Wajumbe baraza la Wawakilishi(CUF-Zanzibar) kuishtaki SMZ

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,710
3,669
image.jpeg
UKISIKIA Balozi Seif Ali Iddi kuchezeshwa ALIFOLA ALIFOLA kweye siasa basi ni huku. Ukiujuwa huu na wezako wanaujuwa huu.

Mgogoro wa uchaguzi visiwani Zanzibar umeingia katika sura nyengine baada Wawakilishi na Madiwani wateule wa Chama Cha Wananchi CUF kufikiria kwenda mahakamani kutetea uongozi wao.

Wamesema tayari Wawakilishi na Madiwani hao wateule walishachaguliwa na kukabidhiwa hati zao za ushindi kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, na kwamba hadi sasa hakuna mgombea wa nafasi hizo kutoka chama chochote aliyekwenda mahakamani kupinga uteuzi wao.

Msimamo huo wa CUF umetolewa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, katika mkutano maalum wa Chama hicho uliofanyika viwanja vya “nngoma hazingwa” Chake Chake Pemba.

Mkutano huo umewajumuisha viongozi wa Wilaya, Majimbo na Jumuiya za Chama hicho Kisiwani humo ambapo mkutano kama huo ulifanyika jana kwa upande wa Unguja.

Maalim Seif ambaye alikuwa mgombea Urais wa Chama hicho amesema viongozi hao waliochaguliwa na wananchi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015 na kupewa shahada zao, watakwenda mahakamani kutetea nafasi zao, na kutoruhusu viongozi wengine wa ngazi hizo kuchaguliwa tena kwa vile wao wanavyo vielelezo vyote vya kuchaguliwa kwao.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi yaliyobandikwa katika vituo vya kupigia kura na kuthibitishwa na wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo, majimbo yote 18 ya uchaguzi Kisiwani Pemba yalichukuliwa na CUF, sambamba na wadi zote 32 za uchaguzi.

Katika hatua nyengine Maalim Seif amewapa matumaini wafuasi wa Chama hicho kwamba atatangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa Oktoba 25, 2015 na hatimaye kuiongoza Zanzibar.

Amerejea kauli yake kuwa wanachokifanya watawala hivi sasa ni kuchelewesha kumtangaza, lakini hakuna namna yoyote ya CCM kuendelea kuongoza Zanzibar baada ya uchaguzi wa 2015 na kwamba uongozi uliopo hivi sasa ni batili kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Amesema Jumuiya na waangalizi wote wa uchaguzi wa kitaifa na kimataifa wameshuhudia uchaguzi huo na kujiridhisha kuwa ulikuwa huru, haki na wa uwazi na wanaendelea kushikilia msimamo wao kutaka mshindi wa uchaguzi huo atangazwe.

Amesisitiza kuwa Chama chake hakitoshiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20/03/2015, kauli ambayo pia imeungwa mkono na wafuasi wa Chama hicho kisiwani Pemba, kama ilivyokuwa kwa upande wa Unguja.

Mapema Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui, amemtaja Maalim Seif kuwa kiongozi aliyebobea kisiasa na anayejali maslahi ya Wazanzibari.
 
Sheria ziko wazi wazi kabisa hakuna aliyewapinga na jecha hana uwezobwa kuwafuta maana msimamizi wa jimbo ndio anamamlaka ya mwisho na sio jecha
 
Kama kawaida cuf na maigizo.
Muda wote kina Paco wanawahimiza kwenda mahakamani walau waoneshe kuna utaratibu haukufuata wao wakazembea wakamsubiri sefu.
Kuwa na cheti sio tiketi,watu wanaingia bungeni,wanakopa baadae wanavuliwa ubunge itakua hao hata kuapa hawakuapa.
Kwa kua uchaguzi umefutwa,basi hivyo vyeti ni sawa na karatasi za chooni
 
Hivi ni kweli kuwa JPJM hawezi kuingilia kati mgogoro huu ukizingatia kuwa yeye, JPJM, ni raisi wa JMT? Je, inawezekana kuwa ni kweli kuwa raisi ni wa Tanganyika iliyovaa koti la Muungano?

Mimi nafikiri JPJM anaweza na anatakiwa walau kutoa tamko/ushauri kuhusiana swala hili!!
 
Mkuu, hakuna uchaguzi wa marudio Zanzibar zaidi ya ule wa tarehe 25/10/2015!!

Na kama manataka mumuone Jecha Salum Jecha mahakamani, this is a very smart move.......mtamuona akiwa shahidi!!

Maalim Seif Shariff Hamad anawazidi akili CCM kwa mbaali sana na kwa hakika, wameshika weee lakini mwishowe wataachia tu!!
 
Vizuri unavyojifariji unajingezea afya njema
 
Hivi ni kweli kuwa JPJM hawezi kuingilia kati mgogoro huu ukizingatia kuwa yeye, JPJM, ni raisi wa JMT? Je, inawezekana kuwa ni kweli kuwa raisi ni wa Tanganyika iliyovaa koti la Muungano?

Mimi nafikiri JPJM anaweza na anatakiwa walau kutoa tamko/ushauri kuhusiana swala hili!!
Haiingii akikini hata kidogo tunapoambiwa na maccm kuwa JPM hana ubavu hata kidogo wa kuingilia maamuzi yaliyofanywa na Jecha wa ZEC.

Lakini hapo hapo tunaambiwa kuwa maccm hayo hayo yalimuunga mkono kwa asilimia 100 JK wakati alipo-influence Jecha aufute uchaguzi uliofanyika tarehe 25/10/2015 kwa uhuru na haki!
 
Mkuu, hakuna uchaguzi wa marudio Zanzibar zaidi ya ule wa tarehe 25/10/2015!!

Na kama manataka mumuone Jecha Salum Jecha mahakamani, this is a very smart move.......mtamuona akiwa shahidi!!

Maalim Seif Shariff Hamad anawazidi akili CCM kwa mbaali sana na kwa hakika, wameshika weee lakini mwishowe wataachia tu!!
Mkuu pole na kazi, kwa akili tu ya kawaida, ambayo si ya kushikiwa uchaguzi haukwepeki zanziba na tarehe 20,match, sasa unahaja ya kupiga kula u kutokupiga kula

Na pengine nikukumbushe kuwa cuf wanatafuta haki kwa 100%ambayo hata amerika haipo, hvyo hyo nindoto ya mchana ambayo haiwezekan kuwa kweli..

Innauma illa ndiyo tiba, uchaguzi ni lazima si ombi mkuu, ila kupiga kula ni hiar
 
Kwanza, masahihisho; tunapiga "kura" na siyo "kula".

Pili, kuchagua viongozi wetu kwa njia ya chaguzi huru na za kidemokrasia ni jambo muhimu na la lazima sana na ndiyo maana tulitoka kwa wingi tarehe 25/10/2015 tukapiga kura na kuchagua viongozi tuliowataka kote bara na visiwani!

Nimesema toka mwanzo kuwa hakuna UCHAGUZI wa marudio huko Zanzibar, bali kinachotaka kufanyika ni UCHAFUZI na ndiyo maana wewe unasema "watu kwenda kupiga 'kula' ni jambo la hiari".

Ni hiari kwenu kwa sbb mnataka kuchafua hali ya hewa huko Zenj, nothing more.....nothing less!!

Trust me ndugu yangu; uchaguzi halali na unaotambulikana kisheria na kikatiba ulishafanyika tarehe 25/10/2015 na matokeo yooote kwa upande wa wabunge, wawakilishi wa BLW na madiwani/masheha yalitangazwa yote with eceptional of presidential results for 23 constituencies!

Tunataka mtuambie sasa, ni nani miongoni mwa wagombea walioshindwa waliamua kwenda kupinga ushindi wa walioshinda mahakamani kama sheria na katiba inavyotaka??.......Najua huna jibu na wenzio wote hawana majibu katika hili!!

Isipokuwa nikusaidie mimi jibu la swali hilo kwa herufi kubwa kabisa kuwa, "HAKUNA" isipokuwa Jecha S. Jecha mwenyekiti wa ZEC ndiye mlalamikaji, ndiye msikiliza malalamiko na ndiye mtoa hukumu/maamuzi. Sijui ni kwa mujibu wa kifungu gani cha sheria na katiba ya Zanzibar!!!

Tunaposema CUF are smarter than Jecha na CCM hamuelewi. Nafikiri muda ni mwamuzi mzuri sana, ukifika, basi mtaelewa tu. There is no other way...........Hakuna uchaguzi wa marudio Zanzibar labda nyie muwe mnaishi sayari ya Mars na sio hii ya Dunia. Na kama ishu ni kutaka kuleta UCHAFUZI wa hali ya hewa tu huko Zenj, watu wako tayari pia kwa hilo!!
 
Iyo kes wanafungua kenya au mahakama hizi za ccm

Ni hizi hizi za CCM mkubwa!

Na ifahamike kuwa kuna wakati mahakimu au majaji huona aibu kupindua haki iliyo wazi na dunia nzima ikiwa inaona!!

Kwa kesi hii, mahakimu na majaji wa mahakama hizi za CCM, hawana option nyingine bali ni kuamua kwa haki, else............
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom