Wajuvi wa DStv naombeni msaada hapa.

Wajuvi wa DStv naombeni msaada hapa.

Joined
Jul 18, 2017
Posts
90
Reaction score
119
Wakuu habari zenu. Heri ya sikukuu na poleni na majukumu ya kila uchao. Matumaini yangu mu wazima wa afya pamoja na familia zenu.

Msaada wenu tafadhali ili nami sikukuu yangu iende mswano.

Sikuwepo home kwa muda kidogo ile nafika jana nakutana na tatizo hili katika TV yangu ambayo natumia kisimbuzi cha DStv. Ukikiwasha kinaishia kwenye ku scan na hai scan baada kuna ujumbe inaleta.

Nimeambatanisha picha hizi hapa

IMG_20181226_084513.jpeg
IMG_20181226_084123.jpeg

Kulingana na ujumbe huo mimi nimeona tatizo lipo kwenye dish, hiyo LNB cable naweza kuisolve mwenyewe au mpaka nimuite fundi.

Wakuu msaada wenu leo mchana kuna game za Premier League na Seria A. Walau sikukuu iishie nyumbani siyo bar.
 
Jaribu kuangalia ule waya unaingia kwenye decoder kutoka kwenye dish kama umeingia vizuri, inaonekana hakuna mawasiliano kutoka kwenye dish.
 
Mkuu inaji update hio kwa leo itakua tayari jaribu kuiwasha
Kama itasumbua jaribu kui restart
 
Hilo ni dish limecheza signal zimepotea mtafute Fundi akurekebishea

Acheki cable kwanza ile inaingia kwenye decoder kutoka kwenye dish, huwa unachomoka na hiyo meseji inakuja hivyo pia.
 
Dish litakuwa limeyumba labda jaribu kuchek na mafundi kwanza usijifanye fundi
 
Pamoja na ushauri mzuri uliopewa. Mimi pia nakushauri kama utaona inafaa badilisha kingamuzi chukua Dstv ambacho ni HD, maana naona una Tv ya kisasa, utafurahi zaidi.
 
Back
Top Bottom