Waislamu na Wakristo tutumie dini zetu kudumisha amani na umoja wa kitataifa

Msamiati

R I P
Mar 6, 2011
1,065
697
Habari za wakati huu wapendwa,

Baada ya kusoma nyuzi mbalimbali kwenye majukwaa ya habari na hoja pamoja na Jukwaa la Dini, nimegundua ushetani mkubwa wa jitihada za kuhamasisha matabaka ya kidini na tofauti katika jamii zetu.

Nimegundua maneno ya kujenga chuki na usambazaji wa taarifa za kujenga hisia kali za kidini na mpasuko wa kijamii baina ya wakristo na waislamu kwenye Jamii yetu. Maneno ya kejeli, matusi mazito na maudhi yamekuwa kama lugha ya kawaida kwenye mijadala ya dini, tena sasa hivi imekuwa kama sample ya kutafutia umaarufu hapa JF.

Kwanza ningependa kuuliza kwa uchungu kabisa, je! tunapanda hii mbegu kwa faida ya nani ? hizi chuki za kuchukiana wenyewe kwa wenyewe tunazo pandikiza, tumeshawahi kukaa na kutafakari siku zikiota mizizi utakuwa mzigo wa nani ? Tumekaa na kutafakari faida ya hizi chuki za kidini ?

Naomba kuuliza ! Hivi ni kweli social interaction tuliyokuwa nayo baina ya waislamu na wakristo, hivi sasa haitufai tena na tunaitaji kuishi kwenye matabaka ya kidini na chuki kwa madai ya kutafuta pepo !? Ni sawa sasa kujenga mtazamo wa uadui baina ya waislamu na wakristo !? Tuwe na maduka ya waislamu na wakristo, tuwe na mitaa ya waislamu na wakristo, Je! tunataka iwe hivyo ?

Hivi ni kweli tumekuwa wapumbavu kiasi cha kushindwa kujua kuwa Mataifa mengi ya nje yanafanya dini as a part of social activities, vita na mauaji yanayoendelea sio tu kwa ajili ya masilahi ya kuingia peponi, bali kuna masilahi ya ki-utawala, masilahi ya kiuchumi, masilahi ya ki-taifa dini zinatumika tu.

Ndugu zangu, katika nchi zote duniani, Tanzania ni nchi pekee inayofata dini katika misingi ya haki, ndio maana kuna amani na utulivu huu tulio nao. Mungu wa kweli anatajwa hapa kupitia uislamu na ukristo ndio maana maombi ya Mshekhe na Mapadri kuiombea amani nchi yetu yamekuwa na mafanikio miaka yote.

Nigeria kuna Mashekhe na Mapadri kama hapa kwetu, wanaomba amani na wanaitaka kama ilivyo hapa kwetu lakini Mungu wetu mpenda haki na amani kutowajibu maana yake ni kwamba hawasimamii haki bali masilahi ya Kiuchumi, kiutawala na kijamii kama nilivyoeleza awali.

Hoja yangu kwenye paragraph mbili zilizotangulia, ni kwanini tuipe nafasi mienendo ya dini kwenye mataifa mengine iingilie utaratibu mzuri na mtizamo mzuri tulio nao kwenye imani zetu. Kwanini tuhukumiane, tuchukiane, tunyosheane vidole tutukanane kwasababu tu ya matukio yanayofanya Naigeria, Somalia, Kenya, Amerika, Uingereza na maeneo mengine duniani kwa kigezo cha dini ?

Tunaimani safi mbele za Mungu, Tuna ukristo safi na Uislamu safi. Miongozo ya imani zetu ni Biblia na Quran sio Wamarekani wala ISIS. Miongozo yetu haisapoti Ushoga wala Ugaidi, tunapoletewa hayo mambo yakiwa na sura za kidini tutambue kuwa ni hila za shetani, tuamke na kung'amua kuwa hawafanyi hayo kwa manufaa ya imani zetu, Tuamke.

Nimekereketwa na mengi sana kwenye swala hili lakini, naomba nimalizie kwa kuwasihi Ma Great Thinker katika hili, JF ina-impact kubwa sana kwenye Jamii, Taifa letu linaweza kuharibika kabisa na kuingia kwenye machafuko makubwa ya kidini na chanzo kukawa mimi na wewe kutoka JF.

Kwa mada hii, Simaanishi kuwa ni vibaya kufanya midahalo inayohusiana na tofauti za imani zetu, sio vibaya kujadili uungu wa Yesu, wala sioni vibaya kujadili uislamu wa kina kaini na Habili, mijadala hii ilikuwepo mika na miaka tena tumeifanya kwa mihadhara na kuheshimiana.

Nashauri tuzingatie zaidi mambo yanayotuunganisha kuliko yale yanayotutenganisha, Tofauti kwamba mtume wa wakristo ni Yesu na mtume wa waislamu ni Mohammad S.A.W sio kitu cha kufungamana nacho sana kuliko ukweli kuwa Wote tunamwita Mungu mmoja, wote tunaamini mitume mbali mbali iliyoshushwa na Mungu.

Naomba kwa moyo mkunjufu niwaalike wote kwenye mjadala
Shukran.
 
Viongozi wa serikali, wananyima haki za wananchi; amani itatoka wapi? Jamani itumike kuwajenga viongozi wetu ili watende haki.

Nayachukia sana majitu tuliyoyapa fursa/dhamana ya kutuongoza halafu yanachafua hali ya hewa ya nchi na mkubwa wao anayashukuru kuwa machafuzi haya walitoa uongozi wenye uaminifu na uadilifu!

Pambaf!
 
hao ni ''KEYBOARD GANGSTERS''.....KWA KUWA HAWAONEKANI WANAAMINI HAWAKAMATIKI HATA WAENEZE CHUKI VIPI.....
online_fraud.jpg
word-gangster-on-keyboard-rs112054536.jpg

 
kwa kuwa leo nimekutana na muislamu muungwanana mstaarabu naomba niitumie nafasi hii kujielimisha na baadhi ya mafundisho ya kiislamu niliyowahi kusikia. Mnasena muislamu ndugu yake mwislamu na ukimuua asiye mwislamu unapata thawabu.
Ikoje hii ndugu yangu?
mie sina dini
 
Huoni kwa kufanya hivyo wewe mwanadamu unampigania Mungu wako kana kwamba Mungu unayemuamini hana uwezo wa kujipigania mwenyewe bila intervention yako? Unaweza kumshusha Mungu kiasi hicho na ukajihesabu uko sahihi bado?
 
Shida kibwa inayotuchanganya ni tofauti ya wenye nacho na wasionacho. Walionacho wanatetea walichonacho kwa kutumia wasionacho kwa kisingizio cha imani ili wawamalize adui zao.
Wewe masikini mwenzangu mkristu au muislamu tunachogombania ni nini kama sio kuna tajiri pembeni anamlipa mmoja wetu ili aue.
 
Sengeon 13:01 Today
Nimejaribu kufikiri habari za Magaidi nikashindwa
kupata majibu hasa wanachokitaka ni nini. Jana
Nchini Pakistan kundi la Taleban lilishambulia
Shule na kuua Watoto zaidi ya 84. Watoto hawa
ni wadogo na ambao hawafahamu chochote
kuhusu ugomvi wa Taleban na Serikali. Lkn hayo
Mashetani wamewaua na kudhulumu haki zao za
kuishi.
Sasa ukijaribu kuuliza kuwa faida yao ni nini
wanasema wanatetea Dini ya Mwenyezi Mungu.
Hivi mwenyezi Mungu anatetewa kwa kudhulumu
haki ya kuishi ya wanadamu wengine? Na je
huyu Mungu anayetetewa amekosa nguvu kiasi
gani mpaka atetewe na Mtu ambaye yeye ndie
aliyemuumba?
Mimi naamini kuwa Kama hawa watu
wanapigania Dini, Basi Dini hiyo ni ya Shetani na
haifai kuwepo Duniani.
Mu7 nzalendo incharge mseku

Wapendwa Hebu tuwe watu wenye kutazama kwa upeo mrefu na mpana..... Sasa uzi huu ulilenga BOTH dini zote mbili (WaiSlam & WaChristo) !! Lakini inaonesha wazi Wote tumejikita kuuzungumzia Uislam (interesting au Kizuri kinachovutia).!!

Niwape Mfano mdogo ktk daily life za kila siku:~ Yaani wengi tunashuhudia na kuona kuwa wapo waDada/Mabinti wanauza miili yao kama kazi za Ukahaba, Sasa ni haki kweli ndiyo tuwatuhumu wanawake wote kuwa ni waovu au ke wote ni malaya ?!!!? ambapo kuna Mama zetu na dada zetu na shangazi,Bibi na binti zetu wa kuwa zaa!! Hakika hivyo itakuwa Uonevu !!

Jibu kw andugu Videsto,
Hadi hii leo hakuna Mtu anadai kuuwa au kudhuru Mtu mwingine kwa WAKALA wa dini ya kiislam.... hiyo NEVER !! ila huyo Muuaji anakuwa na agenda zake, anakuwa na uchu wake fulani, au Upiganaji wa kunyakuwa Madaraka fulani.
Sasa Mkuu Usichanganye Makundi ya wapiganaji na Jamii ya Wacha Mungu wenye Imani za Dini. Huko PAKISTAN na AFGHANISTAN hakuna tofauti na tunayoona kwa jirani zetu wa KENYA na SOMALIYA !!!! again ni makundi makundi yenye kupigania na kushurutishana na kulazimisha kati yao " WHO is WHO "
Hapo nothing to do with Mwislamu na Imani yake ( japo kuwa wakazi wengi ni waisilamu) Je hawatakim Uongozi?!!

Si Ndonkasema binaadamu ameumbwa na kukirimiwa na kufadhiliwa, Sasa tuna Mazuri yetu na Maovu yetu....Shetani hutumika pande zote. ( Wengine hutumia silaha na wengine hutumia ulimi katika utendaji ).
Na kuhusu Dini hapa Duniani kila mmoja atafuata aitakayo hapatukwa na shortage/uhaba wa waumini. Motokeo baada ya Uhai/siku ya mwisho.

Mpendwa Mu7,
Karibu sana uujue Uisilamu , hata kama hautoufuata Lakini utamaduni na Thaqafa zake utakupa manufaa ya maisha mbeleni....KM;- Uvumilivu, kwenye Msiba,kuabudu kwa raha na tafrija,kupenda Masikini,kuondoa kiburi,nk,nk...
Uisilamu kamwe haupropagate kuuwa upate Thawab, Bali hata kuchinja kuku au myamama (mbuzi,kondo,ng'ombe,nk) kuna Rehema na huruma ya kumtendea ili asiteseke au kujeruhika...Ndo maana waisila wakapewa jukumu la Kuchinja. !!

karibu sana na Ubarikiwe.
 
Last edited by a moderator:
Japokuwa mm sijaalikwa kuchangia bt naomba nikupongeze mtoa mada. Mbegu ya udini n mbaya kuliko hata ya ukabila na siasa. Hatatoka mtu! Nimeishi na ndugu zangu waislamu km majirani, shuleni, chuoni na wengine n ndugu wa ukoo & hata maeneo ya kazini waislamu ni wengi. Sijaona tatizo nao na ninafurahi kuwahudumia. Maandiko yanasema, "Tukiwatendea mema wale tu walio kwetu hakuna thawabu."

Ila kuna maswali najiuliza, hawa magaidi kwa nn wameweza kufanikiwa kuutumia mwamvuli wa uislamu namna hii? Je! Kuna juhudi zozote zilizofanywa na waislamu kuwapinga? Kama zipo na hazikufanikiwa, kwa nn mataifa ya magharibi yapoingia kuzuia ugaidi waislamu wanayachukia tena? Sielewi! Mtu akinielewesha hapa nitafurahi, otherwise simchukii mtu lkn naishi na maswali kichwani.

Mungu ibariki Tanzania, dumisha uhuru na umoja.
 
Japokuwa mm sijaalikwa kuchangia bt naomba nikupongeze mtoa mada. Mbegu ya udini n mbaya kuliko hata ya ukabila na siasa. Hatatoka mtu! Nimeishi na ndugu zangu waislamu km majirani, shuleni, chuoni na wengine n ndugu wa ukoo & hata maeneo ya kazini waislamu ni wengi. Sijaona tatizo nao na ninafurahi kuwahudumia. Maandiko yanasema, "Tukiwatendea mema wale tu walio kwetu hakuna thawabu."

Ila kuna maswali najiuliza, hawa magaidi kwa nn wameweza kufanikiwa kuutumia mwamvuli wa uislamu namna hii? Je! Kuna juhudi zozote zilizofanywa na waislamu kuwapinga? Kama zipo na hazikufanikiwa, kwa nn mataifa ya magharibi yapoingia kuzuia ugaidi waislamu wanayachukia tena? Sielewi! Mtu akinielewesha hapa nitafurahi, otherwise simchukii mtu lkn naishi na maswali kichwani.

Mungu ibariki Tanzania, dumisha uhuru na umoja.

Kiongozi wa urusi amepiga marufuku kufananisha uislamu na ugaidi kwakuwa ni vitu viwili tofauti
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1418823697981.jpg
    uploadfromtaptalk1418823697981.jpg
    113.8 KB · Views: 125
Kutoka kwa mbunge urusi
The MP said in an interview with Izvestia that lately the mass media are freely and frequently using expressions like ‘Islamic terrorists’, ‘Islamists’, ‘Jihadists’, ‘Shahid belt’, ‘Terrorist Islamic State’ and many others of this kind.

“These expressions push people towards the conclusion that Muslim religion and terrorism are the same thing. Common people automatically begin to associate Muslims with bandits, murderers and terrorists,” Saraliyev said.

At the same time, the majority of Muslims prefer to distance themselves from radical groups, preferring to call them ‘Kharijites’ – Arabic for ‘dissenters’ or ‘insurgents’, the lawmaker noted.

One typical example of such people are the supporters of the Islamic State (IS, formerly ISIS/ISIL), he said.

“They call themselves the Islamic State, but they have absolutely nothing to do with Islam! For them Islam is just a cloak with which they cover their evil deeds!”

Saraliyev reiterated the thesis that traditional Islam is a kindness and creation that promotes peaceful coexistence between all peoples. The reports about Muslim religion calling for aggression and extremism is a either a mistake or a baseless lie, he added.
 
Na mahakama ya umoja wa ulaya imeitoa hamas kwenye list ya magaidi, which means they are fighting for a good cause, kutetea ardhi yao isichukuliwe na ubaguzi ndani ya ardhi yao wenyewe
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1418824812898.jpg
    uploadfromtaptalk1418824812898.jpg
    18.7 KB · Views: 78
  • uploadfromtaptalk1418824943332.jpg
    uploadfromtaptalk1418824943332.jpg
    48.9 KB · Views: 79
Na mahakama ya umoja wa ulaya imeitoa hamas kwenye list ya magaidi, which means they are fighting for a good cause, kutetea ardhi yao isichukuliwe na ubaguzi ndani ya ardhi yao wenyewe

Okay...kwa mtazamo wako makundi ya kigaidi n km yapi?
 
Love is the only solution. I have a dream speech by martin luther ina maana kubwa sana. Judge through content of the mind and not color of their skin or ethinicity or tribe or religion. Dini zote zimeletwa na wakoloni waliotutesa na bado zinatutesa akilini mwetu...i am African.
 
Kwa uzoefu ni kwamba mijadala baina ya dini zenye imani tofauti huishia kuvunja amani maana haiwezekani kufikia consesus. Therefore ni meaningless kuwa na mijadala ya aina hiyo. Lakini zaidi sana mijadala ya kidini kati ya ukristo na uislamu haiwezi kuisha vzr maana ukweli wenzetu waislamu si watu wa amani kabisa. Huo ndio ukweli!

Waislamu sio watu wa amani kama jinsi unavyoona na kusikia kwenye mataifa mengine mimi ni mkristo, nimesoma nao, nimekua nao nafanya nao kazi, ni watu wazuri kuliko watu wengine wowote wale. may utupe mfano wa waislamu unaoona sio watu wema ndani ya jamii yetu na mabaya waliyofanya ili turekebishane. Juzi maostadh wamejitolea kusafisha mifereji huku mtaani kwetu, mifereji inayotumiwa na wakristo na waislamu bila kujali, waislamu wa tanzania ninaowajua mimi ni watu Wema, Nita ujaji uislamu kwa hawa ninaowajua mimi na wanao nizunguka
 
Ondoa dhulma katika jamii
Ondoa ubaguzi na upendeleo maeneo ya kazi hasa za umma
Gawa keki ya taifa kwa haki kwa watu wote; na sio kuwapa jamii moja

Amani ni zao la haki, ukweli, na upendo kwa wote;
 
Kwa kuwa leo nimekutana na muislamu muungwanana mstaarabu naomba niitumie nafasi hii kujielimisha na baadhi ya mafundisho ya kiislamu niliyowahi kusikia. Mnasena Muislamu ndugu yake mwislamu na ukimuua asiye mwislamu unapata thawabu.
Ikoje hii ndugu yangu?

@nzalendo Na hivi ndivyotunavyotakiwa kuishi, Ukifanikiwa kumuelimisha vizuri, umeshamuokoa ndugu yako na kumuingiza kwenye dini ya haki
 
Back
Top Bottom