Waislamu waapa kuendelea na maandamano kesho kutwa licha ya mafuriko

Status
Not open for further replies.
Kwa hali iliyopo sasa hivi maandamano hayo yaahirishwe..haitakuwa vizuri hata kidogo na wala hayataweza kushuhudiwa na wananchi wengi...Tuzike kwanza ndugu zetu kisha mengineyo yatafuata...

Acha wafu wazike wafu wenzao kwanza mkuu!
 
Humu JF CHADEMA kuandamana halali ila Waislam kuandamana kwa maslahi yetu ni haramu eeeh? Hii inanipa rangi halisi ya JF na CHADEMA!

ndugu yangu wewe bana. Kwa kupenda kuchanganya habari....

CDM ni chama cha siasa, Waislamu ni 'waumini wa dini ya islam.
 
jamani waislam hamna wasomi hata wakuwasaidia??? hebu acheni hizo bana mnakuwa kama mbayuwayu! vipi nyie mnaboa ala!1

Jamani hawa ni ndugu zetu bana, wana wa Ibrahim (Abraham), Isaack & Yakobo(Yakub), chonde chonde jamani.
 
kwani tunatibiwa bure? Na hiyo pesa tunayotoa kupata huduma huwa inarudi serikalini?

Serikali Ina hospitali wilaya? Kama sio za mashirika ya dini kuombwa kuwa DDH, Designated District Hospital. Huenda na wewe ulizaliwa katika hizo hospitali. Jengeni zenu na nyie muombe MOU ni serikali kama alivyosema Sheikh Mkuu wa Dar es salaam au hukumsikia? Au utasema yule ni Padre au Mchungaji aliyezungumza jana TBC News time?
 
Mtu akiwa na hamu ya virungu utamuona tu. Wanatania hawa, hakuna mwanaume wa kuandamana kisa ana hamu ya kufungwa PoP kwa fedha ya MoU.

FFU wanabonda jamani acheni, mweh!
 
Hawaandaman kwa kutaka sifa.unaongelea imani sio siasa kwa hyo virungu sio ishu.iache dunia ijue mbali na mafuriko wapo watu wanaonyesha hisia zao through maandamano.
 
Humu JF CHADEMA kuandamana halali ila Waislam kuandamana kwa maslahi yetu ni haramu eeeh? Hii inanipa rangi halisi ya JF na CHADEMA!
Hakuna mtu anakataza waislam kuandamana ila kipindi mnachotaka kuandamana taifa lipo katika hali tete ya mafuriko kwanini msisubiri hali itakavyokuwa?

Halafu watu wakifa kwenye mafuriko huko kwenye maandamano mtapitisha bakuli la kuomba msaada na kulaumu serikali
 
Hawaandaman kwa kutaka sifa.unaongelea imani sio siasa kwa hyo virungu sio ishu.iache dunia ijue mbali na mafuriko wapo watu wanaonyesha hisia zao through maandamano.

Hivi kwa akili yako unadhani Waislam wenye akili zao na shughuli za kufanya wataandamana? Hawa ni wahuni tu wanaokosaga kazi za kufanya. Kiongozi wa BAKWATA katoa nasaha zake kwa Waislamu kuhusu hayo maandamano na kawaeleza wazi kuwa hayana mashiko. Kilichopo kwa waislamu ni kushiriki kuijenga Tanzania badala ya kuandamana kupinga ambao wanajitoa kufanya hivyo.
 
Unajua this is so unfair - kwanini watu wanapozungumzia "Waislamu" wanazungumza kana kwamba Waislamu ni kundi moja lisilo na tofauti zozote na lenye kukubaliana kwa kila kitu? Hivi, mtu akisema "Wakristu ni wauaji wa halaiki" tutasema anamaanisha "wakristu wote"? Au hata kusema "Waafrika ni watu wa x au z" ina maana sote Waafrika tuko hivyo? Kwa mfano, mtu akitaka kuzungumzia utapeli wa Wanigeria ina maana ndio Watanzania pia kisa wote ni Waafrika?


Tujifunze kuweka maneno sawasawa - maandamano haya hayakuandaliwa na taasisi zote za Waislamu na kule kupingwa tu na baadhi ya Waislamu kunafanya maandamano hayo kukosa uhalali wa kuitwa "Maandamano ya Waislamu". Maandamano ya Chadema haywezi kuitwa maandamano ya "Upinzani" wakati Wapinzani wengine wanayapinga!
 
sasa wataandamana baada ya mvua au watapiga kavukavu hivyohivyo??
 
nafikiri kama kuna kikundi cha waislam, hata kama ni waislam wote......japo in this case sio wote, wanataka kuandamana kutoa dukuduku lao ambalo wameona halisikilizwi katika utaratibu wa kawaida, basi na wafanye hivyo, ni haki yao. Kama raia, kama haki wanayodai ni halali, why not bana.
Waingie barabarani, swala la kuwatisha kwamba watapigwa virungu, hilo tuliache, kwani wakipewa kibali virungu vitatoka wapi?

Go guys go.......nendeni mkadai 'haki' yenu.
 
Hivi kwa akili yako unadhani Waislam wenye akili zao na shughuli za kufanya wataandamana? Hawa ni wahuni tu wanaokosaga kazi za kufanya. Kiongozi wa BAKWATA katoa nasaha zake kwa Waislamu kuhusu hayo maandamano na kawaeleza wazi kuwa hayana mashiko. Kilichopo kwa waislamu ni kushiriki kuijenga Tanzania badala ya kuandamana kupinga ambao wanajitoa kufanya hivyo.

Bakwata imeshindwa kusimamia mambo ya waislam kama sio unafki wa Bakwata na serikali hili suala la kadhi lingekuwa limeisha na kama sio ukiazi wa Bakwata shule, hospitali na taasisi zingine za kiislam nazo zingetakiwa ziwe included ktk MoU kwan hizo ni kodi zetu wote regardless ya dini zetu. Lingine mi naona huyu sheikh wa mkoa Dar kama sio mbumbumbu njaa inamsumbua yeye kaongea ka nani ndani ya Bakwata? Kwani Bakwata haina katibu, msemaji au uongozi wa juu? Yeye wanaomhusu ni waislamu wa Dar tu! Sio waislamu wa nchi nzima
 
Hawa jamaa sometimes huwa nawashangaa, huwa hawajali masuala ya jamii nyingine inayowazunguka zaidi ya yale yanayowagusa wao, huwezi wakuta wanazungumzia au kuandamana kuhoji serikali kutotoa huduma muhimu kwa wote, this is simply selfishness.

waislamu tunaonewa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom