Waislam wataka haki zao ndani ya katiba

Pafyum

JF-Expert Member
Feb 7, 2012
208
112
TAASISI ya Jumuiya ya Waislamu na Taasisi za Kiislam, zimetaka Katiba mpya itamke kuwepo na chombo cha kisheria kitakachosimamia na kuwa na mamlaka ya kusikiliza masuala ya Kiislamu. Maoni hayo yaliwasilishwa jana jijini Dar es salaam kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na viongozi wa taasisi hizo waliowakilishwa na Sheikh Musa Kundecha.

Kundecha alifafanua kuwa wametaka Katiba mpya iwe na chombo hicho na kwamba mchakato wake ufanyike kwa umakini ili kuepusha ucheleweshaji kama ilivyokuwa katika Mahakama ya Kadhi. Pia walipendekeza kuwa mawaziri wote wasiwe wabunge bali wachaguliwe na taasisi, asasi, vyama vya siasa na viongozi wengine.

Aidha Kundecha alisema wamependekeza Katiba mpya itoe uhuru wa elimu ya dini katika mashule yote. Pia suala jingine ambalo walitaka litamkwe katika Katiba ni kutaka waumini wa Kiislam, siku ya Ijumaa wafanye kazi nusu siku. Alisema kuwa siku ya Ijumaa ni siku ya ibada hivyo Waislamu wanatakiwa wapewe mapumziko.

Aidha Sheikh Kundecha alisema kuwa amependekeza kutenganishwa kwa vyeo vya ubunge na uwaziri ambapo alisema hali hiyo inasababisha kuwepo kwa upendeleo wa maendeleo katika maeneo mbalimbali. Naye askofu mkuu wa kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Mashariki mwa Tanzania, Mchungaji Mark Malekana, ametaka rasilimali za nchi ziwekewe usimamizi ulio wazi kwa watu wote.

Pia kanisa hilo limetaka fursa za maendeleo ziwe sawa katika maeneo yote ambapo mchungaji huyo alisema kwa sasa kuna maeneo yameendelea zaidi kuliko mengine hivyo ametaka Katiba mpya itamke juu ya kuwepo kwa usawa katika maeneo yote.


Source: TANZANIA DAIMA
 
maoni mazuri kabisa,lakini kwa kuwa utawala wa ccm hawapendi haki sawa kwa wate,haya maoni mazuri watayapinga
 
maoni mazuri kabisa,lakini kwa kuwa utawala wa ccm hawapendi haki sawa kwa wate,haya maoni mazuri watayapinga
hapo hakuna kwa upande wa kuundwa chombo cha kisheria cha kusimamia masuara ya waslam siungi mkono kabisa, katiba inatakiwa iwe neutral isitambue dini ya mtu yeyote je? kila dini ikitaka iwe na chomo cha kisheria tutafika? Serikali itahudumia vyombo vya kidini vingapi?
 
hapo hakuna kwa upande wa kuundwa chombo cha kisheria cha kusimamia masuara ya waslam siungi mkono kabisa, katiba inatakiwa iwe neutral isitambue dini ya mtu yeyote je? kila dini ikitaka iwe na chomo cha kisheria tutafika? Serikali itahudumia vyombo vya kidini vingapi?
wewe una chuki na waislam,sasa embu tueleze kati ya yote yaliyosemwa na waislamu ni lipi unaunga mkono?
 
Back
Top Bottom