Wajumbe wa tume ya Katiba, Pendekeza nani awemo?

Wapo majaji ambao wamesomea contitunal law. Hao mara nyingi wanatumiwa na nchi za nje ili waanda mabadiliko ya katiba. Na wanajulikana sababu hawana upande watakao chukuwa na wanajali uzalendo Awachukuwe hao.

Kutaka wananchi au taasisi kupendekeza ni delay tactics tu.
 
ni muda wa mashoga nao kushiriki na kudai haki yao iwe ya kikatiba. Kazi ndo imeanza.

hilo sahau kabisaaaaaaaaaaaa. Ukinogewa na huo mchezo, wahamasishe wenzake mwende mkaishi kenya au ulaya na marekani.
 
Wapo majaji ambao wamesomea contitunal law. Hao mara nyingi wanatumiwa na nchi za nje ili waanda mabadiliko ya katiba. Na wanajulikana sababu hawana upande watakao chukuwa na wanajali uzalendo Awachukuwe hao.

Kutaka wananchi au taasisi kupendekeza ni delay tactics tu.

Mkuu mchakato wa muafaka wa kitaifa hauchukui siku 100.

Mkuu unataka hao Constitutional Lawyers wajifungie na kuandika Katiba kisha wailete kwa wananchi? Kutakuwa na tofauti gani kati ya katiba ya sasa na hiyo kw kuwa zote zitakuwa ni imposed constitutions. Tunataka Katiba ambayo itatokana na brainstorming of the highest level kwa maana ya asilimia kubwa ya wananchi kutoa mawazo yao hata kama ni ya kijinga. Wazo laweza kuwa la kijinga kwako lakini kwa mwingine si la kijinga na kwa kuwa nchi ni yetu sote na katiba itakuwa ni yetu sote basi hakutakuwa na wazo la kijinga hata moja. Kuna mkuu amesema mashoga nao washiriki; kwa kuwa ni Watanzania basi ruksa nao kutoa mawazo yao.
 
Tutakuja kufanya kosa kubwa kwa kudhani Kamati hii itaindwa na watu wa Dar es Salaam tu! na wasomi tu ama watu tunaowaona kwenye runinga. Hii Tume itakuwa inakusanya maoni toka kwa Watanzania wote hivyo ni muhomu ikawa na mchanganyiko maalum. Mimi napendekeza mkulima mmoja toka kijiji cha Kemondo anaitwa Mzee Kateme. Napendekeza mfugaji mmoja toka kijiji cha Mbuyuni huko Chunya anaitwa Masanja Mazuri. Mwisho nampendekeza mlima bangi mmoja toka kijiji cha Kemakorere anaitwa Mwita Gekerero Marwa.

ivi utakuwa na digree nyingi 2 wewe.a gues may be ur mr bashiru ally
 
Dr. Salim Ahmed Salim, awe mwenyekiti wa tume. Ni mtu wa kuheshimika sana na kujiheshimu! Ni muumini mzuri wa utawala bora, muungano wa kweli, mzalendo na demokrasia, si mwanasiasa wakulipiza kisasi na mwenye upeo! Huyu ataupa mchakato mzima kuaminika [credibility!]
 
TISS mumeshaanza!
Prof.Chris Miana, Bashirryy nawaunga mkono

Na mimi naomba niwemo plz plz.
Samahani kwa kujipendekeza mwenyew lakini naamini inarusiwa.
Naomba niwemo.

Niko tayari kujitegmea mwenyewe bila posho yoyote.
 
Napenda kukiri kuwa kwa jinsi TZ iliyo tajiri wa watu wenye vichwa nadhani hawa wafuatao watafaa:
1. Judge Barnabas Samatta
2. Judge Warioba
3. Prof Issa Shivji
4. Advocate Tindu Lissu
5. Ananilea Nkya
6. Helen Kijobisimba
7. Adam Mambi
8. James Bwana
9. Johnson Jason Meena
10. Obed Mwakitalika
11. Ridhwan J. Kikwete
12. Happiness Katabazi
13. Ayoub Ryoba
14. Adson Cheyo
15. Clement Mwashambwa
16. Patrick E. Chove
17. Ekwabi Mujungu
18. Zitto Kabwe 19. David Kafulila
 
Yaani Jf imevamia na vilaza siku hizi. Yaani mtu anatoa thread yenye maana watu wanaleta jokes. Eti mlima bangi, mpiga zeze. Acheni utani kama huna cha maana kalale sio kufuka utumbo hapa.
Mie napendekeza m/kiti wa kamati awe Shivji huyu mze Warioba anapwaya sidhani kama atakuwa na msimamo. Af prof. Kabudi na Bansen Bana wasiwemo hawa wanatumiwa na ccm, sina imani nao.
 
..naomba Salim Salim na Joseph Warioba wasiwepo.

..hawa ni waoga na watajaribu kila njia kuunusuru muungano.
 
Jenerali Ulimwengu..

Mussa Kundecha (shiekh)

Prof. Ibrahim Lipumba

Kardinali Pengo
 
Tume ya katiba inatakiwa kuwa na wajumbe 30 katika uwiano wa 15 Tanzania Bara na 15 Zanzibar!mchanganyiko wa watu kutoka makundi mbalimbali,taaluma mbalimbali,uzoefu mbalimbali ni muhimu sana lakini muhimu zaidi ni uwezo wa wajumbe kuwa wasikivu wa maoni, wachambuzi na wasioweza kuyumbishwa na chama chochote au dini yoyote au kundi lolote hivyo waweke mbele utaifa na kujari maoni ya watanzania na kuhakikisha maoni hayo yanaheshimiwa hii itakuwa ni enzi mpya katika Tanzania yetu.
 
Wanabodi kama tujuavyo Raisi Jakaya Kikwete amealika taasisi mbalimbali na wadau wampelekea mapendekezo ya majina ya watu ambao atafikiria miongoni mwao awateuwe wawe wajumbe wa Tume ya kukusanya maoni na kuandika rasimu ya katiba mpya! Nadhani haitakuwa vibaya kama tukijadili na kupendekeza nani anatufaa katika tume hii sauti zetu zina maana sana hata kama hatutapeleka rasmi lakini wengi wanatapita na kusoma humu hviyo naamini watatusikia tu.

Tume inahitaji watu MAKINI, WASIKIVU na WANAOJALI MASLAHI ya TAIFA. Kwa kuanza napendekeza wafuatao ambao sio wabunge na nadhani kati yao wangefikiriwa watatusaidia katika kuyajari maslahi mapana ya taifa letu :


  1. Wanahabari: Ayubu Ryoba, Hamisi Dambaya, Rosemary Mwakitwange na Joseph Mihangwa
  2. Wanataaluma: Prof. Chris Peter Maina, Mugongo Fimbo, Dr. Masumbuko Lamwai, Dr. Frola Kessy, Dr. Vicensia Shule, Dr.Honest Prosper Ngowi na Bashiru Ally
  3. Asasi za Kiraia: Jefred Myenzi, Usu Mallya, Ananelia NKya…
  4. Kutoka JF: Pasco wa JF ... Vyama vya Siasa: Prof.Mwasiga Baregu, Dr. Sekondo Mvungi na Prince Bagenda…
  5. Wanamichezo: Filbert Bayi…
  6. Wanasanii: Chemudu Ngwao, Irine Sanga na John Kitime…
  7. Viongozi wa Dini: Sheikh Mkuu wa Dar es Salaama-alhad Mussa Salum, Pd.Stevene Kaombwe
  8. Walemavu(physical challenged):...
  9. Wafanyabiashara:...
  10. Wanafunzi:...
  11. Wafanyakazi:..
  12. ...
Wengine wengi tubaki au wabaki katika kundi la watoa maoni, wahamasishaji wa watu kwenda kutoa maoni mbele ya tume, waelimishaji(elimu ya uraia hasa juu ya katiba) na wachambuzi kwa Mfano kama wakina Dr.Lwaitama, Prof Issa Shivji, Generali Ulimwengu, Mwanakijiji, Makwaia wa Kuhenga, Prof Kabudi, Heleni Kijo-Besimba, Dr. Kitila Mkumbo, Privatus Karugendo,Deus Kibamba n.k ningependa waachwe ili waje kutusaidia katika uchambuzi na ukosoaji wa rasimu itakapo kuwa tayari ili kuleta mawazo mapana zaidi.

Katiba ni jukumu letu sote tujenga misingi ya sasa na ya baadaye!tuna nafasi ya pekee sana ambayo HISTORIA haitacha kutusahau na kutuhukumu.

Je wewe mdau ungependa nani awemo katika kamati ya katiba?

Mawazo yako yapo sawa ktk baadhi ya maeneo ila tatizo lililopo ni madaraka anayopewa Rais kuteua kamati hii, kama ulisikia hotuba ya mwisho wa February alisema "makundi wapendekeze majina lakini wasishangae majina hayo kutokuwepo kwenye orodha ya watu 30 wanaotakiwa" hii ina maana yeye tayari ana majina ambayo ameandaa.
Kama uwazi ungelikuwepo majina yote yangekuwa wazi na yakapigiwa kura kutoka kila kundi husika, vinginevyo hilo ni bao la kwanza kwenye mchakato ambalo tumeruhusu lifungwe.
Tusikate tamaa tuendelee kuelimishana ili tuwe na Katiba iliyo bora kwa maslahi yetu na vizazi vijavyo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom