Waifu Kanifuma Kanishikia Bango

gwangaeto

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
492
529
Yamenipata, baada ya kuotea virai(hela) flani ivi nikasema ngoja nitafute saiti, nikapata sehemu flani ivi kuna kajumba na kauwanjaaa kazuriii ila hapana umeme, nikasema hakuna noma nikafanya muamala nikachukua ile saiti nikaanza kupambana na hali yangu ya kuhakikisha navuta waya nihamie.

Basi siku iyo nkaondoka kimazabe hom, sina tabia ya kumuaga waifu huwa siamini kama anaweza kunifatilia, basi nikachukua mkaa, waifu akaguna, 'watu wanaenda kupika uko' sikumjibu nilikua namuwahi fundi alikuwa amefika saiti na ameagiza mkaa na chumvi ya magadi kwa ajili ya kutengeneza 'ethi rod' ile ya kuzuia radi.

Basi nikafika saiti tukapiga kazi na fundi fresh tukamalizana akasepa nikabaki nafungafunga milango, sasa ile kucheki ng'ambo nyumba ya jirani nkamwona mdada, haaa huyu si namfahamu, nkaenda kumsabahi aa dada (jina lake) vipi kumbe unakaa apa?? Akajibu ndio ndo kwangu' Nilikua na makofidensi ya ajabu kozi kuna kipindi tuliwahi kuvunja amri ya sabini, nkamwambia aaa nikaribishe ndani basi, akasema aa apana usiingie, nkaona ananizingua nkazama mpaka geto kwake nkacheki cheki vichupi vyake kavitundika ukutani, ile natoka nkashangaa anakuja mkuku mkuku kama anakimbizwa na jeshi la waasi, 'mkeo huyo anakujaa' akabana mlango paaa akanifungia kwa ndani, asalaleeeeee...

Niliishiwa nguvu, nikaona apa ndo kalikoroga, picha limeingiliwa jambazi kaua steringi itakuaje, nikarudi rum kwake mara nasikia nje uko waifu anamaka 'mme wangu yuko wapi, nimemuona apa kwa macho yangu!!!' Yule dada akajibu 'mme wakoooo.... Hajaja apa labda umeona jini..' Wakaanza kuchambana pale timbwili la asha ngedere mi nko ndani nachungulia dirishani, nkawa nasikia majirani wanasogea.

Waifu anakaza mbaya pale autisaidi 'mfungulie mme wangu, siondoki apa bila kumwona, anawaonyesha majirani,' baskeli yake ile palee, nimemwona kaingia apa, uyu dada anakataa hajamwona'. Kule ndani nilikua nimepoa kama naishi kwenye friji, nkawa najisemea tu, 'huyu mwanamke si aondoke tu akanisubiri nyumbani.... , lakini mawazo yangu yalikua tofauti sana na ya waifu ambae aliendelea kukomaa pale nje afunguliwe mlango, mmewe yuko ndani.

Yule dada alivoona watu wanazidi kujaa akabana mlango na kufuri akasepa, alivofika mbali akanitext nifanye kila namna waifu aondoke pale atamtuma mtu aje kunifungulia. Nikamtumia waifu meseji 'funguo iko wapi niko nyumbani, mbona haupo??? Hapo ndo nikasikia kichaa cha mbwa, waifu alibweka kule nje,' funguo wapi wakati uko humu ndani, toka tu mme wangu twende nyumbani,.... akawa anahubiri pale nje huku anazunguka ile nyumba. Watu wengine wakawa wanamuona kama chizi, anapigaje makelele kwenye nyumba ya mtu wakati mwenye nyumba hayupo, afu nyumba imefungwa wengine wakaanza kuondoka, nikamsikia akisema 'atatoka tu mi siondoki apa'. Kweli alipiga patroo kutoka saa 12 mpaka saa tatu usiku. Uko ndani niliganda kama nimehifadhiwa mochwari.

Mara ikaingia meseji ya msela saa 3 io night, 'oya bro nimetumwa nikufungulie lakini naona waifu wako kaweka gadi ya kufa mtu apa, mlango wa nyuma kuna mmama, mbele kuna mmama afu yeye anazunguka apa, ko endelea kuvuta subira' Daaamn nilichoka uko ndani nilikauka ka panzi kwenye tandu la buibui.

Baadae mida kama nne ivi nkasikia wamama wanashauriana uko nje, 'tuondoke tu mama naniii, kamsubiri tu nyumbani atakuja'. Apo waifu akatoa tangazo fupi, 'mme wangu naondoka lakini tambua nimekuona uko humu ndani, utanikuta nyumbani, tutamalizana uko'. Nkasikia vishindo 'tu..tu..tu...tu....tu'..... wakaondoka, nikapumua hfuuuuuuuuuu.

Baada ya robo saa yule msela akaja akanifungulia,' da broo pole sana, mkeo ni noma sana mzeee angefaa kuwa mlinzi wa benki'. Nkawa sina la kusema, nilikua nimekasirika vibaya, nkawa mmeinama mmeshika magoti ka fowadi aliyekosa penati, dogo akafunga mlango, tukaondoka.

Ntakuja Na Mrejesho, Kilichonipata Baada Ya Kurudi Nyumbani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom