Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,011
- 9,879
Katibu wa Baraza la Maulamaa, Sheikh Hassan Chizenga ametaka waumini wa dini ya Kiislamu nchini Tanzania kufunga kwa siku tatu kuanzia Machi 8 ili kumuomba Mungu aepushe janga la CoronaVirus.
Pamoja na Mfungo Baraza Kuu la Waislamu Tanzania limeona haja ya kurejesha dua za Kunuti katika swala zote tano hadi COVID-19 itakapotokomea.
Serikali ilisema Tanzania inachukua tahadhari dhidi ya COVID19 ambazo ni kujifukiza na kumtegemea Mungu.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mufti wa Tanzania, Katibu Mkuu wa Baraza la ulamaa na Msemaji wa Mufti wa Tanzania Sheikh Hassan Said Chizenga ametoa agizo hilo kwa misikiti yote nchini kurejesha tena dua ya kunuti katika swala zote tano pamoja na kuchukua tahadhari zote zinazotolewa na Wizara ya afya kwa ajili ya kujingika na maambukizi ya ugonjwa wa Corona
"Baada ya kuonekana kwamba baadhi ya mashambulizi tuliyoyapata mwaka jana kana kwamba yanataka yatokee tena basi kilichokuwa sahihi ni kuzungumza na Mungu nakutumia utaalamu wa kisayansi unaotakiwa na Mungu tumweke mbele tukifanya hivyo tutafanikiwa" amesema Sheikh Hassan
Aidha watanzania wameshauriwa kutokutetereshwa kiimani na mtu yeyeote kuhusiana na silaha waliyoitumia na kuwapatia ushindi mwaka jana ambayo ili leta utofauti kati ya Tanzania na nchi nyingine badala yake wazidi kumtegemea mwenyezi Mungu.
"Tusiyumbishwe kwa namna yeyote kuiacha silaha yetu iliyotupa ushindi mwaka jana kwa kushawishiwa kutumia silaha iliyothibitishwa kuwa aina uwezo wa kupambana na korona," amesema amesema Sheikh Hassan
Sheikh Hassan Said Chizenga ametoa maagizo na tamko la Baraza la ulamaa BAKWATA kwa watanzania hii leo kwa niaba ya Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir Ally aliyeshindwa kuhudhuria katika mkutano huo kutokanana sababu za kibinadamu.
Chanzo: EATV