Wajanja Kazi na bata inaendeleaje?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
WAJANJA KAZI NA BATA INAENDELEAJE!?

Leo 16:30pm 07/04/2022

Washamba tunalia hali ngumu huku mchele,unga na dagaa vyote vimepanda bei, nauli ya bajaji toka sh 500 hadi sh 1,000 vipato vyetu na mishahara ileile havijaongezeka, Wajanja mmeshindwa kuongea na Putin awape mafuta ya bei rahisi, tutakufa mjue, najua Economic recessions huwa hazina mbabe lakini Mjanja mwenzenu Rais wa Ufaransa katoa mabilioni kwa Wananchi wake ili kudhibiti ongezeko la bei ya Umeme na Gesi, Mjanja mwenzenu kaongeza marupurupu kwenye mishahara ya Wananchi wake ili kupambana na mfumuko wa bei, Wajanja mmeshindwa kugundua uko deep Sea kuna meli nyingi zinauza mafuta kutoka Urusi kwa bei rahiisi chini ya bei ya soko la Dunia, au na nyie washamba!!? You cannot mitigate sababu myumbo/mdondoko wa uchumi huja na some unavoidable factors kama vita inayoendelea huko Ukraine ha ha ha...!

Ni wakati sasa wakuangalia yapi ya msingi twende nayo kipindi hiki na yapi tuyasimamishe kidogo,ninyi Wajanja bwana hatuwezi kufa na njaa hivi hivi wakati ninyi mpo, japo sasa hivi jirani akipakua naenda kula hanifukuzi,si unajua sisi Wajamaa ha ha ha jirani ataona aibu kunifukuza, Mzee Baba Magufuli angekuwepo angetoa ruzuku kufidia kwa muda na ninaamini angeongea na Putin kama India na China tukanunua direct toka Russia,Mzee Baba, Chuma,Simba wa Yuda angeongea tu na Masimba wa Yuda wenzie wangetulegezea, Haaa sasa nyie wajanja kabisa halafu mnataka kuzidiwa na Mzee Baba, Chuma, ongeeni na Putin bwana, Kipindi chake ilipanda sukari tu...mijitu ikatoa povu kama imetiwa pilipili...wajanja walificha baada ya Mzee Baba kusema hakuna kuongeza bei sukari,

Mzee Baba kapita, mtenda mema mengi kaenda, sasa hivi kila kitu juu wajanja mnaupiga mwingi hadi mnapitiliza,Mnyika nae anaupiga mwingi,Mwepesi Mzee wa kigoma mwisho wa reli ha ha ha nae anaupiga mwingi yupo mezani anakula sasa hivi,ukiwa unakula hakuna kuongea,ripoti ya 2022 imetoka hatupo uchumi wa kati yeye yupo mezani kanogewa na paja la kuku ha ha ha kaula,wakati wa Mzee Baba,Chuma,Simba wa Yuda tuliongeza mapato ha ha ha wajanja walivyokuja wakasema yalikuwa mapato ya dhuluma,wakaachana nayo majibu wamepata hatupo tena uchumi wa kati,Mzee Baba Chuma alioongeza na kutanua wigo wa ukusanyaji mapato tuendelee nayo tufikirie kupunguza kodi kwenye mafuta ambayo athari yake imekua ni kubwa kwa wananchi na sisi washamba,tuangalie hata yale mapato ya sehemu nyingine tufidie kwenye bei ya lita ya petrol na diesel,

Mwana kulitafuta,mwana kulipata kwa kifipa tunasema "What goes around comes around" ukweli mchungu,wapo waheshimiwa ambao wamekwaa Uwaziri awamu hii ya sita walimshikia bango sana marehemu Mzee Baba,Chuma,Simba wa Yuda wakisema analeta maendeleo ya vitu na si watu,Wajanja mtupe sasa maendeleo ya watu,mlimnanga kwa umahiri ile misemo ya kazi na bata na nyumba inaongozwa/imepewa washamba,Mungu si athumani Wajanja mmepewa nyumba, janga la vita ya ukraine.

Tuone sasa mbinu za kushusha bei za bidhaa za vitu vinavyoleta maendeleo ya watu,Wajanjaa,mnaupiga mwingi,tuone uongozi wenu wa nyumba,Mwenzenu mliye mnanga kipindi kile alitoa uongozi uliotukuka kwa kujitoa sadaka wakati wa corona, aliongea kijijini akajibiwa mjini Marekani na Uingereza,Mzee Baba aliwapa facts za kikemia makemistry, mapublic health, na biostatistics, mastatistics, manumber to harm na manumber to treat akaiachia dunia,wazungu wakakiri hadharani corona tutaishi nayo kama maradhi mengine. Mzee Baba, Simba wa Yuda aliliona hili miaka miwili kabla ya hawa Wazungu kukiri hadharani juzi kati.

Nimalizie na ma cost of purchase ya mabidhaa yaliyoongezeka,ma cost of transportation yaliyoongezeka, madaladala, pikipiki, bajaji kuongeza bei, mamwendokasi najua yataongeza bei, ma kodi ya nyumba, gharama ya pango, umeme, maji, Ulinzi, usafi, misosi imeongezeka bei, mshahara mdogo tutashindwa kulipa vyote hivi, chipsi kavu toka 1,500 hadi 2,000 wali maharage toka 1,000 hadi 2,500 Niseme tu. There is a difference between problem addressing and solving leader/government naamini mtatuokoa sisi Wananchi toka kwenye huu mfumuko wa bei, naahidi kuwa nanyi bega kwa bega, Mimi mshamba lakini sijui kama mtanikubali nikae meza moja na ninyi, Mama yetu Tanzania hatuna pa kwenda, niwatakie heri na Baraka, na Mwenyezi Mungu awashushie maono muweze kutafuta namna ya kutupunguzia bei vitu hivi vinavyoendelea kupanda, Amina.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Neno murua ila sijui kama watasikia.

Maka...ba umesikia mpigaji wangu?
 
Hili ZOEZI ni muhimu lakini UKWELI ni kwamba SERIKALI imepoteza USHAWISHI huku MITAANI ndani ya mwaka mmoja jinsi inavyoshughulikia MATATIZO , Tatizo kubwa la kwanza kusababisha MIFUMKO YA BEI lilikuwa ni TATIZO LA UMEME USIOELEWEKA NCHI NZIMA hivyo kusababisha ONGEZEKO KUBWA LA GHARAMA KUBWA za SHUGHULI za kibiashara na KIUCHUMI pamoja na Uzalishaji MALI sehemu mbalimbali ikiwemo Viwandani.
Hivyo kwa hapa Tanzania bara MIFUMKO ya bei ina mwaka ikiwemo vifaa vya Ujenzi vyakula nk nk
Hivyo kwa mwaka mmoja sasa WATANZANIA bara hawajaona KAULI wala JUHUDI za MAKUSUDI za SERIKALI kushughulikia MIFUMKO ya bei na vyanzo vyake ikiwemo MAKATIZO YA UMEME USIOELEWEKA YANAYOENDELEA NCHI NZIMA.
SERIKALI zote dunia ikiwemo SERIKALI ya Zanzibar wamechukua hatua Kudhibiti MIFUMKO ya BEI
Lakini huku Tanzania bara maelekezo ya kiongozi mkuu ni kama kuhalalisha MIFUMKO ya bei kwa kuelezea sababu zake
Tatizo letu wanaCCM yeyote anayetoa feedbacks kutokana na hali halisi mitaani anaonekana haipendi SERIKALI ya awamu ya SITA
Ila anayeisifia asubuhi mchana jioni na usiku bila kutoa maoni mapendekezo ushauri wala feedback anaonekana ndio shujaa.
 
Kuna MASHINDANO ya MIFUMKO ya bei ya mafuta hapa Afrika Mashariki ??
SERIKALI za Kenya Zanzibar Uganda Rwanda zote zimechukua hatua za Kudhibiti
Ya Tanzania bara imechukua hatua ya kuhalalisha MIFUMKO ya bei
Kumbuka MIFUMKO ya bei Tanzania bara umekuwa mkubwa sana sababu ya kwanza na ya msingi ni MAKATIZO ya umeme usioeleweka NCHI nzima.
SERIKALI ya upande wa Tanzania bara haijachukua hatua yeyote hadi kesho
Tatizo kubwa la kwanza kusababisha MIFUMKO YA BEI lilikuwa ni TATIZO LA UMEME USIOELEWEKA NCHI NZIMA hivyo kusababisha ONGEZEKO KUBWA LA GHARAMA KUBWA za SHUGHULI za kibiashara na KIUCHUMI pamoja na Uzalishaji MALI sehemu mbalimbali ikiwemo Viwandani.
Hivyo kwa hapa Tanzania bara MIFUMKO ya bei ina mwaka ikiwemo vifaa vya Ujenzi vyakula nk nk
Hivyo kwa mwaka mmoja sasa WATANZANIA bara hawajaona KAULI wala JUHUDI za MAKUSUDI za SERIKALI kushughulikia MIFUMKO ya bei na vyanzo vyake ikiwemo MAKATIZO YA UMEME USIOELEWEKA YANAYOENDELEA NCHI NZIMA.
SERIKALI zote dunia ikiwemo SERIKALI ya Zanzibar wamechukua hatua Kudhibiti MIFUMKO ya BEI
Lakini huku Tanzania bara maelekezo ya kiongozi mkuu ni kama kuhalalisha MIFUMKO ya bei kwa kuelezea sababu zake
Tatizo letu wanaCCM yeyote anayetoa feedbacks kutokana na hali halisi mitaani anaonekana haipendi SERIKALI ya awamu ya SITA
Ila anayeisifia asubuhi mchana jioni na usiku bila kutoa maoni mapendekezo ushauri wala feedback anaonekana ndio shujaa.
 
KUPWAYA KWA UPINZANI


Kinachoelekea ni kwamba UCHAGUZI ujao unaelekea utakuwa wa kuachiana MAJIMBO kutokana sio Berlin bali kinachoelekea kuwa Dodoma Conference
Kinachoelekea UCHAGUZI ujao kuna baadhi ya wabunge wasio na NGUZO za uhakika majimbo yao yatatolewa sadaka ili vyama vile navyo vipate wabunge vipate RUZUKU vipunguze kelele kama ilivyo upande wa kule visiwani.
Tunaelekea kwenye siasa za mezani zaidi badala ya siasa za majukwaani.
Hivyo mambo mengi yatafanyika mezani tu kikubwa wapinzani wanahitaji tu RUZUKU yao yaende hivyo kelele zote hasa watu wa kamati kuu zao wanahitaji kurudi bungeni tu ndio hitaji lao kubwa tu.
Wakilala wakiamka ni UBUNGE tu na yule mwingine anawaza Kiongozi wa kambi rasmi ya UPINZANI bungeni tu pamoja na remuneration zake
 
Hakuna kitu kilichopanda bei, tafuta pesa tu.
Tunataka CCM itakayozungumzia matatizo na shida za WAPIGA KURA wetu
MAKATIZO ya umeme
MIFUMKO ya bei ya bidhaa mbalimbali
Hatua CCM ya Mzee Kinana itakazochukua kuisimamia SERIKALI ili gharama kubwa za maisha kwa Mwananchi wa kawaida huku mitaani zipungue katika wakati huu mgumu wa global Economy slowdown.
Kwa ufupi CCM INATAKIWA KUENDELEA KUWA NI SAUTI YA WANANCHI WOTE
 
Back
Top Bottom