Wajue wabunge VIHIYO wa CCM...


NA WEWE UNAANGUKIA HUMO HUMO NINI, MBONA UMEKUJA JUU HIVYO!!!! ACHA LONGO LONGO SHULE MUHIMU BWANA!:smile-big:
 
Kwanini walifeli hicho kidato cha nne? Si ndio ukihiyo wenyewe huo au huo mwaka hakuna wanafunzi waliofaulu, acha kutetea upuuzi, narudia tena, shule ni muhimu hahsa kwa dunia ya sasa hivi, huo kihiyo wao ndio unaowafanya wajisifie kujenga shule nyingi za kata ambazo hazina walimu na kiwango duni cha elimu, wenyewe hawana elimu wataona umuhimu wa elimu kweli?
 

Wanaenda kuwa rubber stamps wa hoja za CCM. We are completely lost.
________________________________________________________________
Tiambize Zumbe mwe inu nyika.
 
Mpendanchi-2, Umechemsha, nadhani hukuwa na takwimu sahii, maana kati ya uliowataja, katika orodha yako, kuna wengine wamepiga shule! Mfano Mh. Mtutura Abdallah Mtutura amesoma na amefanya kazi sehemu za uhakuka, kwatarifa yako huyu Mh. ana Advance Diploma katika mambo ya Usafurishaji ambayo aliipata katika chuo cha Taifa cha Usafirishaji mnamo mwaka 1991/94, na kabla ya hapo alikuwa ni mfanyakazi wa shirika la Umeme Tanzania kwa kipindi kirefu katika karakana yao ilyoko Ubungo(wakati huo) ambapo alikuwa kiongozi katika karakana, na ana FTC ya Ufundi wa Magari kama sikosei. Baada ya kutoka Tanesco aliajiliwa katika Shilika la Umoja wa Mataifa(UN) Tanzania kama Mkuu wa Transport and Logistics, kweli ndugu yangu huyu Mh, amemaliza Form 4 au ndo umeamua kumchakachua? Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpatie! jamaa amepiga shule, jinsi ninavyo mfahamu, si shuleless.
 

ww sikiliza, maana ww unafikiria mwisho ya macho yako yanapoona, nenda NEC, CCM hqtrs na hata magazetini walitoa, na ccm wenyewe walitoa, sasa unapinga nini??? umesema kafanya kazi...? kwani failures si watafanya kazi hivyo hivyo tu, wanapewa directions, na ndio maana mashirika yetu kama haya ya tanesco, kiwanda cha magari (kimekufa) yapo hoi, kwa sbb watu hawana sifa ni vihiyo tu, kufanya kazi si hoja ww, kumbuka hapa tunaongelea kiongozi, kuwa mbunge, si jokes unavyofikiria, sasa failures, vihiyos wakiwapeleka shimoni kesho ww unakuwa wa kwanza kulalamika, acha kufikiri mwisho ya macho yako, au na ww ni kundi hilo no dought
 

Usichukie au na wewe ni miongoni mwa vihiyo walioorodheshwa. Kihiyo ni kihiyo tu. hatuwezi kuongozwa na darasa la saba na form four. Ndiyo maana nchi haiendelei kwa sababu wanaokaa bungeni hawajui hata wanachojadili. darasa la saba na kidato cha nne wanajua nini. kama ni kozi za kujiendeleza sana sana ni komputa tu ambayo nayo ni elimu ya kuwawezesha kufungua tovuti za ngono tu. ukitaka heshima kasoma darasa. usilete ubishi hapa.
 
mwaka huu mpaka uishe tutaona mengi,nashauri ukaguzi wa vyeti usionee dagaa tu,wakati wakubwa wanajilinda na kila siku wanawaandama masikini kwa ukaguzi,uhakiki.

mfano uanze kwa rais kama alivyotoa mfano kwenye uhakiki wa silaha,tena wafanye hadharani.
bunge na wabunge wakaguliwe pia
baadae aingie makamu,waziri mkuu,mawaziri,makatibu wakuu,wakurugenzi,

hii isiishie hapa,vyama vya watu wenye fani mbalimbali kama vyama vya madaktrai,mainjinia,wanasheria......navyo viitishe vyeti au NECTA iitishe vyeti kupitia vyama vilivyowasajili,iingize katika mfumo,

usafi sio serikalini tu,kuna mwingine yuko.sekta binafsi lakini ana feki
 


Ungetaja shule na miaka waliyomaliza masomo yao, kuna wengine hapa tunaambiwa walitoroka shule wakiwa darasa la pili
 
DUUUH huyu atakuwa ni yule wa mtera maana hanaga lugha za kistaarabu.
 
Na yule wa Bangi kuwa zao la biashara ana elimu gani?
 
...[HASHTAG]#TataMadiba[/HASHTAG]...

Ova
 
Hii post is bad!! Aliyeiweka sii muungwana kabisa, sijui alitakaa kuonyesha nini, kwamba??
Hao ma Dr. walioko huko ccm wameifikisha wapi hii nchi???
Elimu rasmi - ya darasani- haiwezi ikawa ndio kigezo pekee cha uongozi bora.

Nakubaliana nawe kuwa hasa kichwa cha habari ni Bad ila content kwangu naona ni sahihi kwa sababu;
1. Kazi ya kwanza ya Bunge ni kutunga sheria, sasa elimu ya darasa la saba ukweli ni kuwa haitoshi kutusaidia kupata hizo sheria nzuri.
2. Wabunge hawa wanatengeneza kamati mbalimbali za Bunge, ambao ndio huwa wanapitia documents mbalimbali na ripoti, kuisimamia serikali na kadhalika. As you know, documents muhimu ziko complicated hata wenye elimu ya juu kupitia mikataba mbalimbali ambayo ni technical ni ishu kubwa. Kumbuka huyu anatuwakilisha sote, walau nadhani ni vyema tuwe na imani kuwa atapitia docs zote kabla ya kukubali au kuzikataa.

Finally nakubaliana nawe pia elimu rasmi sio kigezo pekee cha uongozi bora, lakini ni vyema kuwa nayo kwa sababu kabeba dhamana ya jimbo zima. Akipiga kura ya NDIO kusapoti jambo fulani, walau afanye hivyo akiwa na all facts.
 
Lakini mkuu hao hapo juu wa darasa la saba mbona wanakimbiza kuliko hao wa form 4!!hata majimbo wanaoongoza mbona ni majimbo matata sana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…