NAFIKIRE
JF-Expert Member
- Sep 5, 2014
- 681
- 466
Wadau:
Nianze bandiko langu hili kwa kusema kwamba mimi sio mbaguzi wa rangi, kabila,dini au ukanda.Ninauchukia ubaguzi na ninamchukia mtu mbaguzi.Mimi ni Mtanzania mzalendo ninaipenda nchi yangu na serikali yake.
Ila ninawiwa kutoa ushauri wangu wa kiroho ambao wengi mnaweza kuutafsiri kama wa kibaguzi lakini sio na unaukweli mkubwa ndani yake.
Ushauri wangu kwa mkuu wa kaya yetu
Ninakushauri mkuu kama unataka kufanikiwa sana kiuchumi na kisiasa uwashirikishe katika serikali yako kuanzia ngazi ya uwaziri na nyanja mbalimbali za uongozi na ushauri katika serikali yako watu kutoka miteremko ya mlima Kilimanjaro
Hawa ni watu wanaofanya kazi kwa bidii na wanajua maendeleo na uchumi ni nini..
Ukifanya utafiti wa haraka kuanzia ngazi ya familia na sehemu mbalimbali ambapo hawa watu wamepewa nafasi ya kuongoza utaona zimefanikiwa sana na utapata mantinki ya ushauri huu.
Nathubutu kusema hawa ni watu waliobarikiwa sana kama Wana wa Israeli kutoka mashariki ya mbali ndio maana ninawaita 'Waisraeli wa Tanzania
Huu ni ushauri wa kiroho zaidi na pale utakapoona vema kuufanyia kazi ushauri huu basi utaona uongozi wako utakavyoshamiri na kufanikiwa sana.
Wasalaam
Wako katika Ujenzi wa Taifa.