Waislamu wa Kenya Walaani Upotoshaji wa Serikali Kuhusu Siku Sahihi ya Eid

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
44,034
50,769
Baadhi ya Waislamu nchini Kenya wameishutumu serikali ya Kenya kwa kuwapotosha watu baada ya kutangaza kuwa Ijumaa ni siku ya mapumziko kwa ajili ya Eid al-Fitr.

Waziri wa mambo ya ndani nchini Kenya Kithure Kindiki alitangaza Jumatano kwamba Ijumaa ni siku ya mapumziko kwa ajili ya Eid.

Mwenyekiti wa Baraza kuu la Waislamu nchini Kenya (Supkem) Hassan Ole Naado, ambaye alizungumza na gazeti la Nation, alisema kuwa tangazo la serikali linawakanganya Waislamu nchini humo, kwani uamuzi wa siku ya Eid hutegemea muonekano wa mwezi.

Bw. Naado alisema kuwa: "Serikali inafaa kuomba ushauri Waislamu kabla ya kufanya uamuzi. Hili ni kosa kubwa na upotoshaji,” alisema.

Baadhi ya Waislamu nchini humo wameandika kwenye mitandao ya kijamii kulaani hatua ya serikali.

Eid al-Fitr ni sikukuu muhimu kwa Waislamu, ya kuadhimisha mwisho wa mwezi wa Ramadhani, ukiwa ni mwezi wa tisa katika historia ya Kiislamu.

Mara kwa mara Waislamu wamekuwa wakitofautiana kuhusu siku ya mwisho wa mwezi wa Ramadhani, baadhi wakiuona mwezi kabla ya wengine.

Chanzo: BBC
 
Tatizo liko kwa waislam wenyewe, kwa nini wasiweke fixed date ya kufungua wanapoanza kufunga? Mara mwezi umeandama Singida, mara umeandama uarabuni, mara wapi, ni vurugu tupu! Wanailaumu serikali bure. Kenya nayo iige tanzania, mambo ya kutangaza muandamo wa mwezi iwaachie waislam wenyewe wajitangazie. Anyway, kwa kuwa siasa inatawala dini acha serikali iipangie dini mambo yao
 
Waislam wa Nchi jirani ambayo ilisheherekea Sikukuu ya Eid el fitr siku ya Ijumaa wamelalamikia kitendo cha Serikal kutangaza mwandamo wa mwezi

Waislam hao wamesema jukumu la kutangaza Muandamo wa Mwezi ni la Waislam wenyewe
 
Baadhi ya Waislamu nchini Kenya wameishutumu serikali ya Kenya kwa kuwapotosha watu baada ya kutangaza kuwa Ijumaa ni siku ya mapumziko kwa ajili ya Eid al-Fitr.

Waziri wa mambo ya ndani nchini Kenya Kithure Kindiki alitangaza Jumatano kwamba Ijumaa ni siku ya mapumziko kwa ajili ya Eid.

Mwenyekiti wa Baraza kuu la Waislamu nchini Kenya (Supkem) Hassan Ole Naado, ambaye alizungumza na gazeti la Nation, alisema kuwa tangazo la serikali linawakanganya Waislamu nchini humo, kwani uamuzi wa siku ya Eid hutegemea muonekano wa mwezi.

Bw. Naado alisema kuwa: "Serikali inafaa kuomba ushauri Waislamu kabla ya kufanya uamuzi. Hili ni kosa kubwa na upotoshaji,” alisema.

Baadhi ya Waislamu nchini humo wameandika kwenye mitandao ya kijamii kulaani hatua ya serikali.

Eid al-Fitr ni sikukuu muhimu kwa Waislamu, ya kuadhimisha mwisho wa mwezi wa Ramadhani, ukiwa ni mwezi wa tisa katika historia ya Kiislamu.

Mara kwa mara Waislamu wamekuwa wakitofautiana kuhusu siku ya mwisho wa mwezi wa Ramadhani, baadhi wakiuona mwezi kabla ya wengine.

Chanzo: BBC
Iyo serikali binafsi naiunga mkono, iweje Saudia wao wale Eid ijumaa na ilihali mlianza nao kifunga sawa sawa alafu eti ile siku ya mwisho useme mwezi haujaonekana ? Ndio maana iyo serikali ikatazama tu Saudia ika.aamua mechi
 
Back
Top Bottom