KIMBURU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2011
- 210
- 189
Ni jambo la kusikitisha sana kuona mpaka leo tarehe "33" bado watumishi wa wilaya ya Urambo wanaowakilishwa bungeni na mh. Sitta na Kapuya hawajapata mishahara yao. Tabia hii ya kuchelewesha mishahara inaonekana kuota mizizi kwani hata mwezi uliopita mishahara ilitoka tarehe "34".
Mh. Rais na wote wanaohusika na hili naomba mlitilie maanani ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha watendaji wanaosababisha hali hii; kwani watumishi wa Urambo hasa walimu (sijajua sekta nyingine) wako kwenye hali ngumu na kuishia kukopakopa tu jambo linalowashushia heshima yao machoni pa jamii na hivyo kupunguza hata ufanisi wao wa kazi.
Na pia ni jambo la kusikitisha kuona watumishi wanasherehekea siku yao ya Mei mosi wakiwa hawana hata sent tano mfukoni.