Wajue waliong’oka ama kukimbia PPF ya Erio kwa sababu mbalimbali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wajue waliong’oka ama kukimbia PPF ya Erio kwa sababu mbalimbali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kimi, Feb 17, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. k

  kimi Member

  #1
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1. Bw. William Chenza (Mkurugenzi): Huyu alifikishwa mbele ya Bodi ili afukuzwe lakini bodi ikaona hakukua na sababu za kumfukuza wakati huo. Baada ya hapo akawa hashirikishwi kwenye kazi za uwekezaji na mipango. Mazingira ya kazi kwa Bw. Chenza yalikuwa magumu sana akaacha kazi. Kwa sasa baada ya kuona hawezi kuajiriwa ameamua kuwa mjariamali na sasa anaendesha shule.

  2. Bw. Oscar Mwachang'a(Mkurugenzi) : Huyu alifariki tayari akiwa amefikishwa mbele ya Bodi ili afukuzwe kazi. Alifariki kabla hajafukuzwa kazi. (kifo cha kawaida)

  3. Bw. Michael Mjinja (Mkurugenzi): Huyu alifikishwa mbele ya Bodi ili afukuzwe kazi. Bodi ilikataa na akarudi kazini lakini akawa anafanya kazi katika mazingira magumu sana. Aliwekwa pembeni kwenye mambo mengi. Hatimaye alikuja kufukuzwa "technically". Kurugenzi yake iliunganishwa na Kurugenzi nyingine akaambiwa akitaka aombe. Aliomba kazi hiyo akaitwa kwenye interview lakini akashindwa na msaidizi wake.

  4. Bw. Baduru Msangi: (Mkurugenzi) Mzee huyu bahati mbaya hakuwa amempenda muda mrefu tu. Lakini kwa kuwa mzee huyu alikuwa hana makuu na watu hakuweza kupata sababu za kumshitaki kwenye bodi. Yeye aliondoka technically. Idara yake iliunganishwa naye kama ilivyokua kwa Bw. Mjinja akaambiwa akitaka aombe. Aliomba akaitwa kwenye interview akapigwa chini.

  5. Bi. Irene Isaka (Meneja): Huyu baada ya Bw. Chenza kuondoka yeye ndiyo alikuwa awe Mkurugenzi, alienda Benki ya Stanbic na baadae SSRa ambako sasa ni DG wa SSRA.

  6. Bi Carina Wangwe (Mkurugenzi): Ameenda SSRA (hajafukuzwa).

  7. Bw Emmanuel Kakuyu (Meneja): Aliondolewa kwa tuhuma mbalimbali. Kumekuwa na madai kwamba yeye ndiye anatuhumiwa kutoa siri nje.

  8. Bi Siriel Mchembe (Meneja): Ameachishwa kazi akituhumiwa kutoa siri nje ya PPF.

  9. Bw. Kedron Mbwilo (Meneja); Alikua idara ya Uhasibu akahamishiwa idara nyingine kabla ya kuhamishiwa Mbeya kabla ya kuondolewa kazini moja kwa moja.
   
 2. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Na wewe inaelekea uko ndani ya PPF. Kama wenzako walifukuzwa kwa kuleta mambo ya Erio hapa JF, wewe huogopi kufukuzwa?

  Tiba
   
 3. +255

  +255 JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,909
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Hao walikuwa Wakurugenzi na Mameneja wa idara gani?!
   
 4. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Huwezi kukaa kimya wakati huna amani moyoni, kuna mambo yakuweka moyoni, na kuna mengine utajikuta yanakukondesha na kuona bora uyaseme ili upate kuwa na amani.
   
 5. M

  Mpendakwao Member

  #5
  Feb 17, 2012
  Joined: Mar 29, 2007
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Once again, nazidi kuthibitisha kuwa hii issue is more within 'personal interest' than 'public interest'. Kwanza kwa claim za kuwa mie ni insider!!! Well for your information am not. Sorry!!!, But the only reason why I am a member of this forum is to read everything thoroughly, and make my own informed judgement.

  Thread imewataja watu watatu 'Walionewa' Moja kafa wengine wawili waliaachishwa kazi, lakini moja tunaambiwa anafanya kazi mahala fulani, ila kati ya wawili walioonewa, MJINJA hatukuambiwa kuwa ana kazi nyingine, this to me implies, MJINJA ndiyo Commander wa mpambano haya dhidi ya ERIYO. If am wrong from my deductive analysis, please correct me. I am humble enough to apologise. Lakini, I feel that hii isssue ni mtu anapambana na mtu ,ila anataka ulimwengu wa WaTanzania tuaamini kuwa there is a 'Smoking Gun".

  Kifupi:

  Matatizo ya PPF yanayoendelea sasa ni muendelezo wa matatizo ya muda mrefu sana tokea wakati wa David Mataka na baadae Naftali Nsemwa na baadae William Erio na yataendelea kwa anayekuja kama hatua madhubuti hazitachukuliwa. Kwa sasa baadhi ya waathirika na wenye malengo binafsi wamekua wakitumia JF ama kuwatumia wana JF kupenyeza mambo yao na kutia chumvi baadhi ya matukio na mengine kuyarudia rudia na wengine hata kutumia lugha zisizofaa katika JF.

  Matatizo haya yanasababishwa na mambo mengi, lakini mawili ndio naona ni makubwa;

  1- Ni tamaa ya madaraka miongoni mwa watumishi wanaoamini kwamba wanaweza kuwa Wakurugenzi na;

  2- Ni watu wa nje ya PPF ambao wana maslahi ndani ya PPF wakiwamo wafanyabiashara, wanasiasa na wataalamu washauri ambao kwa namna moja ama nyingine wanapigania maslahi yao. Katika kundi la wataalamu washauri wamo wanajifanya ni wataalamu wa upelelezi na huchukua dhamana kwa mambo ambayo baadaye hulazimika kutunga uongo waweze kulipwa kwa kazi husika. Hii imewagharimu wengi sana hata walio nje ya PPF.

  Nitawajadili Baadhi ya watu waliotajwa na mtoa mada na nitajikita kwa vinara;

  A-William Chenza- Huyu anaitwa Charles Chenza na si William na ni mtu makini na mwenye uwezo na amekuwa na uzalendo mkubwa katika kipindi kirefu alichokuwa PPF (amewahi kugomea ufisadi wa Sh bilioni 200), lakini kwa bahati mbaya sana ameathiriwa na matukio yaliyomgusa na ambayo yamemlazimu sasa kujiingiza kwenye makundi ambayo badala ya kumsaidia sasa yanamtumbukiza kwenye matatizo zaidi na yanaweza kuathiri hata biashara zake za sasa asipokuwa makini na watu wanaotumia jina lake vibaya.

  Chenza alikua na madaraka ya juu wakati Erio akiwa ni mwanasheria wa PPF chini ya DG Naftali Nsemwa. Wakati Erio anapata madaraka, alimuamini sana Chenza na wasaidizi wake wengine ambao hakuwa na hiyana kuwaachia ofisi na mamlaka makubwa anaposafiri.

  Kinachomsumbua Chenza hadi akawa anashindwa kupata nafasi za juu anakijua lakini kama ni msomaji wa JF nitamgusia tu kama anakumbuka yaliyomtokea pale aliposalitiwa na mwanataaluma mmoja aliyekuja pale PPF na baadaye kukiuka maadili ya kazi yake na kwenda kutoa siri iliyomsaliti Chenza. Baadaye Chenza aliitwa na kuhojiwa na TIS kabla ya jalada lake kuchafuliwa vibaya sana. Tukio hilo ndilo liliwalazimisha TIS wamtake Gray Mgonja aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya PPF na Katibu Mkuu Hazina amchukulie hatua Chenza huku kukiwa na mkono mkubwa wa mfanyabiashara ambaye alikosa dili la Sh bilioni 200. DG Erio hakuweka msisitizo wa kuchukuliwa hatua kwa Chenza maana hata maamuzi aliyoyafanya Chenza kukataa dili la Bilioni 200 aliyabariki na hivyo bodi haikumfukuza Chenza. Bahati mbaya sana Chenza akaona kama Erio amemsaliti na akaendelea kujenga chuki, lakini kwa kuwa naye (Chenza) ana kiunganishi TIS anajua fika jinsi jalada lake lilivyochafuliwa hata wakati alipoomba nafasi ya Ukurugenzi LAPF (ambayo anastahili) aliponzwa na jalada kuwa chafu. Chenza alijua fika hataweza kuajiriwa serikalini hadi atakaposafisha jalada lake na kwamba angeendelea angeweza kupata matatizo zaidi na ndipo alipoamua kuacha kazi na kwenda kuwekeza kusini mwa Tanzania katika mradi mkubwa wa Shule. Anajua alikopata mtaji manaa si mjadala wake hapa.

  Yapo mengi yanayomhusu Chenza na wenzake, lakini hii vita dhidi ya Erio haiwasaidii sana, japo inaweza kumgharimu Erio hapo baadaye kutokana na hulka ya binadamu kuamini jambo linalorudiwa rudiwa mara kwa mara hata kama halina uzito unaostahili.

  B. Michael Mjinja: Huyu, amekuwa ni mtu mwenye malengo makubwa na amekuwa akijiamini kupita kiasi katika utendaji wake pamoja na kuwa na watu wengi wanaomuunga mkono (kwa sababu anazozijua). Ameonyesha uwezo mkubwa kote alikopitia na amejiendeleza na amepata uzoefu wa kutosha, lakini naye historia yake alikotoka kuanzia TRA, VETA, EPZ na kadhalika amejijengea maadui wengi ambao naye kwa bahati mbaya amewasahau au anawadharau na anashindwa kutambua alikojikwaa na anaangalia alipoangukia (PPF) wakati wale watu ambao hawakumbuki wana nafasi muhimu katika vyombo vya maamuzi japo kwa siri sana na ndivyo vinavyozidi kumkwamisha katika malengo yake makubwa anayostahili kama atatulia. Mjinja arudi nyuma alikotoka aangalie alijikwaa wapi ili asafishe njia, maana anaweza kufanikiwa kama hataendelea kujijengea maadui kwa kupambana na watu. Vita nzuri ni ya kupambana na mfumo si mtu. Mjinja na wenzake, ambao bahati mbaya sana wanaitumia JF kama uwanja wao, wanashindwa kuelewa kwamba Erio ni binadamu na ni mtu mmoja na hawezi kuwa na uwezo wa Kimungu kuwazuia kila mahali wasifanikiwe na kwamba hatakua DG milele pale PPF, ataondoka kama kina Mataka na Nsemwa na watakuja wengine ambao hakika hawataweza kuwarudisha PPF na badala yake watawaangalia kwa jicho la woga. Mjinja yeye anaamini kwamba anaweza kuwa Mkurugenzi mzuri wa PPF kuliko Erio na ndio maana anamdharau na kujenga chuki jambo ambalo nalo ni mjadala. Mambo mengine ni binafsi na hayana nafasi humu yakiwamo mambo ya mahusiano ambayo baadhi wanayatumia vibaya JF.

  C. Badru Msangi: Kusema kwamba Erio hakuwa akimpenda ni jambo linalotia shaka maana amewahi kumuchia nafasi ya kukaimu mara kadhaa na akiwa amemuachia kwa kumuamini mambo nyeti ambayo angeweza kusema atayafanya atakaporejea safarini. Msangi aliteuliwa na Erio kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni ya PPF nafasi ambayo ni nyeti sana na wote wanajua kiasi kwamba watu waliamini kwamba amependelewa na Eruo. Sisi tuliokuwamo ndani ya PPF (wakati huo) tulidhani kwamba mzee Msangi ni mtu wa karibu sana na Erio. Suala la kubadilishwa muundo ni mchakato ambao haufanyiwa na DG na kwamba hata wao (Mjinja na Msangi) walikwa sehemu ya mchakato na waliamini kuwa watabebwa kwa kuwa karibu na DG na walipewa imani na watu wengine wa nje na wa wanawajua japo walikuwa hawana uwezo. Wenzao walifanya jitihada na wakajiandaa vyema kwenye usaili na wakashinda wao walijiamini sana. DG hana kauli ya mwisho katika usaili na wao wanajua, lakini walikasirishwa na Erio kutowatetea na kuacha washindwe na watu waliowaona hawana uwezo.

  D. Irene Isaka: Kuondoka kwake PPF na kwenda Stabic (si Backlays) hakukutokana na matatizo, bali ilikua ni mikakati yake ya kujiendeleza na kupata uzoefu na maslahi zaidi, na ndicho kilichomsaidia kufanikiwa kuwa DG wa SSRA. Kama angeondoka PPF vibaya asingeandikiwa barua ya siri ya kumwagia sifa kemkem kuwa anaweza kuongoza SSRA ambako amewachukua baadhi ya watumishi wenzake wa PPF kwenda kumsaidia kazi.

  E. Carina Wangwe kama alivyo Irene Isaka huyu ameenda SSRA kufuata maslahi zaidi na hajafukuzwa PPF. Carina kitaaluma ni Mwalimu na aliona akiwa PPF ambayo ina kazi nyingi za kila siku, asingepata muda wa kufundisha baada ya kujiongezea elimu. Kwa sasa anafanya kazi SSRA na kufundisha.

  F. Kedron Mbwilo; Huyu anaweza kuwa chachu ya chuki na mlolongo wa mambo yanayoendelea PPF kwa sasa maana alikuwa kitengo cha Uhasibu chini ya Mkurugenzi wa Fedha Martini Mmari, na taarifa ni kwamba walitofautina na ugomvi halisi ulikua kati ya Mbwilo na Mmari na si Mbwilo na Erio. Mbwilo aligomea kuidhinisha malipo ambayo bosi wake aliidhinisha na wakurugenzi wote waliridhia na hapo ndipo 'bifu' likaanza hadi leo. Erio alipoona Mbwilo hana maelewano na bosi wake akatafuta sababu na kuhamisha lakini hakutaka kuweka public ugomvi wa wenzake. Hilo nalo Mbwilo analijua lakini anafunika.

  Kwa hayo machache, naamini wana JF wawe makini na maugomvi na maslahi ya watu kuhamishiwa JF kwa kisingizio cha kupambana na ufisadi.
   
 6. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  bado bado bado.........ukiona simba kaingia njini!!!!
   
 7. Ikwanja

  Ikwanja JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  kwahiyo huyo DG atakuwa analingwa na nani, ina maana bado analindwa na mjomba wake Mkapa? Malipo hapa hapa!!
   
 8. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  hawa ndo wanasababisha fomula igome na kulipa maprofesa pensheni ya milioni 7! wakati NSSF walimu wa msingi wanakula 30 mil!

  kuna shida.....nahisi PPF ni kiota cha mafisadi!
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kuna vitu kidogo vinanipa shida:

  No 2. Oscar Mwachanga alikufa lini na Erio alishika lini huo wadhifa? Na kama alikuwa amefikishwa mbele ya bodi ni kwa nini? Kifo chake kinatokana na huyo Erio?

  No 3. Kuhusu Mjinja unasema idara yake iliunganishwa na aliomba kazi hiyo akaitwa kwenye interview lakini akaambiwa ameshindwa na msaidizi wake ambaye uwezo wake mdogo sana. Nani alikuwa anafanya hiyo interview? Ni huyo Erio peke yake? Kama ni zaidi ya Erio, hao watu wanalazimishwa kufanya atakayo Erio?

  No 8. Unasema Serieli Mchemba ni mtu straight, aliyekuwa hapendi kujipendekeza kwa uongozi na ambaye spade alikuwa anaiita spade. ah ah aha ah ah... Sirieli Mchemba straight? Sirieli Mchemba mtu asiyependa kujipendekeza?
   
 10. T

  TRIX New Member

  #10
  Feb 17, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ufisadi kila kona
   
 11. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #11
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Jinsi nilivyokuwa nikiendelea kusoma ndivyo nilivyokuwa nikiendelea kuamini kuwa hii itakuwa ni kweli walau 99%!
   
 12. kibai

  kibai JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 201
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Umemsahau Kang'ombe Patrick! Hakuwa meneja but intelligent
   
 13. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kwani hakuna sehem hawa watu wakapata kulalamika na haki zao zikasimamiwa?
  Au wanamakosa kweli?
  lakini mengine nayaona minor kabisa et kamwandikak atika mtandao!!

  Kwanini akasilike kama si kweli?
  Mtu asiyemuovu hawezi kuamaki hovyo!

  Mh huyu bro, nouma sana!
   
 14. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  No. 2 Hajasema Erio alisababisha kifo chake bali anasema alimpendekeza kwenye bodi ili afukuzwe na akafariki kabla ya bodi haijakaa.
  No. 3 Kumbuka Erio ni DG yeye ndio mwenye maamuzi ya mwisho kwenya Interview na kwa tabia yake (kama anavyoeleza ndivyo ilivyo) hata hiyo interview ilikuwa ni udhalilishaji tu na kuonyesha kwamba yeye ndiye bosi.
  No. 8 Kama huyo dada hayuko straight sema basi maake inaelekea unamfahamu badala ya kuuliza kwa mshangao!!

  Ila pamoja na kwamba huyo Erio ni mjomba wake Mkapa lakini akumbuke pia hiyo kazi hatafanya milele, na kwa namna anavyojitengenezea maadui wengi ajue kwamba siku moja na yeye atashughulikiwa after all malipo ni hapa hapa duniani hata uwe fisadi vipi!!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...