Waziri Makamba: TANESCO mpya imezaliwa leo, tunataka iendeshwe kibiashara

I wish i have

Senior Member
Nov 2, 2021
136
62
Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba amesema ni wakati sasa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kuanza kujiendesha kibiashara, kwa ufanisi ili kuchangia uchumi wa Taifa.

Mhe. Makamba amesema hayo leo Septemba 26, 2021 wakati akizungumza na Mameneja wa TANESCO wa ngazi ya Kanda, Mikoa, Wilaya na Makao Makuu.

Aidha Mhe. Makamba amewatambulisha Wajumbe wa Bodi ya TANESCO wakiogozwa na Mwenyeki, Bw. Omari Issa, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Maharage Chande, walioteuliwa Septemba 25, 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Wajumbe wa Bodi ya TANESCO waliotambulishwa ni pamoja na Bw. Nehemia Mchechu, Bi. Zawadia Nanyaro, Bw. Lawrence Mafuru, Mhandisi Cosmas Masawe, Balozi Mwanaidi Maajar, Mhandisi Abdallah Hashim, Bw. Abubakar Bakhresa na Bw. Christopher Gachuma.

Mhe. Makamba amesema Bodi iliyochaguliwa ina wajumbe kutoka nyanja mbalimbali na watasaidia Shirika kufikia malengo.

"Tunataka baada ya miaka mitatu Shirika liingie katika orodha ya mashirika bora, yenye thamani na yanayoheshimika Afrika" alisema Mhe. January Makamba

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Bw. Omari Issa, amesema atahakikisha Bodi inafanya kazi na kutimiza malengo yake kwa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa malengo na uwajibikaji.

Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Maharage Chande, ameeleza vipaumbele ambavyo ni masilahi ya rasilimaliwatu, Wateja wa Shirika na utekelezaji wa mipango, hivyo ameomba ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi wa TANESCO.

"Nimhakikishie Mhe. Waziri tutahakikisha tunarudisha heshima ya Shirika na ufanisi kupitia ushirikiano wenu, hakuna Shirika lolote linalotoa huduma ya umeme zaidi yetu sisi, yamkini tuwape wateja wetu huduma wanayostahili", " alisema Bw. Maharage Chande

Meneja Mwandamizi Rasilimaliwatu, Bw. Francis Sangunaa, aliwahakikishia viongozi ushirikiano kwa niaba ya wafanyakazi wa TANESCO.
 
Mwendazake alikosea sana kwenye demokrasia lakini TANESCO aliondoa mikataba isiyoeleweka, akaimarisha Kinyerezi na akaondoa mgao wa ratiba uliokuwepo wakati wa Mkapa na Kikwete na alikuwa anaenda kumaliza nyundo ya mwisho Rufiji, haina haja ya Tanesco mpya itakayorudisha mikataba mibovu.

Mwendazake aliweza kuondoa Service charge ya 7,000 kila mwezi Tanesco ya zamani, Tanesco mpya inahangaika na buku kwenye Luku
 
Mwendazake alikosea sana kwenye demokrasia lakini TANESCO aliondoa mikataba isiyoeleweka, akaimarisha Kinyerezi na akaondoa mgao wa ratiba uliokuwepo wakati wa Mkapa na Kikwete na alikuwa anaenda kumaliza nyundo ya mwisho Rufiji, haina haja ya Tanesco mpya itakayorudisha mikataba mibovu
Tanesco wamekuwa watoto grafla ... Kuzaliwa
 
Unavyoongea hivi nilipo jumapili nzima hatukuwa na umeme.

Jana umeme ulikatika Mara 3

Leo pia ushakatika zaidi ya Mara mpaka Sasa hakuna umeme

Huyu Ni moja ya mawaziri vilaza Sana kuletwa tanesco Kama alivyokuwa Karamagi na Ngereja.
juzi nililalamika kama wewe ila nimeenda sehemu nakuta nguzo chakavu zimelazwa chini kumbe walikata wanafanya mabadiliko, sasa usikute unalalamika huko kumbe ni kitu kama hiki wanafanya..
 
Mwendazake alikosea sana kwenye demokrasia lakini TANESCO aliondoa mikataba isiyoeleweka, akaimarisha Kinyerezi na akaondoa mgao wa ratiba uliokuwepo wakati wa Mkapa na Kikwete na alikuwa anaenda kumaliza nyundo ya mwisho Rufiji, haina haja ya Tanesco mpya itakayorudisha mikataba mibovu
Hatuna shida na tanesco mpya sisi tunataka umeme wa rufiji umalizike ulioachwa na jpm ili bei ishuke
 
Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba amesema ni wakati sasa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kuanza kujiendesha kibiashara, kwa ufanisi ili kuchangia uchumi wa Taifa.

Mhe. Makamba amesema hayo leo Septemba 26, 2021 wakati akizungumza na Mameneja wa TANESCO wa ngazi ya Kanda, Mikoa, Wilaya na Makao Makuu.

Aidha Mhe. Makamba amewatambulisha Wajumbe wa Bodi ya TANESCO wakiogozwa na Mwenyeki, Bw. Omari Issa, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Maharage Chande, walioteuliwa Septemba 25, 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Wajumbe wa Bodi ya TANESCO waliotambulishwa ni pamoja na Bw. Nehemia Mchechu, Bi. Zawadia Nanyaro, Bw. Lawrence Mafuru, Mhandisi Cosmas Masawe, Balozi Mwanaidi Maajar, Mhandisi Abdallah Hashim, Bw. Abubakar Bakhresa na Bw. Christopher Gachuma.

Mhe. Makamba amesema Bodi iliyochaguliwa ina wajumbe kutoka nyanja mbalimbali na watasaidia Shirika kufikia malengo.

"Tunataka baada ya miaka mitatu Shirika liingie katika orodha ya mashirika bora, yenye thamani na yanayoheshimika Afrika" alisema Mhe. January Makamba

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Bw. Omari Issa, amesema atahakikisha Bodi inafanya kazi na kutimiza malengo yake kwa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa malengo na uwajibikaji.

Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Maharage Chande, ameeleza vipaumbele ambavyo ni masilahi ya rasilimaliwatu, Wateja wa Shirika na utekelezaji wa mipango, hivyo ameomba ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi wa TANESCO.

"Nimhakikishie Mhe. Waziri tutahakikisha tunarudisha heshima ya Shirika na ufanisi kupitia ushirikiano wenu, hakuna Shirika lolote linalotoa huduma ya umeme zaidi yetu sisi, yamkini tuwape wateja wetu huduma wanayostahili", " alisema Bw. Maharage Chande

Meneja Mwandamizi Rasilimaliwatu, Bw. Francis Sangunaa, aliwahakikishia viongozi ushirikiano kwa niaba ya wafanyakazi wa TANESCO.

Litajiendeshaje kibiashara wakati mtu anatuma maombi ya kuunganishiwa umeme anasubiri zaidi ya miezi mitatu? Tena hiyo mi3 ndio wameenda haraka otherwise inaweza kuchukua zaidi ya miezi hata 6.

TANESCO nunueni mita za kutosha muwapatie huduma wateja.
 
Majina haya hayapo Tanzania na interest yao:-

1. Juvénal Habyarimana

2. King Kigeli Rwabugiri

3. Dominique Mbonyumutwa

4. Grégoire Kayibanda

5. Gérard Prunier

6. Agathe Habyarimana

7. Augustin Ndindiliyimana

8. Théoneste Bagosora

9. Linda Melvern

10. Emmanuel Mughisa

11. Mbaye Diagne

12. Landwald Ndasingwa

13. Faustin Twagiramungu

14. Marcel Gatsinzi

15. Pascal Musabe

16. Joseph Nzirorera

17. Aloys Ntabakuze

juzi nililalamika kama wewe ila nimeenda sehemu nakuta nguzo chakavu zimelazwa chini kumbe walikata wanafanya mabadiliko, sasa usikute unalalamika huko kumbe ni kitu kama hiki wanafanya..
Haijaanza leo toka mwezi 9 umeme unakatika ovyo Sana kila Jumapili hakuna umeme, hata maeneo ambayo umeme ulikuwa haukatiki ovyo Sasa Ni kukatika tu ovyo ovyo yaani Ni upumbavu mtupu.
 
Unavyoongea hivi nilipo jumapili nzima hatukuwa na umeme.

Jana umeme uoikatika Mara 3

Leo pia ushakatika zaidi ya Mara mpaka Sasa hakuna umeme

Huyu Ni moja ya mawaziri vilaza Sana kuletwa tanesco Kama alivyokuwa Karamagi na Ngereja.
Mkuu samahani sana kukwambia ukweli Ila kiuhalisia huelewekagi unataka nini.. ni kama mwanamke malay.a, alitokea mtu akawa na bidii ya kumaliza tatizo la umeme ukawa unashinda mitandaoni kumwombea mabaya leo hii bila aibu upo unalialia kama mtoto yatima. Nakufananisha na machinga fulani rafiki zangu ambao mwaka Jana walikuwa bize kumshangilia Lissu eti NI YEYE, mara tunataka demokrasia na Uhuru wa kujieleza huku wakikandia vitambulisho vya elfu 20. Juzi wamefulumushwa kariakoo wanaanza kulaani nikawakumbusha ndo demokrasia waliokuwa wanalilia. Kwa kumalizia nakukumbusha, hakuna kiongozi wa nchi atakayeweza kumaliza shida zote za wananchi, angalia mwenye nafuu mpe sapoti.. vinginevyo endelea kulialia mpaka uingie kaburini.
 
Malamiko ya kukatika umeme yamekuwa mengi na hukatika bila taarifa. Na hata kama ilikuwa emergency hakuna maelezo yanayofuata.
TANESCO Waweke wazi tatizo ni nini.
Moro moja hapa.
 
Mkuu samahani sana kukwambia ukweli Ila kiuhalisia huelewekagi unataka nini.. ni kama mwanamke malay.a, alitokea mtu akawa na bidii ya kumaliza tatizo la umeme ukawa unashinda mitandaoni kumwombea mabaya leo hii bila aibu upo unalialia kama mtoto yatima. Nakufananisha na machinga fulani rafiki zangu ambao mwaka Jana walikuwa bize kumshangilia Lissu eti NI YEYE, mara tunataka demokrasia na Uhuru wa kujieleza huku wakikandia vitambulisho vya elfu 20. Juzi wamefulumushwa kariakoo wanaanza kulaani nikawakumbusha ndo demokrasia waliokuwa wanalilia. Kwa kumalizia nakukumbusha, hakuna kiongozi wa nchi atakayeweza kumaliza shida zote za wananchi, angalia mwenye nafuu mpe sapoti.. vinginevyo endelea kulialia mpaka uingie kaburini.
Very well said.
 
Omari Issa aliyesababisha mateso makubwa TTCL ndio mmemuona anafaa!!!
Duh machozi mengi.
Mungu atusaidie
 
Huu ndio uzuri wa Makamba ana leadership qualities ni mtu wa kusikiliza, JF wamempiga madongo naona wametambua umuhimu wa engineers kwenye body ya wakurugenzi.

Pili ana misimamo A means A hakuna compromise kwenye agenda, labda kwenye kubadili njia ya kufikia agenda that is another strong leadership trait (provided the mission is necessary for the nation).

Tatizo lake moja tu sometimes anakuwa too ambitious anawaza kukimbia wakati ata balance ya kutembea bado; hilo tu ndio tatizo lake. Anaweza kuja na plans ambazo si sio size ya third world kabisa.
 
Haijaanza leo toka mwezi 9 umeme unakatika ovyo Sana kila jumapili hakuna umeme, hata maeneo ambayo umeme ulikuwa haukatiki ovyo Sasa Ni kukatika tu ovyo ovyo yaani Ni upumbavu mtupu.
Kuna mfano wa I WISH I HAVE PENISS na msosi wake ni mwepesi kuuchezea!?
 
Back
Top Bottom