Waislamu Ikataeni CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waislamu Ikataeni CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kamanzi, Feb 11, 2011.

 1. k

  kamanzi Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Asalam Aleikum waungwana. Leo mimi kama mtanzania mwenye uchungu na watanzania wa dini zote naomba kuchukua nafasi hii kuwashauri ndugu zangu waislamu. ACHANENI NA CCM INAWALOSTISHA. SAbabu ni nyingi ila nawapa hizi chache hapa chini:

  CCM imewadanganya kuwa itawapa mahakama ya kadhi na kuiingiza Tanzania kwenye jumuiya ya kiislamu (OIC). Cha kusikitisha ni kwamba hadi leo hii hakuna hata dalili ya debates juu ya swala hilo. Kama wangeona ni muhimu kufanya hayo wangeshafanya. Kama mnabisha angalia walivyolikubali kwa haraka swala la kuilipa DOWANS. Yani hilo swala lilikuwa muhimu mpaka uamuzi wake haukuitaji kikao cha baraza la mawaziri. KWA TAHARIFA TU, priority ya CCM kwa sasa ni kuimaliza CHADEMA. Hilo la mahakama ya kadhi na OIC ni changa la macho.

  Pili, CCM inauzalilisha uislamu kwa kuwachaguliwa kionozi wao wa dini. Amini usiamini, ni dini ya kiislamu tu inachaguliwa kiongozi wake (mufti) na CCM kwa kupandikizwa na Usalama wa Taifa (TISS). YAni hata dini ndogondogo Tanzania zipo huru na mkono wa CCM lakini dini kubwa kama uislamu kuchaguliwa wa kuwaongoza ni dharahu zinazopaswa kupingwa waziwazi.

  Tatu na mwisho kwa leo, wale walioko CCM wanaojiita waislamu na kuwashawishi si waislamu wa kweli. Niliwahi kuwaeleza kuhusu paper iliyokuwa presented hapa Cambridge University na authority wa dini ya kiislamu (jina kapuni). Yeye alisema hivi, kuna tofauti kubwa kati ya moslem (kama hawa waliopo CCM) na islamists (waislamu wa kweli). Moslem wapo kwa faida ya matumbo yao na wala si kumcha Mungu. Ndio maana Makamba ni moslem, Rostam ni moslem, Kikwete na DOWANS yake no moslems ndio maana hawaogopi Mungu wanaila Tanzania mchanamchana. Mpaka uwe islamist ndio unakuwa musilamu kwelikweli. Sasa nyie ndugu zangu kwanini mnakubali kuendeshwa na Moslems badala ya Islamists? IKATAENI CCM tuijenge nchi mpya kama EGYPT walivyoamua kuondokana na Moslem wao MUBARAK!!!
   
 2. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mambo si mambo, imekaa kidini dini lakini inaukweli japo sina data zaidi ya kujionea mwenyewe na kusikia kwa masikio yangu.

  Maoni yangu:
  1)Nachoona hapa mie ni kuwa adui yetu si dini wala kabila au chochote kile ila kuna watu wakiongozwa na CCM wanatumia hizi dini, kabila na kila aina kutuvuruga watanzania. kwa interest zao.
  2) Hakuna haja ya kujiingiza kwenye imani zetu na siasa, tukaeni pamoja tuwape somo hawa viongozi wetu. Kinachofanyika hapa ni kama kukomoana kuwa kwa kuwa umeniumbua basi na mimi nakuvurumishia haya makashfa yasiyo ya kweli.
  3) Hizi dini zikae pembeni japo zina influence kubwa kwa watanzania wengi lakini wakae kimyaaa, wao wapige neno na kuwaonya hawa viongozi wetu. Lakini kwa vile viongozi wa dini hawako pamoja basi leo huyu kesho yule kila mmoja anavutia kwake mwisho wa siku wanasiasa wanaanza kutumia hizo tofauti za kidini kujipatia yale wanayotaka.

  MWISHO: udini,ukabila na umimi havitatufikisha popote zaidi ya kutuchelewesha, ila kuna watu wanapenda hivyo vitu na ni juu yetu kuwakemea kwa pamoja.
   
 3. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Mkuu mwana Cambridge,salama? Huku manzese hatujambo! Mkuu udini uko kwenye vyombo vya habari na ukija huku mtaani hatuna udini! Ccm inaaminisha raia kuwa kuna udini wakati serikali ya ccm ndo korofi,ila hapa moslems fight a devil they don't know! Wanakimbilia kuilaumu cdm wakati hawana udhibitisho kuwa kama cdm ni ya kidini basi ccm ni ya waislam au ccm haina dini/wapagani! Hapana! Hapa ni uchochezi wa ccm kuhiaribu nchi. Rais ajaye ana kazi ngumu sana kulijenga taifa!
   
 4. Mwadui

  Mwadui Senior Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mtoa mada nakuunga mkono, ccm inatumia mgongo wa waislamu kufanikisha mambo yao, na waislamu nao wamekubali kutumika wakihisi kuwa ccm ni mkombozi wao, kumbe not
   
 5. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  CCM ni adui wa kila Mtanzania sio waislam au wakristo wote asui yetu ni CCM na Fisadi Kikwete:twitch:
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Dini na siasa hazitenganishwi, kwani zihusu mifumo ya maisha. Ila faith tolerance between variuos religion is inevitable for life to go on. Tatizo lililopo sasa ni la kitaalamu, jinsi ya kutengeneza miundo ya vyama na serikali ili kuondoa hisia na dhana za udini. Unakuta chama kina viongozi wote karibu kutoka dini fulani, hii inaua chama ikiwa kimo katika jamii yenye mchanganyiko wa dini mbalimbali. Hii nimetoa mfano tu. Lazima kuwe na mikakati, hasa kupitia usalama wa umma, kuvisaidia vyama kubalance structures. CCM asilia wanajua mambo haya, sijui vyama vingine vinajua.

  Msipokuwa makini mtachakchuliwa na wenye uchu wa madaraka. Ila na kwa usalama wa taifa hili jukumu ni muhimu kwa maslahi ya taifa. Inabidi tutoke huku kwanye mapambano ya udini.
   
 7. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,893
  Likes Received: 5,346
  Trophy Points: 280
  this ia crap,garbage,bullshit,...huwezi ukabalance dini kwenye uongozi,uongozi utokane na sifa,..kama wote ni waislam poa au wote ni wakristo poa ili mradi wawe na sifa,...haya mawazo yenu ya kidini mnayapata wapi??
   
 8. A

  ASK Member

  #8
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asalam Aleikum. si nia yangu kupinga maoni yako, ila ninachona unapendekeza watu wachague kiongozi kwa kutumia viongozi wa vyama vya siasa vinavyoegemea kwenye uislam! Naona unakotupeleka ni kwenye udini ambao baadhi ya viongozi wamekuwa wakiuhubiri kwamba upo ilhali mwananchi wa kawaida hajauona na wanaishi pasipo kujali dini ya mtu mwingine.
  Kama hoja ni CCM na udini mbona hujawaambia waislam wachague kiongozi wa chama gani ambacho kitakuwa kinasimamia maslahi ya waislam zaidi?
  Nikiangalia Egypt naona hakuna tofauti ya Muislam na Mkristo katika kudai maslahi yao.
  Hoja ya udini isiendekezwe kwani inaweza kutugawa wa TZ ambao katika makazi ya yetu hususani nyumba za mijini tunaishi pamoja tukiombana kiberiti cha kuwashia moto asubuhi na jioni hukaa barazani kucheza bao pasipo kuulizana dini.
  Tujenge hoja za kupambana na viongozi wasiotujali kwa misingi ya kuwa tu WATANZANIA na si kwa misingi ya MIMI MUISLAM NA YULE MKRISTO.
   
 9. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #9
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Okay nimekusoma wakishaikataa waende chama gani kitakacho watekelezea ahadi zilizohadaiwa na CCM? umeelezea hoja zako lakini umewaacha njia panda hukuwaeleza chama mbadala kitakachowafaa!
   
 10. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,893
  Likes Received: 5,346
  Trophy Points: 280
  cuf
   
 11. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Huu ni udini, hata kama kuna point ukishaweka udini unazitenga jamii zingine zisizoamini katika imani yako wewe.....
   
 12. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hoja walizohaidiwa haziwezekani kwa kuwa Tanzania haina dini 'secular state' ile ilikuwa danganya toto, kuhusu chama cha kwenda ni dhahiri kwamba ni uamuzi wao maana vyama vipo zaidi ya 15 Tanzania, maana hatacuf nao ni wale wale tu.
   
 13. Malunkwi

  Malunkwi JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  c waislamu wote tumekubali kutumiwa na ccm!! Islamists tunasimamia tunachokiamini ccm ni wanafiki wakubwa
   
 14. d

  dotto JF-Expert Member

  #14
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Udini katika siasa za TAnzania ni wa kuchonga ili watu waconcentrate na udini wasahau kudai haki zao kama katiba, pesa zao zilizopokwa na mafisadi. So, mafisadi hutumia magazeti yao na midomo yao na nafasi zao wamekuwa wakipelekea kuwa hawapendwi sababu ya dini yalizonazo. Mfano. Dr.Salim A.Salim ni mtanzania mwenye dini gani asiyemdhamini kama kiongozi wa ukweli. Wamekigawa chama chao kimakundikundi na sasa wanatugawa watanzania kiitikadi. Tuwe macho maana kiongozi dhaifu ndo zao!!
   
 15. N

  Nyamanoro JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 575
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 60


  Ushauri wako umechelewa!! Kwanini usubiri ccm kimeingia tena madarakani ndio utoe ushauri huo wakati unajua kabisa ahadi hizo hazikutolewa leo?.
   
 16. A

  ATENGEZEKE Member

  #16
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haaaa unachekesha kaka mlisha onyesha tangu mwanzo kuwa chadema ni chama cha kanisa ndio maana mlimsimamisha mchungaji agombee.mmekosa ndio mnarudi kutafuta wanachama wa kiislam,tutajiunga baada ya slaa kuoa maa takrab zinaaaaaaaaa
   
 17. peck

  peck JF-Expert Member

  #17
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 220
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  mi naona itakuwa nzuri kama waislamu wote muwe CUF na wakristo wote tuwe CHADEMA halafu CCM wabaki mafisadi wote pamoja na wasio na dini halfu vyama vingine vyote vibaki na dini zingine zote, nadhani hii itakuwa bab'kubwa.
   
 18. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #18
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hivi unafikiri Waislamu ni wajinga? yaani unataka kuwafundisha na kuwaonyesha wapi ndipo kunapowafaa? yaani wao hawajui wala hawaoni? sasa kama unawashauri Waislamu wajiondoe CCM NA SIDHANI kuwa waislamu wote wako CCM kwani wako wengi wasio na chama, wengine wako CUF, wengine wako CDM, na hata NCCR! una chama kingine mbadala ambacho kitawahakikishia Waislamu kupata mahakama ya kadhi, OIC, na haki zao zote?
   
 19. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #19
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo mko tayari kuwapoteza ZITTO na ARFI?
   
 20. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #20
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Simple mind tend to ignore simple things that may cause a very big dissester. to them everything is crap. it is ok anyway. Sasa kwa taarifa yako hatutoki CCM, kwa sababu wameweza kutuweka pamoja watu wa dini zote. Nyie bakini na vyama vyenu vya udinidini.
   
Loading...