Unyanyasaji wa kijinsia Misri umeota mizizi kiasi kwamba mtendwa hana haki.

Ndiyo haya sasa ya kulaumu wahanga. Manake akipita tena mwingine anaonyesha cleavage yake basi ni kama vile 'rukhsa' kwa hao wahuni kumzonga kisa kakiuka tamaduni zao (ambazo hata hazieleweki). Moja ya dalili za failed states ndo hizi sasa. Watu kujichukulia tu hatua mkononi bila hata ya kuogopa adhabu toka dola kwa visingizio dhoofu kama utamaduni. Utamaduni gani wa kuzonga na kutisha watu?
 
ulikuwa wapi shosti manake nilishambuiwa sana
Wanaume wanataka shida zao ziwe ndio miongozo ya maisha yetu.

dah! Ungenistua kwa pm. Wanajishaua tu. Wanapenda sana tena vimini wananunua wenyewe. Tungepewa nafasi za kukutana na wapenzi /wake zao tungeona karibia wote wametupia miwigi kichwani na vipedo kabisa.
Nafikiri washakoma. Lol.
 
Tena wamezidi mamii
Kama ni chu** si za kwenu, wala haziwahusu
Kama ni utupu si wa kwenu, kinachowauma nini
Tembeeni hata uchi mwaya, wasiwabanie uhuru wenu

we shemeji ndio maana nakupenda. Kila kitu chetu ila bado wanakereka. Nyie tupigeni chabo tu. Si mnaangalia mnatuachia vitu vyetu.
Haviwahusu kabisa, watuachie viungo vyetu tuvifanye tunavyotaka.
 
wadada!tutaendelea kudhalilishwa mpaka lini?
Mbona wakaka wanataka kutunyima uhuru wa kuvaa tutakavyo.

Qn:vipi hii ikukutokea wewe shosti? Au mkaka vipi uko na demu wako ikamtokea hii ?

nani aliyetoa vipimo vya nguo fupi?serikali au ukame+ukata wa wavaa vitisheti vya ccm?inaanzia wapi?isoneshe kinii?
nguo fupi relative kwa nguo ipi?






iringa stendi ya mkoa​

au mnataka tuvae hivi ili muridhikeeeeeeeeeeeee​

jamani mbona wamasai hawazomewi? Wanavaa uchi uchi kuliko hao? Je kabila la wadzabe(samahani kama nimekosea spelling) nao je?
 
Ninawaza kama angekuwa mwanaume angefanyiwa hivyo.

Au wanaume ikija kwenye mavazi hawawezi kukiuka taratibu na mila za Iringa? Double standards....anyone?
 
Mkuu ulisema ushamaliza kumpigia mbuzi gitaa naona umerudi tena teteeeh.Kilichonivutia hapa ni mdada mmoja akimshukuru mwenzie kwa kumsuport maana wanaume wamemshambuli sana humu,safi saana. Hoja hapa ni wanaume wote (including Nyani Ngabu) ndio chanzo cha udhalilishaji huu.
 
Hoja hapa ni wanaume wote (including Nyani Ngabu) ndio chanzo cha udhalilishaji huu.

Yakhe tafadhali bana miye simo. Hao wadada ndo chanzo bana. Wanajisababishia wenyewe. Wajifunike kama wale wa Afghanistan na Saudia waone kama wataguswa. Teh teh teh teh
 
Wamisionari walivyokuja East Africa; waliwakuta waswahili Mombasa, wakawapa masketi na masuti waswahili na kuwaambia hii ni ushenzi tena ni dhambi kuvaa vitambaa vinavyositiri nyeti na matiti tu!

Over a century or so; Waswahili na masuti na matai; wakawakuta wazungu beach Mombasa wakiwa na swimming suits wakisunbath, wakawapa wazungu wale masuti na misketi na kuanza kuwahubiria jinsi gani ilivyo dhambi kuwa robotatu uchi!
 
Mimi niavutiwa na baadhi ya post zako nyani ngabu. Lakini pointi niliyotaka kubring home here ni kuwa hata wewe pamoja na juhudi zote bado hawakutofautishi? Kwa urahisi kabisa nilitaka kusema hakuna dhambi fulani ni maalumu kwa wanawake tu au wanaume tu. Kuwa mwanamke au mwanaume hakukufanyi kuwa bora au dhaifu. na ikitokea mchaga kaiba haina maana wachaga wote ni wezi. Ohoooo ni mfano tu! mbona Ngadu unanitolea macho?
 
kwani hapo unaona maumbile ya ndani?mbona wazungu wanavaa vikaptula chupi flani unawakuta mtaani wakijiacha sembuse hii

Kwa hiyo kitu akifanya "mzungu" ni sawa? Soon mtaanza kulana madenda hadharani na mtafunga ndoa za jinsia moja kama wazungu wanavyofanya. Hii copy and paste mh!
 
Hiyo nguo haina tatizo lolote.Ana uhuru wa kuvaa anavyotaka.Ufuska hautokani na nguo mtu anazovaa.
 
Hiyo nguo haina tatizo lolote.Ana uhuru wa kuvaa anavyotaka.Ufuska hautokani na nguo mtu anazovaa.

Hilo yaelekea wengi ni wagumu kulielewa. Na kilichofanyika dhidi ya huyo dada ni kosa kubwa mno kuliko hilo kosa analodaiwa kafanya yeye kwa kuvunja mila au sijui utamaduni. A total mismatch.
 
Kwa kuwa serikali haitaki kuwashughulikia wanaoharibu maadili ya mtanzania ni vizuri tu watu kama hawa wakiwa wanazomewa labda watajirekebisha tunaiga mambo ya wenzetu ambao utamaduni wao unawaruhusu tunasahau utamaduni wetu
 
Back
Top Bottom