Msamiati
R I P
- Mar 6, 2011
- 1,063
- 697
Habari za wakati huu wapendwa,
Baada ya kusoma nyuzi mbalimbali kwenye majukwaa ya habari na hoja pamoja na Jukwaa la Dini, nimegundua ushetani mkubwa wa jitihada za kuhamasisha matabaka ya kidini na tofauti katika jamii zetu.
Nimegundua maneno ya kujenga chuki na usambazaji wa taarifa za kujenga hisia kali za kidini na mpasuko wa kijamii baina ya wakristo na waislamu kwenye Jamii yetu. Maneno ya kejeli, matusi mazito na maudhi yamekuwa kama lugha ya kawaida kwenye mijadala ya dini, tena sasa hivi imekuwa kama sample ya kutafutia umaarufu hapa JF.
Kwanza ningependa kuuliza kwa uchungu kabisa, je! tunapanda hii mbegu kwa faida ya nani ? hizi chuki za kuchukiana wenyewe kwa wenyewe tunazo pandikiza, tumeshawahi kukaa na kutafakari siku zikiota mizizi utakuwa mzigo wa nani ? Tumekaa na kutafakari faida ya hizi chuki za kidini ?
Naomba kuuliza ! Hivi ni kweli social interaction tuliyokuwa nayo baina ya waislamu na wakristo, hivi sasa haitufai tena na tunaitaji kuishi kwenye matabaka ya kidini na chuki kwa madai ya kutafuta pepo !? Ni sawa sasa kujenga mtazamo wa uadui baina ya waislamu na wakristo !? Tuwe na maduka ya waislamu na wakristo, tuwe na mitaa ya waislamu na wakristo, Je! tunataka iwe hivyo ?
Hivi ni kweli tumekuwa wapumbavu kiasi cha kushindwa kujua kuwa Mataifa mengi ya nje yanafanya dini as a part of social activities, vita na mauaji yanayoendelea sio tu kwa ajili ya masilahi ya kuingia peponi, bali kuna masilahi ya ki-utawala, masilahi ya kiuchumi, masilahi ya ki-taifa dini zinatumika tu.
Ndugu zangu, katika nchi zote duniani, Tanzania ni nchi pekee inayofata dini katika misingi ya haki, ndio maana kuna amani na utulivu huu tulio nao. Mungu wa kweli anatajwa hapa kupitia uislamu na ukristo ndio maana maombi ya Mshekhe na Mapadri kuiombea amani nchi yetu yamekuwa na mafanikio miaka yote.
Nigeria kuna Mashekhe na Mapadri kama hapa kwetu, wanaomba amani na wanaitaka kama ilivyo hapa kwetu lakini Mungu wetu mpenda haki na amani kutowajibu maana yake ni kwamba hawasimamii haki bali masilahi ya Kiuchumi, kiutawala na kijamii kama nilivyoeleza awali.
Hoja yangu kwenye paragraph mbili zilizotangulia, ni kwanini tuipe nafasi mienendo ya dini kwenye mataifa mengine iingilie utaratibu mzuri na mtizamo mzuri tulio nao kwenye imani zetu. Kwanini tuhukumiane, tuchukiane, tunyosheane vidole tutukanane kwasababu tu ya matukio yanayofanya Naigeria, Somalia, Kenya, Amerika, Uingereza na maeneo mengine duniani kwa kigezo cha dini ?
Tunaimani safi mbele za Mungu, Tuna ukristo safi na Uislamu safi. Miongozo ya imani zetu ni Biblia na Quran sio Wamarekani wala ISIS. Miongozo yetu haisapoti Ushoga wala Ugaidi, tunapoletewa hayo mambo yakiwa na sura za kidini tutambue kuwa ni hila za shetani, tuamke na kung'amua kuwa hawafanyi hayo kwa manufaa ya imani zetu, Tuamke.
Nimekereketwa na mengi sana kwenye swala hili lakini, naomba nimalizie kwa kuwasihi Ma Great Thinker katika hili, JF ina-impact kubwa sana kwenye Jamii, Taifa letu linaweza kuharibika kabisa na kuingia kwenye machafuko makubwa ya kidini na chanzo kukawa mimi na wewe kutoka JF.
Kwa mada hii, Simaanishi kuwa ni vibaya kufanya midahalo inayohusiana na tofauti za imani zetu, sio vibaya kujadili uungu wa Yesu, wala sioni vibaya kujadili uislamu wa kina kaini na Habili, mijadala hii ilikuwepo mika na miaka tena tumeifanya kwa mihadhara na kuheshimiana.
Nashauri tuzingatie zaidi mambo yanayotuunganisha kuliko yale yanayotutenganisha, Tofauti kwamba mtume wa wakristo ni Yesu na mtume wa waislamu ni Mohammad S.A.W sio kitu cha kufungamana nacho sana kuliko ukweli kuwa Wote tunamwita Mungu mmoja, wote tunaamini mitume mbali mbali iliyoshushwa na Mungu.
Naomba kwa moyo mkunjufu niwaalike wote kwenye mjadalaShukran.