Wajinga ndio waliwao!

Pape

JF-Expert Member
Dec 11, 2008
5,488
79
Hivi jamani kila siku magazeti yanatangaza kuhusu hawa watu matapeli ambao wanatumia ujanja wa kuwalaghai watu kwamba wanafanya biashara! Hawa matapeli huja na 'gia' kwamba uwape pesa fulani kidogo halafu wakupe faida! Wabongo bado tu wanakamatika tu! Haya...wabongo acheni tamaa ya kutaka utajiri wa haraka haraka! Mambo sio rahisi kama unavyofikiri! Watu wameshajua kwamba wengi wa wabongo ni 'mazoba' kwahiyo ndio maana kila kukicha wanakuja na mbinu tofautitofauti! We jiulize kweli dunia ya sasa mtu akupe faida wewe tu hivi hivi? Aaah haiingii akilini! Asiyesikia la mkuu huvunjika guu! Amkeni!
 
Tatizo letu tunahusudu "culture ya madili". Kila kitu dili, na hizi dili ndizo zinatuponza
 
Kuna tajiri mmoja lagos anafinance matapeli wanaokuja bongo, na wanawajua watanzania na mapungufu yao.
Akili kumkichwa ukilemaa unaachwa feri
 
bado kila siku watu wanalizwa lkn wengine bado wanaingia kichwa kichwa tu...
 
Back
Top Bottom