Ni zaidi ya miaka 30 sasa serikali wanahangaika kuwaondoa machinga na mamalishe kwa kutumia polisi na mgambo wa jiji na hawajafanikiwa. Kwangu mie sioni mantiki ya kuwatimua mjini kwani hakuna mwenye hakimiliki ya kuishi mjini.
Kinachopaswa kufanyika ni kuwajengea uwezo hawa mamalishe na machinga ili waweze kukuza mitaji na badae kuwa wafanyabiashara wakubwa.
Kwanza, serikali inapaswa kuwaunganisha katika vikundi vya ujasiliamali na wapewe mafunzo na wasajiliwe ili watambulike na idadi yao ijulikane.
Pili, wapewe vitambulisho na wawekewe utaratibu wa kuwa na sare ili wateja wao waweze kuwatambua ili kuweza kuwatofautisha na matapeli vibaka na wahuni wengine.
Tatu, wapewe mashine za EFD na wasajiliwe na TRA ili mwisho wa mwezi waweze kupeleka marejesho na kulipa kodi stahiki sawa na wafanya biashara wengine.
Nne, wawezeshwe kuwa na mitaji kwa kupewa mikopo kwani watakuwa wanatambulika na ni rahisi kuwafatilia kujua maendeleo yao kibiashara.
Tano, machinga wawekewe utaratibu wa kuuza bidhaa zao badala ya kutandika chini kwenye njia za watembea kwa miguu, wenye mtaji mdogo mfano wauza karanga jojo sox na leso watembee na bidhaa zao kwenye beseni na wenye uwezo kiasi kama wauza mpesa wawe na kabati zenye magurudumu na miamvuli au baiskeli za guta kama wauza Ice cream wa Azam.