Waishitaki INEC wakitaka irekebishe kanuni za maadili

Waishitaki INEC wakitaka irekebishe kanuni za maadili

Hamna kitu hapa. Huyu hawezi kuwa BOLD judge! Watoto wa juzi hawa hawawwezi ku resist pressure za madikiteita!

RIP MWALUSANYA, KATITI, LUGAKINGIRA
Mnalipwa pesa kiasi gani Ku-underrate harakati za hao vijana.
 
Wanaharakati wanaojitambulisha Raia ni Sisi, Kumbusho Kagine na Bubelwa Kaiza wamefungua kesi namba 12670/2025 kupitia mtandao dhidi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiiomba Mahakama itoe amri ya kurekebisha upungufu uliomo kwenye Kanuzi za Maadili ya Uchaguzi.

Taarifa kutoka kwa Raia ni Sisi wanaowakilishwa na mawakili wasomi Mpoki Bukuku na Jebra Kambole imesema kesi imetajwa leo Jumatano, Juni 25, 2025 mbele ya Jaji Kagomba, Mahakama Kuu Dodoma.

Taarifa Zaidi zinadai kuwa Serikali imeweka pingamizi dhidi ya umahiri wa kiapo.

“Jaji Kagomba amepanga kusikiliza na kutolea uamuzi pingamizi la wajibu maombi siku ya Alhamisi Julai 3, kisha, iwapo ataona pingamizi halina mashiko, kuendelea kusikiliza shauri hilo. Shauri litasikilizwa Mahakama ya Wazi, [Mahakama Kuu] Jijini Dodoma,” imesema taarifa ya Raia ni Sisi.
Lifunguliwe na shauri la dharula kusimamisha uchaguzi mkuu hadi haki za maoni za wananchi kuhusu marekebisho ya sheria zifuatazo kuelekea kipindi hicho zifanyike ndipo uchaguzi ufanyike
1. Matokeo ya rais yahojiwe mahakamani
2. Wapiga kura waondoke na namba ya karatasi ya kupigia kura kama ushahidi kwamba alipiga lakini kuwa tayari (to corroborate evidence once recalled in teh court of law)
3. Mwenyekiti na wajumbe wa tume wasiwe wateuliwa wa rais ambaye naye ni mgombea na wasiwe wanachama wa chama chochote cha siasa sio kukana kwa muda uanachama wakati ndani wanafahamu wanalinda maslahi ya nani
4. Polisi wasiingile mchakato mzima wa uteuzi, uthibitishajjina ugombeaji wa nafasi yoyote ya kisiasa
5. Matokeo ya awali yatangazwe kila kituo cha kupigia kura kuanzia madiwani, wabunge mpaka ya rais ujulikane kituo mama kabla ya majumuisho
6. Wakati wa kutangaza matokeo ya rais polisi wasihusishwe ila wanajeshi pekee ndio wasimamie
7. Sheria ya usalama wa taifa iliyofanyiwa marekebisho na kuwapa mamlaka ya kukamata, kuhoji na kushikilia mwamnanchi anayetofautina na itikadi ya mwananchi mwingine ifutwe
8. Iwe ni marufuku kwa spika na wabunge kuitetea na kusifia serikali nje ya kushauri, kuisimamia na kuiwajibisha mahali panapostahili
9. Chama tawala kilichoko madarakani kwa sasa kiache tabia ya kuwanyanyasa wananchi wanaowahoji kuhusu kutowajibika ikiwa pamoja na rais ambaye wao ndio waajiri wake, asitumie vyombo vya dola kunyamazisha maoni jenzi hata kama hayamfurahishi yeye au wapambe wake binafsi
10. Chama tawala kiache kejeli kwa wapinzani na kuchochea migogoro kupitia msajili
11. Serikali iache kukadamiza haki ya kuabudu kila mwenye itikadi yake ilimradi havunji katiba nasheria za nchi
12. Watu wote waliokamatwa, na kubambikwa kesi za kisiasa waachiliwe bila masharti ili kuimarisha matendo ya HAKI, AMANI, UPENDO, MSHIKAMANO na WAJIBU wa wananchi na watawala.
13. Vikundi vya wasiojulikana vikomeshwe kwa dhati bila kuingiza siasa na polisi ijitenge na wanasiasa kuwatumia kuumiza wananchi wenye mtazamo tofauti na wafuasi wa chama tawala
14. Vitendo vya utekaji vikomeshwe na wahusika wapatikane na kuchukuliwa hatua za kisheria bila kujali cheo, nafasi katika jamii au mamlaka aliyokasimiwa
15. Chama tawala kisijimilikishe na kuhodhi uongozi kwa nchi nchi ya Tanzania wakati kila Mtanzania mwenye itikadi tofauti ana haki ya kuiongoza kwa mjibu wa katiba iliyopo.

TANZANIA BILA UONEVU INAWEZEKANA kinachohitajika ni BUSARA, HEKIMA, NA UNYENYEKEVU kwa wnanchi wote

'Allegiance' inajitokeza baada ya kutomtendea haki mwananchi aliyedhulumiwa
 
Leo Jumatano, Juni 25, kupitia mtandao, kesi namba 12670/2025 imetajwa mbele ya Mhe. Jaji Kagomba, Mahakama Kuu Dodoma. Kesi imefunguliwa na Raia ni SiSi; Kumbusho Kagine pamoja na Bubelwa Kaiza, wakiwakilishwa na Mawakili wasomi Mpale Kaba Mpoki na Jebra Kambole

TOKA MAKTABA :
14 Aprili 2025

Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi INEC, Ramadhan Kailima - CHADEMA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI WOWOTE HADI 2030

1750870007858.jpeg

Photo : Bw. Ramadhan Kailima wa INEC

Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi - INEC, Ramadhan Kailima amesema Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema hawatashiriki uchaguzi huu hadi mwaka 2030.Chadema ni kati ya vyama 19 vya siasa vilivyosajiliwa Tanzania, Na ndicho chama pekee ambacho hakijasaini kanuni za uchaguzi, jambo ambalo linawanyima fursa kisheria kushiriki katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 nchini Tanzania unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba, 2025.
 
TOKA MAKTABA :

02 JUNE 2025

KIONGOZI MKUU ACT WAZALENDO - SINA IMANI NA TUME YA UCHAGUZI INEC

1750870234745.jpeg

Wakati Tanzania ikielekea katika uchaguzi mkuu wa kiti cha urais, wabunge na madiwani Oktoba mwaka huu, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo ina dhamana ya kusimamia uchaguzi na kuhakikisha wananchi wanashiriki uchaguzi ulio huru na wa haki, imekuwa ikilalamikiwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani kikiwemo chama cha ACT Wazalendo. Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Dorothy Semu ameniambia ni kwa nini hawana imani na Tume hiyo.
 
Leo Jumatano, Juni 25, kupitia mtandao, kesi namba 12670/2025 imetajwa mbele ya Mhe. Jaji Kagomba, Mahakama Kuu Dodoma. Kesi imefunguliwa na Raia ni SiSi; Kumbusho Kagine pamoja na Bubelwa Kaiza, wakiwakilishwa na Mawakili wasomi Mpale Kaba Mpoki na Jebra Kambole

TOKA MAKTABA :
14 Aprili 2025

Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi INEC, Ramadhan Kailima - CHADEMA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI WOWOTE HADI 2030

View attachment 3382950
Photo : Bw. Ramadhan Kailima wa INEC

Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi - INEC, Ramadhan Kailima amesema Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema hawatashiriki uchaguzi huu hadi mwaka 2030.Chadema ni kati ya vyama 19 vya siasa vilivyosajiliwa Tanzania, Na ndicho chama pekee ambacho hakijasaini kanuni za uchaguzi, jambo ambalo linawanyima fursa kisheria kushiriki katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 nchini Tanzania unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba, 2025.
Sura inaongea
 
WANAHARAKATI WAHOJI BUNGE KUCHELEWA KUFUNGWA KUNA NINI, CCM WATAKA CHADEMA WALETE MGOMBEA,NO REFORMS

View: https://m.youtube.com/watch?v=P0Gza-ycva0

Watu makini wajadili kuhusu haya Mambo yanayotokea kwa sasa, muda utatuambia kama Bunge la Dodoma pia litaongezewa ukomo wake zaidi kutoka tarehe 27 June 2025 hadi 13 Agosti 2025,
  • je itakuwa kwa ajili gani ? miezi karibu miwili ya ziada Bunge la CCM litafanya majukumu gani ?
  • Je Kujazana mapesa au
  • Je ni kupitisha miswada ya dharura?
  • Je Miswada hiyo ni ya kukubali hoja za kundi kubwa la watanzania wanaodai No Reforms No Election ?
 
JE, BARAZA LA WAWAKILISHI LIMEREFUSHA MUDA ILI KUTUNGA SHERIA MPYA ?

Unguja, Zanzibar

Rais Dr. Mwinyi aongeza ukomo wa Baraza la Wawakilishi hadi Agosti 13, 2025

1750870911011.jpeg

Habari kwa kina :
Dk. Mwinyi alitoa kauli hiyo leo, Juni 23,2025 wakati akihutubia hotuba ya kulifunga baraza hilo huko Chukwani, Zanzibar, ambapo alisema ukomo wa Baraza la 10 utafikia mwisho Agosti 13 2025, kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.

Amesema kwa mujibu wa Kifungu cha 91(2)(a) cha Sheria ya Zanzibar ya mwaka 1984, anayo mamlaka ya kuongeza muda wa Baraza hilo.

Baraza hilo la 10 lilifunguliwa rasmi na Rais Dk. Mwinyi Novemba 11, 2020, baada ya kuingia madarakani.

Baraza hilo linaundwa na wajumbe kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), ACT Wazalendo na mjumbe mmoja kutoka Chama cha ADA-TADEA
 
Hamna kitu hapa. Huyu hawezi kuwa BOLD judge! Watoto wa juzi hawa hawawwezi ku resist pressure za madikiteita!

RIP MWALUSANYA, KATITI, LUGAKINGIRA
Huyu judge ni mchanga Sana,tumezimisi mikiki mikiki ya majaji nguli,ngoja ni kumbushe kidogo
1.LUHEKELO KYANDO
2.KAHWA LUGAKINGIRA
3.MWALUSANYA
Mawakili nguli
Professor Mgongo Fimbo,
Masumbuko Lamwai
Musa Kwikima
Uzito wa kesi hii aliyeifungua na jaji anayeisikiliza nawaona ni wepesi,kwa mtizamo wangu
 
Uko sahihi kabisa!

1750871506283.png

Judge Mwalusanya
 
Hiyo ni staged ili serekali ionekane imefanya reforms baada ya kubwagwa mahakamani.
 
Wanaharakati wanaojitambulisha Raia ni Sisi, Kumbusho Kagine na Bubelwa Kaiza wamefungua kesi namba 12670/2025 kupitia mtandao dhidi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiiomba Mahakama itoe amri ya kurekebisha upungufu uliomo kwenye Kanuzi za Maadili ya Uchaguzi.

Taarifa kutoka kwa Raia ni Sisi wanaowakilishwa na mawakili wasomi Mpoki Bukuku na Jebra Kambole imesema kesi imetajwa leo Jumatano, Juni 25, 2025 mbele ya Jaji Kagomba, Mahakama Kuu Dodoma.

Taarifa Zaidi zinadai kuwa Serikali imeweka pingamizi dhidi ya umahiri wa kiapo.

“Jaji Kagomba amepanga kusikiliza na kutolea uamuzi pingamizi la wajibu maombi siku ya Alhamisi Julai 3, kisha, iwapo ataona pingamizi halina mashiko, kuendelea kusikiliza shauri hilo. Shauri litasikilizwa Mahakama ya Wazi, [Mahakama Kuu] Jijini Dodoma,” imesema taarifa ya Raia ni Sisi.
Very excellent.
 
Hivi Kumbusho Kagine alienda kumuomba msamaha mwalimu Mgeni pale Kihesa Sekondari maana huyo dogo alimpa kichapo mwalimu wake wakati yupo kidato cha nne Kihesa Sekondari -Iringa
 
Back
Top Bottom