Wajumbe wa tume ya Katiba, Pendekeza nani awemo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wajumbe wa tume ya Katiba, Pendekeza nani awemo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tosha, Mar 4, 2012.

 1. Tosha

  Tosha Member

  #1
  Mar 4, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Wanabodi kama tujuavyo Raisi Jakaya Kikwete amealika taasisi mbalimbali na wadau wampelekea mapendekezo ya majina ya watu ambao atafikiria miongoni mwao awateuwe wawe wajumbe wa Tume ya kukusanya maoni na kuandika rasimu ya katiba mpya! Nadhani haitakuwa vibaya kama tukijadili na kupendekeza nani anatufaa katika tume hii sauti zetu zina maana sana hata kama hatutapeleka rasmi lakini wengi wanatapita na kusoma humu hviyo naamini watatusikia tu.

  Tume inahitaji watu MAKINI, WASIKIVU na WANAOJALI MASLAHI ya TAIFA. Kwa kuanza napendekeza wafuatao ambao sio wabunge na nadhani kati yao wangefikiriwa watatusaidia katika kuyajari maslahi mapana ya taifa letu :


  1. Wanahabari: Ayubu Ryoba, Hamisi Dambaya, Rosemary Mwakitwange na Joseph Mihangwa
  2. Wanataaluma: Prof. Chris Peter Maina, Mugongo Fimbo, Dr. Masumbuko Lamwai, Dr. Frola Kessy, Dr. Vicensia Shule, Dr.Honest Prosper Ngowi na Bashiru Ally
  3. Asasi za Kiraia: Jefred Myenzi, Usu Mallya, Ananelia NKya…
  4. Kutoka JF: Pasco wa JF ... Vyama vya Siasa: Prof.Mwasiga Baregu, Dr. Sekondo Mvungi na Prince Bagenda…
  5. Wanamichezo: Filbert Bayi…
  6. Wanasanii: Chemudu Ngwao, Irine Sanga na John Kitime…
  7. Viongozi wa Dini: Sheikh Mkuu wa Dar es Salaama-alhad Mussa Salum, Pd.Stevene Kaombwe
  8. Walemavu(physical challenged):...
  9. Wafanyabiashara:...
  10. Wanafunzi:...
  11. Wafanyakazi:..
  12. ...
  Wengine wengi tubaki au wabaki katika kundi la watoa maoni, wahamasishaji wa watu kwenda kutoa maoni mbele ya tume, waelimishaji(elimu ya uraia hasa juu ya katiba) na wachambuzi kwa Mfano kama wakina Dr.Lwaitama, Prof Issa Shivji, Generali Ulimwengu, Mwanakijiji, Makwaia wa Kuhenga, Prof Kabudi, Heleni Kijo-Besimba, Dr. Kitila Mkumbo, Privatus Karugendo,Deus Kibamba n.k ningependa waachwe ili waje kutusaidia katika uchambuzi na ukosoaji wa rasimu itakapo kuwa tayari ili kuleta mawazo mapana zaidi.

  Katiba ni jukumu letu sote tujenga misingi ya sasa na ya baadaye!tuna nafasi ya pekee sana ambayo HISTORIA haitacha kutusahau na kutuhukumu.

  Je wewe mdau ungependa nani awemo katika kamati ya katiba?
   
 2. m

  moma2k JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2012
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 953
  Likes Received: 984
  Trophy Points: 180
  TISS mumeshaanza!
  Prof.Chris Miana, Bashirryy nawaunga mkono
   
 3. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,691
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  wanamichezo,wasanii na JF wasihusike.
  Wanaharakati ndiyo kina nani?.... NGOs au?
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Tutakuja kufanya kosa kubwa kwa kudhani Kamati hii itaindwa na watu wa Dar es Salaam tu! na wasomi tu ama watu tunaowaona kwenye runinga. Hii Tume itakuwa inakusanya maoni toka kwa Watanzania wote hivyo ni muhomu ikawa na mchanganyiko maalum. Mimi napendekeza mkulima mmoja toka kijiji cha Kemondo anaitwa Mzee Kateme. Napendekeza mfugaji mmoja toka kijiji cha Mbuyuni huko Chunya anaitwa Masanja Mazuri. Mwisho nampendekeza mlima bangi mmoja toka kijiji cha Kemakorere anaitwa Mwita Gekerero Marwa.
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,197
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe mkuu, tusiwasahau wawindaji wa asili wanaozunguka Tanzania kutafuta malisho wawe na mwakilishi, watu ambao ni marginalized inabidi wawakilishwe pia. Sisi wa mjini ni maopportunists tutaweka mazingira ya kutufavour sisi na vikaragosi vyetu na kuacha maslahi ya mamia ya watanzania. Naamini huu mchakato utakuwa kijiwe cha kuponea, wastaafu wote watingizwa humu na Ndio watakaojaa.
   
 6. T

  Technology JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  Walioko magerezani wanaotumikia vifungo vya maisha au vifo,jeetu patel,babu wa loliondo nao wawemo
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,197
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Katiba ni ya watanzania wote, wakosaji na wasio na makosa, wafungwa na raia walio huru, Wasio waumini wa dini na washika dini, majambazi, malaya wa kiume na wa kike, watoto, wazee na vikongwe. Wagonjwa na hata wagonjwa wa akili. Katiba ni ya wote, tusiwe na dhana kuwa Katiba ni ya kikwete, kombani na werema na kwamba lissu anaingilia no no no please.
   
 8. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Kama hakuna Sinde Warioba na Shivji msinihusishe. Masumbuko lamwai simwamini hata kidogo. A Ryoba, na wachache ulowataja ni sawa. Sheikh na Askofu hawahitajiki kwa kuwa hatu tengenezi Bible takatifu wala Quran tukufu . Waacheni watu hawa wachunge kondoo zao kwa amani.
   
 9. R

  RMA JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ama kweli!! Nadhani wewe uko bado katika karne ya tano BC!! Ungekaa kimya usingepungukiwa kitu! Au ndio matunda ya sekondari za kata?
   
 10. m

  mharakati JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  majaji wastaafu msimsahau barnabas samatha anaongea sana sense siku hizi baada ya kustaafu nafikiri wakati wake alitaka kufanya kazi ila katiba ilimfunga sana kumfanya surbodinate mdogo tu wa Rais...watu kama hawa na experience yao ya high court wanafaa sana
   
 11. m

  mharakati JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  augustino ramadhani wasimweke kilaza kiana fulani haswa katika kuhahakisha power of judiciary against excutive branch
   
 12. m

  mzambia JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Lusekelo kibona wa ileje naye awepo
   
 13. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Mwigulu nchemba,mzee makamba,mrema,sheikh ponda,mchungaji mtikila,mama lwakatare,dk,manyaunyau,mh.ridh wan kikwete,bila kumsahau ndolanga upande wa michezo!
   
 14. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wanasiasa wastaafu, ma judge wastaafu, wataalam wa haki za binadam,watu kutoka asasi za kiraia, wanasheria. Na mwananchi wakawaida msomi kwenye field nyingine tofauti na sheria aweke balance.
   
 15. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Cpt John Komba na Prof Maji ni muhimu kuwemo hawa
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Wapiga zeze nao vipi mkuu tusiwahusishe kweli? Nadhani umenielewa kwa mujibu wa ID yako.
   
 17. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Jakaya mrisho kikwete asikose kwenye tume hii ;ni dokta;mwanasiasa shupavu;mtu wa watu;handsome na amesafiri sana anajua makatiba ya nje kinoma
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hawa wa asasi za kiraia huwa wamebeba mawazo ya wafadhili. Kuna watani zangu nimesikia wao wanataka bangi ihalalishwe na kuwa zao la biashara. Pia wanataka hukumu ya kifo itekelezwe hadharani. Hayo mambo sijui kama yamo kwenye misamiati ya asasi za kiraia! Tutafute muafaka wa kitaifa ndani ya katiba kwa kumsikiliza kila mtu. Hii inaanzia uwakilishi kwenye Tume na pia kwenye uhuru wa watu kutoa maoni yao wakati wa kukusanya hayo maoni ni mwishowe katika kuratibu maoni.

  Mkuu umenena kwa haki kabisa. Tusije tukajikuta tunawaangalia wasomi tuu na watu wengine wenye nafasi katika jamii.
   
 19. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #19
  Mar 4, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wanauchumi mpoo
   
 20. N

  Ngoiva JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni muda wa mashoga nao kushiriki na kudai haki yao iwe ya kikatiba. Kazi ndo imeanza.
   
Loading...