Waislamu na Wakristo tutumie dini zetu kudumisha amani na umoja wa kitataifa

Asante mkuu Msamiati kwa kuleta hapa mawazo mazuri yenye lengo la kudumisha amani & umoja wa kitaifa.
Ni kweli kuwa chuki za kidini hazileti faida yoyote miongoni mwetu.
Binafsi ninaamini kuwa ikiwa tungeweza ku-apply '[size=+2]The Golden Rule'[/size] ipasavyo, ni wazi kuwa tusingeweza: kuhukumiana, kuchukiana wala kunyoosheana vidole.
Tatizo baadhi ya Misahafu yetu haina hii kitu [size=+2]'The Golden Rule'[/size]! Kama ipo basi ni kwa wale 'wenzetu, kaka zetu, dada zetu ktk imani'
Baadhi ya watu, wamefundishwa kuwa mtu yoyote aliye tofauti na imani yake, mtu huyo ni adui; si rafiki kamwe! Tutumie akili zetu kutafakari yale yote tunayofundishwa kule Makanisani na Misikitini.
Kabla ya kuletwa hizi dini kuu mbili (Ukristo & Uislam) mababu zetu mbona waliishi kwa amani?
Heko ndugu zangu hakuna haja ya kugombana kwa ajili ya tofauti zetu za kidini.
 
Last edited by a moderator:
Kwa uzoefu ni kwamba mijadala baina ya dini zenye imani tofauti huishia kuvunja amani maana haiwezekani kufikia consesus. Therefore ni meaningless kuwa na mijadala ya aina hiyo. Lakini zaidi sana mijadala ya kidini kati ya ukristo na uislamu haiwezi kuisha vzr maana ukweli wenzetu waislamu si watu wa amani kabisa. Huo ndio ukweli!

Mkuu umekosea sana kuhukumu binadamu wenzetu Waislamu!
Mbona tunao marafiki zetu, ndugu zetu, majirani zetu na wafanyakazi wenzetu ambao tunaishi nao vizuri tu! Acha ubaguzi wa kidini ndugu.
 
Sasa dunia inakabiliana tishio la usalama linalosababishwa na uislamu wa msimamo mkali. Huu ni tishio kwa watu wote bila ya kujali dini zao, hata kwa waislamu wenyewe. Somalia, Nigeria, Misri, Syria, Indonesia, Kenya hadi Pakistani ni mifano michache ya wahanga wa mfumo huu wa uislamu wa msimamo mkali.

Ngaa kipo kisingizio cha kueneza dini lakini kumekuwa na athali hata miongoni mwa jamii za kiislamu kama ilvyotokea majuzi kule Pakistani wakati waumini wa msimamo mkali walipowateketeza watoto wa shule zaidi ya 130. Kwa bahati mbaya, jamii ya waislamu imekuwa kimya kukemea na kuchukua hatua dhidi ya unyama huu uliovikwa vazi la kidini ili kutupumbaza na kutugawa.

Sasa ni wakati muafaka jamii yetu ya waislamu kuamka na kuungana na jamii zingine dhidi ya hawa wajifanyao ndugu za waislamu na wenye kuwatetea kumbe sio na ni wenye kuwateketeza hata waislamu wenzao. Muda ni huu, tuchukue hatua kabla hatujajutia maamuzi yetu.
 
Ni mawazo mazur kama yatachukuliwa bila ushabiki wa dini, katika kumcha mwenyezi mungu hakuna cha msimamo mkali katika kuwaangamiza wanaadamu wenzako kamwe!
 
Hayo ni makundi ya mercenaries yanayojificha kwa kutumia miavuli ya kidini ktk kutekeleza mambo yao pale washirika wao wanapokwenda kinyume na makubaliano ndio mauaji hutokea na kusingizia dini. Uislamu wetu haufundishi uovu wa namna hiyo.

Wakati wa mtume (SAW) hakukuwa na ugaidi. Haya mambo yameshamiri kuanzia miaka ya 1990s na yamechagizwa na sera za nje za wamagharibi.
 
Wewe jamaa ----- kwa hiyo ulisikia hayo yanayofanyika ni kueneza dini? Utaenezaje dini kwa kuuwa? Ulizia hivo vikundi vinapata wapi silaha nzito na hio misaada?
 
Hayo ni makundi ya mercenaries yanayojificha kwa kutumia miavuli ya kidini ktk kutekeleza mambo yao pale washirika wao wanapokwenda kinyume na makubaliano ndio mauaji hutokea na kusingizia dini. Uislamu wetu haufundishi uovu wa namna hiyo. Wakati wa mtume (SAW) hakukuwa na ugaidi. Haya mambo yameshamiri kuanzia miaka ya 1990s na yamechagizwa na sera za nje za wamagharibi.

Hakuna muislam alieua watoto Pakistani. Ni Waarabu wameua watoto
 
Waislam wenye siasa kali wataisha pindi marekani itakapoacha kuwarubuni vijana wa kiislam na kuwapa mafunzo ya kivita ili wawapige wenzao,pia wakristo watakapoacha kuwabagua waislam ktk elimu ajira

Kweli wewe ni bongo lala...hapa wamarekani na wakristo wanahusika nini...mwana wa nuru kaongea kama binadamu mwenye ubinadamu mwenye ufahamu wale wakipakistani mlioua wanakosa gani?

huu ni ujinga kuwasingizia kila kitu wamarekani na wakristo. sisi wenyewe hatusomi kwan hili nalo ni la kutaka elimu ya juu kufikiri? UNAWAONA WANACHOFANYA BOKO HARAM?

si kupinga elimu ya magharib? angalau hawa wamepinga waziwaz unadhan ni wangap tunao hapa nchini hawakubal elimu ya magharibi? hebu uliza wasomi weng waliopo hivi sasa wenye miaka zaidi ya 50 kama hawakusoma shule za mishen na bado wamebak kuwa waislamu? angalia historia ya prof lipumba msomi mkubwa wa uchumi. wewe kweli unatumia akili hata kidogo ?

hakuna kitu cha ku justify killing one another hata iweje. uislamu unaonekana ni dini ya majitu makatili kwa sababu ya wapuuzi wachche ambao wanadhani wanaijua dini sana na wengine si binadamu.... hii inatupa shida hata kumshawishi mtu awe muislam labda tupate watu kama akina mike tyson ambao wao wana ukatili toka wadogo.

tuamke sasa tuacheni hizi imani mbovu mbovu tunajidhalilisha sisi wenyewe waislamu.
 
Hao wameuana ni magomvi ya kisiasa na kila mtu kutaka kutawala . Pakistan ni failed state kama vile nigeria baada uhuru kila mwaka mapinduzi ya kijeshi nao pakistani ni hivo hivo. Taliban na wengine wote wanagimbea kuingia ikulu kama M23 kule DRC . Wao kuwa waislam hakufanyi kutumwa na uislam kufanya ushenzi bali wanatumwa zaidi na tamaa ya dunia na kutawala.

Kinachotakiwa ni kupiga vita dhulma. Siasa kali ni tunda la dhulma na uonevu ulovuka mpaka. Watu wakikata tamaa ya maisha mpaka wakiamini potelea mbali i have nothing to loose ujue hapo ni hatari.hivyo tupige vita siasa kali za madhulumati. Tujenge taifa lenye haki na usawa. Hapo hakuna mtu wa kushawishi mwengine kufanya ufedhuli.

Na akitokea tutamzomea. Lakini tusipinge tu siasa kali bali hata siasa laini za Bakwata ambapo wanafanya ufisadi mkubwa kwa mali za waislam na then kulindwa na ssrikali na watu kama wewe.leo Bakwata imeuza kwa ufisadi nyumba za waislam pale upanga zaidi ya 30 . Wameuza kiwanja cha changombe ambacho lengo ni kujenga mashule.

Na sasa wameuza kile kiwanja morogoro rd na bini titi panapojengwa City mall na yule jamaa anauza maduka na maofisi yaliomo ndani. Siasa hii laini ya wizi na ufisadi wa Bakwata pia si wa kuungwa mkono na muislam au mkristo. Na inapotokea watu wenye msimamo sahihi wa kupinga wizi huu kama Ponda waungwe mkono na sio kubezwa na kudhulumiwa haki zao kwa vile wanapinga wizi huu wa siasa baridi za Bamwata.
 
Sasa dunia inakabiliana tishio la usalama linalosababishwa na uislamu wa msimamo mkali. Huu ni tishio kwa watu wote bila ya kujali dini zao, hata kwa waislamu wenyewe. Somalia, Nigeria, Misri, Syria, Indonesia, Kenya hadi Pakistani ni mifano michache ya wahanga wa mfumo huu wa uislamu wa msimamo mkali. Ngaa kipo kisingizio cha kueneza dini lakini kumekuwa na athali hata miongoni mwa jamii za kiislamu kama ilvyotokea majuzi kule Pakistani wakati waumini wa msimamo mkali walipowateketeza watoto wa shule zaidi ya 130. Kwa bahati mbaya, jamii ya waislamu imekuwa kimya kukemea na kuchukua hatua dhidi ya unyama huu uliovikwa vazi la kidini ili kutupumbaza na kutugawa. Sasa ni wakati muafaka jamii yetu ya waislamu kuamka na kuungana na jamii zingine dhidi ya hawa wajifanyao ndugu za waislamu na wenye kuwatetea kumbe sio na ni wenye kuwateketeza hata waislamu wenzao. Muda ni huu, tuchukue hatua kabla hatujajutia maamuzi yetu.

Nadeclare interest kwamba Siweki ushabiki ktk hili

Popote ambapo kuna matabaka kinzani ya mnyonyaji/mnyanyasajI vs. Mnyonywaji/mnyanyaswaji ni lazima kundi linalokandamizwa litatafuta mbinu za kutafuta usawa na kuzitekeleza hata kama mbinu hizo ni Mbaya [That is Human Nature].

So kinachotokea kwa waaslam globally ni zao la vitendo vya ukandamizaji vinazoendeshwa kwa ustadi mkubwa na kusimamiwa na Nchi za magharibi hususani USA na Uingereza. Na pia falsafa ya ku-brand uislam kama dini ya Vurugu; ambao inaendeshwa katika mfumo wa "Give a dog a bad name then kill it" katika Kiswahili rahisi ​"Mpe mbwa jina baya ili umuuwe";

unamuita gaidi ili umuue Cf. Ghadafi na Sadam. Lakini makundi mengine pia yametengenezwa na marekani mf. IS, alqaeda, etc. Hivyo basi kwa maoni yangu nadhani ni wakati muafaka kwa global community "to stop climinalising Islam".Ni dhahiri ya hata mtoto ukiwa unampiga kila siku lazima awe mtukutu.
 
Killing in the name of Allah!!! are christians doing the same? msikatae ukweli na kujificha katika kichaka cha kusingizia wazungu kuwa wanasababisha,kama uislam haufundishi siasa kali wazungu wasingefanikiwa kama ni kweli wanachangia, saidieni waislam wenzenu wa nigeria,Iraq,syria na maeneo mengine dhidi ya itikadi hiyo ya kipumbavu msikalie kusingizia wazungu jamaniiiiiiii

Talibani wanapigania madaraka kwa kushirikiana na Marekani
 
Back
Top Bottom