Wajumbe Bodi zote 50% Wanawake

Wajumbe Bodi zote 50% Wanawake

Ambiente Guru

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Posts
2,623
Reaction score
1,096
Ufisadi katika mashirika na taasisi za umma utapunguzwa kwa kiwango kikubwa pale tu asilimia kubwa ya wajumbe itafanywa na wanawake. Hili pia litaimarisha usawa wa jinsia.

Nchi kama Norway wanafanya hivyo na wamefanikiwa sana. Wanawake wanaweza. Naomba Mhesh Rais aanze na Bodi kama za Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro, TANESCO, TANAPA, TRA, TPA , Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nk
 
Hela ya mboga ya tibaijuka, kwani wakati anasema hivyo alikuwa mwanaume.

Issue hapo ni kuwabana tu na kama kuna aliekwisha husika anafirisiwa wakati huo akiwa anatumikia kifungo cha miaka isiyopungua mitano , wengine wataogopa wataacha kuchezea hovyo mali za umma.

Pia ni kuweka sheria kali kwa wahusika kama zilizopo china, ukihujumu mali ya umma wanakufire basi au kifungo, kufirisiwa na athabu kali weeee naimani hakuna atakae thubutu.
 
Hilo kamwe haliwezi kuwa suluhisho. Kwani sababu kubwa wa bodi kuwa na ufisadi imesababishwa na jinsi wajumbe na wenyeviti walivyoteuliwa. Kwa kweli naweza kusema ni kwa kujuana na kulindana ndio kulikokufikisha bodi kuwa na ufisadi. Kinachotakiwa zitangazwe nafasi watanzania waombe ifanyike interview na sio waziri kuteuwa anaowataka.
 
Hahahahaaa unanikumbusha akina Mama Anna mkapa na kina Salma Kikwete! Ufisadi hauna jinsia mkuu wangu
 
Ufisadi katika mashirika na taasisi za umma utapunguzwa kwa kiwango kikubwa pale tu asilimia kubwa ya wajumbe itafanywa na wanawake. Hili pia litaimarisha usawa wa jinsia.

Nchi kama Norway wanafanya hivyo na wamefanikiwa sana. Wanawake wanaweza. Naomba Mhesh Raisi aanze na Bodi kama za Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro, TANESCO, TANAPA, TRA, TPA , Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nk

Kwa ufanisi wa hayo mashirika utaletwa kwa mlingano wa wajumbe kijinsia?........
 
Wajumbe wa bodi TANAPA vikao vyao vyote wanafanyia Ulaya,,,jk aliiharibu sana hii nchi... Mkurugenzi wa TANAPA kila siku yupo Ulaya
 
Hawa ambao VITENGE na BUKU 2 ziliwatosha kwenye uchaguzi ndo-tuwaamini ?!
 
Ndo mdudu gani huyu? kama unawapenda sana peleka posa kwa wamama wote.
 
Ufisadi katika mashirika na taasisi za umma utapunguzwa kwa kiwango kikubwa pale tu asilimia kubwa ya wajumbe itafanywa na wanawake. Hili pia litaimarisha usawa wa jinsia.

Nchi kama Norway wanafanya hivyo na wamefanikiwa sana. Wanawake wanaweza. Naomba Mhesh Raisi aanze na Bodi kama za Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro, TANESCO, TANAPA, TRA, TPA , Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nk

Watu wengine mnatumiaga viungo gani kufikiri? UKE unasaidiaje kuzui RUSHWA
 
Hivi hao wanawake wa Norway ndiyo wanafanana na kina Tibaijuka na Mama Mkapa.
 
Fikiria tu bodi yenye mama wa hela ya mboga akiwa ndani.
Sasa atataka hela ya mkaa, unga au mchele, nyanya, vitunguu nk
Jinsi ya mtu si kipimo cha uadilifu!
 
M ininahofu na maamuzi yao wakiwakatika zile hali zao! so moody!wapunguzwe!
 
Wateuliwe kwa vigezo sahihi. Manake baadhi ya viongozi wanaume wanatumia madaraka yao kuteua watu wa kuwatumia tu kwa kupitia viti maalum,usawa wa kijinsia na vigezo vingine kama hivyo. Ukweli ni kuwa wanawake tunaweza,wabunge wachache wa kuchaguliwa na wananchi wanatoa picha kuwa. kuwa na vigezo,kujiamini,kujiandaa na kusimamia maslahi ya wananchi ndio sifa sahihi za kupewa nafasi za uongozi au hata bodi. Nachukia kwa dhati ya moyo wangu upendeleo wa kijinsia,ni aina nyingine ya unyanyasaji,nimeliishi hilo.
 
M ininahofu na maamuzi yao wakiwakatika zile hali zao! so moody!wapunguzwe!

Kwa hiyo hizo moods za siku zao zinakuwepo kila siku? siku za vikao vya bodi ndio siku na wao wanakuwa kwenye siku zao kila mara? mama yako amekuleaje kama akiwa kwenye moods hakuwa anafanya yaliyo sahihi?? Mnapenda sana kutumia hali na wajibu ambao Mungu ametuumba nazo kuonyesha hatuwezi. Ila sasa ndio hivyo,hedhi tutakuwa nazo,mimba tutabeba,kulea tutalea watoto,waume na familia zao na bado taifa nalo tutaendelea kulijenga kwa uaminifu.
Hatupunguziki,sio kwa kusoma huku kwa sasa,na kujiamini huku. Mlipo tupo na majukumu ya kiuongozi mnayoweza nasi tunaweza na ndio kwanza tumeanza.
 
Hawa ambao VITENGE na BUKU 2 ziliwatosha kwenye uchaguzi ndo-tuwaamini ?!

Sijawahi kumfikiria mwanamke kabla ya mwanaume katika haya mambo ya namna hii labda ikitokea kwa bahati mbaya
 
Back
Top Bottom