Waitara ampandia Rais Magufuli

Ha ha mfalme badala ya kujenga viwanda anawakamata wote wanaomwambia kakosea. Aisee najutia kura yangu kwa huyu msukuma sikujua kwa kweli.
 
Rais anawagwaya UKAWA, lakini kwa sababu ya rais huyo huyo UKAWA wameanza kuwagwaya Wananchi , 2020 Magufuli hapigi kampeni.
Kwani vipi? Umeona kuna dalili za kujiuzulu kabla ya muda kwa kuona mambo yanamshinda?
 
Kama kunakitu wanataka kutueleza watumie vyombo vya habari na wabandike matangazo!
 
Witara size yake mi Jerry Slaa, kwa magufuli ni mwendelezo ule ile wa kutaka umaarufu pasipo kuwa maarufu.
Ajaribu kwenye jimbo lake kwanza tuone kama atapata watu wa kumsikiliza, yeye alikutana na upepo wa mabadiliko, asije akajidangannya kuwa ana nguvu za kisiasa Ukonga
 
Tangu wanadamu waishi pamoja kumekuwa na mpishano ambao haukomi. Yaani wewe unaenda mm ninarudi., unalala mimi naamuka. unamaliza mimi naanza. kwa hiyo dunia ni mpishano na hivo hakuna utawala utaodumu milele na kwa kuwa vyama ni vingi kuna siku kutakuwa na mpishano tu! kutokubali ukweli huu ni fujo lakini mpishano uko pale pale.
Kwa sababu hiyo hakuna haja ya hii reaction bali tujiandae kupishana kwa amani!
 
mtakubaliana na yale tuliosema sisi kina gogo la shamba kwamba kama ccm wanaona ni vyema kufanya siasa 2020 wao wakae wasubiri lakini wanaoona waendelee na siasa kuanzia sasa waachwe wafanye maana wote katiba inawaruhusu
 
Hii hata kama ni kweli ni mhimu kuzingatia nidhamu ya namna ya kuiwasilisha kwa mkuu wa kaya.
Enzi za Mtemi(Onyama) kule kwetu kulikuwa na utaratibu ambao ulikuwa hauruhusu mtu ambaye si msaidizi wa Mtemi (Ng'wanangwa) kumkosoa au hata kumjibu moja kwa moja Mtemi bila kupitia kwa msaidizi wake.
Kwa mfano hata kama mtakuwa kwenye msongamano ikatokea Mtemi akakukanyaga kwenye unyayo na akawa hajaondoa mguu wake,hata kama anakuumiza namna gani ni lazing umwambie Msaidizi wa Mtemi kuwa amwambie Mtemi kuwa amekukanyaga ili aondoe mguu wake.(Ng'wanangwa, ng'wilage u onyama onipandaga )
Tofauti ya hapo ukimweleza Mtemi moja kwa moja,japo ni kweli,basi utakiona cha mtemakuni.
Nadhani ndo tunatakiwa kuiga nidhamu hii ya kwetu.
 
Hakuna ukweli wowote nilioambiwa hapo, ukweli tutaujua 2019 na 2020.Waitara akirudi mnikate kidole mimi mkurya mwenzake lakini dalili za kumng'oa zimeshaonekana.

Vipi mmeshaitia hofu tume ya uchaguzi na saa hizi mko mahali mnapanga matokeo yawe vipi ama?
 
Mkuu Masters na uDr wa mawaziri wa CCM zinaandikwa na watumishi wa serikali pamoja na mimi nimeandika za mawaziri na wakurugenzi si chini ya watano.

Vyuo vinavyowatunuku si wa kweli kwa sababu kama walikuwa kazini walipata wapi muda wa kuhangaikia hizo shahada zao. Nakumbusha Masters za wateuliwa wa Jamaa yake Lisu wengi wao walikuwa watumishi wa CCM jiulize huko CCM kuna vyuo vikuu vinatunuku shahada. Kama kawaida wanatunukiwa tu bila kuwa na merit zo zote ndiyo elimu yetu hiyo.

Naamini Jamaa yake Lissu ni mmoja waliotunukiwa shahada zao wakiwa mezani kwa kulingana na ujinga unaoonyeshwa (Hata kujua katiba ni issue).
 
Kama umeamua kuandika alichokisema Waitara leo mbona hujasema kuhusu kusifia baadhi ya mambo mazuri ya uongozi wa Rais Magufuli?
 
Naona imekuwa wakati muafaka kwa kila kila mbunge wa chadema kupata kick kwa kutumia jina la magufuli.

Hili neno "kiki" au "kick" naona sasa linazidi kutumika hata out of context!!

Sasa sina hakika utazungumziaje mambo ya nchi hii ya Tanzania ambayo mimi naifananisha na mwili wa binadamu bila kukigusa kichwa (Rais) ambaye kwa sasa ni Magufuli??

Kila media iwe gazeti, TV au Radio na mitandao karibu yote ya kijamii hutaweza kukosa post/habari ambayo inamzungumzia Magufuli John Pombe iwe kwa ubaya au kwa uzuri; kumsifu au kumponda!!

Unafikiri ni kwanini asiwe Jakaya Kikwete tena kama ilivyokuwa hapo kabla ya miezi kumi iliyopita??......hebu nipe jibu Rodney

Au kauli ya "anatafuta 'kiki' huyu kwa......" kwenu nyie mnakuwa mnamaanisha nini hasa??
 
Naona imekuwa wakati muafaka kwa kila kila mbunge wa chadema kupata kick kwa kutumia jina la magufuli.

mim nimefura tu wanavyotisha eti 1.9.2016 ukuta uko pale pale , wao wawe wakwanza kulianzisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…