Wahubiri Wenzangu, tuhubiri utakatifu

Wahubiri Wenzangu, tuhubiri utakatifu

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
2,265
Reaction score
2,457
VIONGOZI TUHUBURI UTAKATIFU

1)Ipo kauli moja ambayo ambayo inapendwa sana na waamini wanaopenda sababu ya kuhalalisha kwao kudumu kuishi kudumu katika dhambi

1)kauli ya kwanza wanayoipenda sana kuisikia DUNIANI SISI WOTE TUNA DHAMBI HAKUNA ASIYE NA DHAMBI


2)Kauli ya pili inayopendwa ili kuhalalisha kwao kudumu katika dhambi zao ni hii...TUNAOKOLEWA KWA NEEMA ..ni neema tu sio kwa jitihada zetu sio kwa matendo yetu sio kwa kulipa gharama .

na mistari wanayoipenda ni hii

1 Yoh 1:8-10
Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.

Rum 3:23-26
kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake,

Efe 2:8-10
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu


Lakini moja ya mafunuo kwa ya wenzetu wa kizazi chetu waliobahatika KUONGEA NA YESU uso kwa uso katoka kizazi chetu hiki cha sasa.

YESU amesissitiza tuhuburi *UTAKATIFU"(kujitenga na dhambi,kutengwa na dhambi..kutakaswa...Ndio maana unaona mahubiri yangu yote ninayohubiri yote kabisa yanaongelea kitu kimoja tu...KUACHA DHAMBI KABISA ...UTAKATIFU...ndio kitu alichokisisitiza Yesu katika hiki kizazi chetu..

Kwa sababu watu wanapenda kudumu katika dhambi na kusema kuna NEEMA na sisi wote ni wenye dhambi kwa hiyo tuendelee tu hatuwezi kuacha dhambi ..tutaokolewa tu kwa neema tu ipo..tu..neema nyingi tu..hata hawawezi kusema nimeokoa ..wanasema duniani hakuna kuokoka wala hakuna utakatifu..wala hakuna asiye na dhambi..


SIO KWELI SISI NI LAZIMA TUWE WATAKATIFU HAPA DUNIANI.

Huwezi kuishi katika dhambi halafu utegemee utaenda kuwa mtakatifu mbinguni baada ya kufa..Hakuna baada ya kufa kitabu chako chaatendo yako hapa duniani kinafungwa kinachofuata ni hukumu..kuvuna ulichopanda kadiri ya matendo yako pindi ulipokuwa hai duniani unatoa hesabu ya matendo yako.

ndio maana unaona hata walutheri hawana ibada ya wafu kuombea wafu waliokufa ili Mungu awapeleke peponi..kinachoamua uende peponi ni matendo yako ukiwa hai duniani baada ya kufa hakuna kuokoka tena unaokoka ukiwa hai duniani kabla hujafa.

1)DUNIANI KUNA WATAKATIFU sio kweli kwamba wote waliopo duniani ni wenye dhambi.

2)sio kweli neema ipo tu nyingi ya kuchezea kwamba unarudia tu kufanya dhambi kwa makusudi halafu baadae unatubu halafu baadae unarudia tu kwa makusudi au unasema acha nitende dhambi kwanzaa nikikaribia kufa au nikizeeka sana nitatubu tu na kuingia mbinguni..ILA .tunatakiwa tuwe watakatifu hapa duniani ni lazima ..kama tunataka kuingia mbinguni kama kweli tunataka kuongia peponi tisiende motoni..NI LAZIMA tuwe watakatifu..hakuna kinyonge kitakachoingia mbinguni,mbingu ni takatifu walioko mbinguni ni watakatifu..tuyasafishe tuyafue mavazi yetu yawe meupe ..yasiwe na madoa doa...TUSIWE VUGU VUGU na michanganyo changanyo..TUOKOKE KWELI KWELI..100% ..Roho mtakatifu anaishi ndani yetu na yeye YESU na BABA wanakuja kukaa ndani yetu ..ndio wanatusaidia tena SIO kwamba roho mtakatifu ni msaidizi wetu ni anatawala kabisa maisha yetu ndiye yeye ROHO mtakatifu ukimruhusu atawale kabisa maisha yako..anakuongoza kabisa kuushinda ulimwengu mwili huu wa dhambi na tamaa zake mbaya.

Yesu alishinda na sisi tunaishinda dhambi kupitia YESU ,kama Paulo alipigana vita akavipiga vyema .

UKISHAOKOKA tu unakuwa upo vitani katika ulimwengu wa roho na ulimwengu wa giza na dhambi..lakini tunaishinda dhambi/mauti kupitia YESU..nasi tunamshinda kwa damu ya mwanakondoo.

HII NEEMA hii NEEMA tunayosema tunaokolewa kwa neema ndiyo hiyo neema inatufundisha kukataa UOVU..hakuna neema inayokufundisha uendelee kudumu katika dhambi na kusema wote tuna dhambi kwa hiyo ni sawa tu.

maandiko haya hapa chini baadhi kidogo.


Tit 2:11-12
Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa

1 Pet 1:15-16
bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.

Zab 16:3 SUV
Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.


Ebr 12:14-17
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao


Ni sahihi kwamba hutupaswi kujisifu kuwa sisi ni watakatifu...mana hata paulo alisema kama ninkujisifu atajisifu katika udhaifu wake..ila sio kitu kizuri kujisifu katika dhambi kwa kusema sisi ni wenye dhambi tu tuendelee kuishi katika dhambi tu mana hatuna namna..ipo tu neema ya kuchota itatusaidia ila hatuna uwezo wa kuishinda dhambi..

Rum 6:1-7
Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?

2 Tim 4:7 S
Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda

Unapo okoka tu mana yake tayari rasmi umeingia vitani...sasa unatakiwa ushinde vita yako...kuishinda dhambi..ni kweli hutaweza peke yako..kwa sabau unavyo mkiri tu YESU tayari hauko tena peke yako unakuwa upo na Yesu..

Naye anatupatia nguvu ya kushinda yote..
Tunayaweza mambo yote kupitia yeye atutiaye nguvu..
Tunapokea nguvu inayotuwezesha kuushinda tamaa mbaya za mwili huu wa mauti na mawazo yake mabaya.

KITU kimoja YESU amesisistiza sana katika kanisa la sasa tuhubiri juu ya utakatifu ili tusizoee kudumu katika dhambi na kusema its okey kila mtu ana dhambi..hakuna asiye na dhambi so its normal ..ipo tu NEEMA ...NEEMA NYINGI TU.

tuhubiri watu WAACHE DHAMBI ...dhambi ikemewe na kuonyana kwa upole na upendo..

sipendelei sana kusema tu wote tuna dhambi tu kwa hiyo ni sawa tu..its ikey tu...wote TUMEPEWA WITO na YESU kuutafuta UTAUWA ,UTAKATIFU..ndio tiketi ya kwenda mbinguni na wote tukonsafarini kuelekea huko hakuna anayetaka kwenda motoni.
 
Yn 8:11
Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]

Yohana 5:14
Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.
 
Yn 8:11
Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]

Yohana 5:14
Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.
sasa kama angekuwa anajua haiwezekani sisi binadamu kuishi maisha ya UTAKATIFU utauwa ya kutengwa na dhambi, asingewaambia hawa watu...wasitende dhambi tena kama haiwezekaniki??
 
  • Thanks
Reactions: K11
Yesu amesisitiza,tuhubiri UTAKATIFU(tukemee dhambi,watu waache dhambi)
 

Attachments

  • images - 2026-03-11T064212.186.jpeg
    images - 2026-03-11T064212.186.jpeg
    38.8 KB · Views: 6
  • Thanks
Reactions: K11
HITIMISHO
tunaweza kuhitimisha kwa kusema.

Ufu 22:11 SUV
Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.
 
Tuhubiri wokovu toba na msamaha.. Utakatifu ni wa Mwenyezi Mungu mkuu
[/QUOTE
Kama tunataka kweli kungia mbinguni peponi na kuikwepa kwenda motoni ni lazima tuwe watakatifu hapa duniani.(peponi/mbinguni ni sehemu ya watakatifu like wise jehanamu ya moto ni sehemu ya wenye dhambi)

Kama mbinguni wataingia wenye dhambi..basi motoni hakuna atakayeingia hata shetani ata claim na yeye kuingia peponi.

ukisoma biblia imeeleza wazi wazi hatima ya wenye dhambi wote ni motoni jehanamu ya moto.

na biblia imeeleza ili uingie mbinguni peponi lazima uwe mtakatifu ingali ukiwa hai hapa duniani.

Na hapa duniani walikuwepo binadamu watakatifu na hata leo wapo ,hata mimi na wewe tunaalikwa kuwa mmoja wao.

Ndio kusudi la Yesu kuja duniani ili kuja kutukomboa wanadamu kutoka utumwani mwa dhambi ili tusiwe tena chini ya dhambi.

NDIO kusudi la ROHO mtakatifu ili kutuongoza...sisi tunatakiwa kumtii Roho mtakatifu...anayetupa nguvu ya kuyaweza mambo yote ..KUMTII MUNGU...

Na sisi tuna hiyo nguvu ya Mungu ufanani na Mungu sisi ni mfano wa Mungu kwa huo utakatifu...

Tufanane na Yesu...petro alifanana na Yesu kuvaa kunena kwake hata kutembea kwake...sisi pia tunapaswa kufanana na Mungu katika maisha yetu yote..

Maisha yetu yote ya kila siku kila dakika ni ibada.
 
Zab 16:3
Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.

Law 20:26
Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi BWANA ni mtakatifu nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe wangu.

Ebr 12:14-15
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu;

1 Yoh 3:8 S
atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.

Ufu 21:8 S
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

1 Kor 6:9-11 SUV
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu?Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.

Wagalatia 5:19-21 BHN
Basi, matendo ya kidunia yanajulikana: Uzinzi, uasherati, ufisadi; kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, choyo, mabishano, mafarakano; husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine kama hayo. Nawaambieni tena kama nilivyokwisha sema: Watu wanaotenda mambo hayo hawataupata ufalme wa Mungu uwe wao.

Ufu 21:27
Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.
 
Hii injili ya utakatifu haihubiriwi kabisa popote ndio maana YESU amesisitiza wahubiri TUHUBIRI injili hii ya KWELI ili watu watubu na kuacha dhambi zao /tutubu sawa ni jambo la kwanza lakini kubwa zaidi ni tusifanye dhambi tena ,..ndivyo hata Yesu alivyoagiza ..tusitende dhambi tena..na ndivyo hata NEEMA ya Mungu inavyotufundisha kutokudumu kwenye dhambi..

12
Tit 2:11-12
Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa

Yn 5:14 S
Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.

WATU WANAHUBIRIWA KUHUSU KUPOKEA MAFANIKIO YA MALINZA DUNIA..BADALA YA WOKOVU HALISI...kuokoa MIOYO YAO Roho zao..

Mana MOYO wako ndio una thamani kuliko mafanikio ya mali za duniani ambazo tunakufa tunaziacha hapa duniani.

Luka 12:23
Kwa sababu uzima ni bora kuliko chakula, na mwili ni bora kuliko mavazi.

tunasumbukia vitu viharibikavyo vyakula,mavazi,magari,nyumba ,mafanikio na kuweka hazina hapa duniani...na sisi tuko safarini kwanza hatukuja na kitu duniani tukizaliwa uchi na tutaondoka duniani uchi bila chochote vyote tutaviacha hapa hapa..ila matendo yetu yatatufata tutatolea hesabu ya matendo yetu huko kwenye kiti cha hukumu..utajiri wa duniani hautatusaidia siku ya hukumu..na mafanikio yake ila matendo yetu yata ambatana na sisi..tuweke hazina mbinguni ya matendo utajiri wa matendo mema.

Mit 4:23-24 SUV
Linda sana moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. Kinywa cha ukaidi ukitenge nawe, Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.

Mt 6:21
kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.

1 Timotheo 6:18 NEN
Waagize watende mema, wawe matajiri katika matendo mema, pia wawe wakarimu na walio tayari kushiriki mali yao na wengine.

Mt 16:26
Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
 
INJILI inayohibiriwa leo watu wanayotaka kuisikia ni ya kupokea mafanikio baraka halafu waendelee kuishi maisha yale yale ya dhambi.

Wamegeuza kusudi la Mungu..wao wanatanguliza mali mafanikio bila kumtafufuta huyo Mungu mtoa riziki mwenyewe.

Wakati Mungu anawataka wao wenyewe wabadilike mioyo yao wafanane na yeye wawe watakatifu
Mathayo 6:33
L*akini utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote atawapa pia.*
 

Attachments

  • images - 2026-03-11T064212.186.jpeg
    images - 2026-03-11T064212.186.jpeg
    38.8 KB · Views: 5
  • images - 2026-03-11T072153.706.jpeg
    images - 2026-03-11T072153.706.jpeg
    9.4 KB · Views: 2
  • images - 2026-03-11T072226.716.jpeg
    images - 2026-03-11T072226.716.jpeg
    35.2 KB · Views: 2
  • images - 2026-03-11T072504.623.jpeg
    images - 2026-03-11T072504.623.jpeg
    37.3 KB · Views: 2
  • images - 2026-03-12T083108.634.jpeg
    images - 2026-03-12T083108.634.jpeg
    40.9 KB · Views: 2
  • 1555667456310.jpeg
    1555667456310.jpeg
    85 KB · Views: 2
INJILI inayohibiriwa leo watu wanayotaka kuisikia ni ya kupokea mafanikio baraka halafu waendelee kuishi maisha yale yale ya dhambi.

Wamegeuza kusudi la Mungu..wao wanatanguliza mali mafanikio bila kumtafufuta huyo Mungu mtoa riziki mwenyewe.

Wakati Mungu anawataka wao wenyewe wabadilike mioyo yao wafanane na yeye wawe watakatifu
Mathayo 6:33
L*akini utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote atawapa pia.*
Mathayo 6:33
Lakini utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote atawapa pia.

ndio mana watu wanaenda kwa mitime na manabii wa uongo wanaotumia nguvu za giza na mafuta kutoka kuzimu,maji ya maiti,michanga ya kaburi..

vitu wanavyodanganywa kuwa ni vya upako mafuta ya upako,maji ya upako,keki ya upako wanalishwa vitu vya kichwawi na uganga wa kienyeji kutoka kuzimu
wanapandikizwa majini mapepo huko kwa mitume na manabii..
MUNGU AWASAIDIE NI HURUMA NA HUZUNI napoona mtume na nabii wa uongo watu wamejazana wana gombania mafuta ya upako...ni huzuni...
 
Kwa nini Yesu alisema, “Nenda na usitende dhambi tena,” ikiwa hilo haliwezekani?

Katika Yohana 8:11, Yesu anamwambia mwanamke aliyenaswa katika uzinzi “nenda zako na usitende dhambi tena”. Kwa nini Angesema hivi ikiwa isingewezekana kuacha dhambi?

Watu wamejaribu kueleza wanachofikiri Yesu alimaanisha kwa maneno haya. Wengine husema kwamba Yesu alisema hivyo kwa matumaini kwamba tungejaribu kuacha dhambi lakini hatarajii tufanye hivyo kweli. Watu wengine wanafikiri kwamba Yesu alikuwa anadhihaki na kumwambia mwanamke huyo aende na asitende dhambi tena kwa sababu alitaka kuwafundisha Mafarisayo somo. Karibu hakuna mtu aliyethubutu kuuliza: Je, ikiwa Yesu alimaanisha kile Alichosema?

Inamaanisha nini “kutotenda dhambi tena”?
Je, ikiwa “Nenda na usitende dhambi tena” kwa hakika ni amri ya kuacha kuishi katika dhambi? Je, hilo haliwezekani? Yesu alimaanisha nini – maana Yohana anaandika kwamba sisi ni waongo tukisema kwamba hatuna dhambi? ( 1 Yohana 1:8 )

Mistari katika Yakobo 1:14-15 inatoa maelezo mazuri ya dhambi hii ambayo sisi sote tunayo. “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukuwa mimba huzaa dhambi.”

Kuna dhambi ndani yetu sote, tumezaliwa nayo. Ni tamaa zetu wenyewe mbaya (dhambi iliyo ndani yetu) ndizo zinazotupeleka mbali na kutujaribu. Hiyo ndiyo maana ya Yohana anapoandika kwamba tuna dhambi. Lakini kuwa na dhambi haimaanishi kwamba tunapaswa kukubali majaribu hayo. Ni pale tu tunapokubaliana na mawazo ya dhambi tunayojaribiwa nayo na kusema Ndiyo, ndipo tumetenya dhambi.

Kwa hiyo Yesu aliposema, “Nenda zako na usitende dhambi tena,” hakutarajia kwamba mwanamke huyu angeacha asili yake ya dhambi ya kibinadamu pale pale na hatajaribiwa tena. Alikuwa akimwambia aseme Hapana kwa dhambi iliyokuwa ikiishi ndani yake, asikubali alipojaribiwa, na kuacha tamaa isikue na kuwa dhambi; kukomesha jaribu la kuwa dhambi.
 
Kwa nini Yesu alisema, “Nenda na usitende dhambi tena,” ikiwa hilo haliwezekani?

Katika Yohana 8:11, Yesu anamwambia mwanamke aliyenaswa katika uzinzi “nenda zako na usitende dhambi tena”. Kwa nini Angesema hivi ikiwa isingewezekana kuacha dhambi?

Watu wamejaribu kueleza wanachofikiri Yesu alimaanisha kwa maneno haya. Wengine husema kwamba Yesu alisema hivyo kwa matumaini kwamba tungejaribu kuacha dhambi lakini hatarajii tufanye hivyo kweli. Watu wengine wanafikiri kwamba Yesu alikuwa anadhihaki na kumwambia mwanamke huyo aende na asitende dhambi tena kwa sababu alitaka kuwafundisha Mafarisayo somo. Karibu hakuna mtu aliyethubutu kuuliza: Je, ikiwa Yesu alimaanisha kile Alichosema?

Inamaanisha nini “kutotenda dhambi tena”?
Je, ikiwa “Nenda na usitende dhambi tena” kwa hakika ni amri ya kuacha kuishi katika dhambi? Je, hilo haliwezekani? Yesu alimaanisha nini – maana Yohana anaandika kwamba sisi ni waongo tukisema kwamba hatuna dhambi? ( 1 Yohana 1:8 )

Mistari katika Yakobo 1:14-15 inatoa maelezo mazuri ya dhambi hii ambayo sisi sote tunayo. “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukuwa mimba huzaa dhambi.”

Kuna dhambi ndani yetu sote, tumezaliwa nayo. Ni tamaa zetu wenyewe mbaya (dhambi iliyo ndani yetu) ndizo zinazotupeleka mbali na kutujaribu. Hiyo ndiyo maana ya Yohana anapoandika kwamba tuna dhambi. Lakini kuwa na dhambi haimaanishi kwamba tunapaswa kukubali majaribu hayo. Ni pale tu tunapokubaliana na mawazo ya dhambi tunayojaribiwa nayo na kusema Ndiyo, ndipo tumetenya dhambi.

Kwa hiyo Yesu aliposema, “Nenda zako na usitende dhambi tena,” hakutarajia kwamba mwanamke huyu angeacha asili yake ya dhambi ya kibinadamu pale pale na hatajaribiwa tena. Alikuwa akimwambia aseme Hapana kwa dhambi iliyokuwa ikiishi ndani yake, asikubali alipojaribiwa, na kuacha tamaa isikue na kuwa dhambi; kukomesha jaribu la kuwa dhambi.
Na je, hii si amri ile ile anayotupa sisi sote?

Nguvu ya msalaba

Yesu mwenyewe asema katika Luka 9:23, “Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate.” Hiyo ina maana kwamba tunapaswa kusema Hapana kwa mawazo na tamaa zinazotujaribu na kutunasa. Kwamba tunapaswa kuchukua msalaba wetu na kuacha kabisa mawazo haya kabla hayajawa dhambi. Kwa njia hii tunafuata mfano wa Yesu ambaye “alijaribiwa katika kila namna kama sisi, lakini hakutenda dhambi”. Waebrania 4:15.

Kuchukua msalaba wetu - hilo ndilo jambo muhimu zaidi. Ikiwa tutafanya hivi - ikiwa hatutaruhusu tamaa hizi za dhambi kuwa dhambi - basi tunamfuata Yesu, kama alivyotuambia kufanya. Kisha tunatimiza agizo la “nenda na usitende dhambi tena”.

“Basi vifisheni viungo vyenu vilivyo vya katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu.” Wakolosai 3:5.

"Na hao walio wa Kristo Yesu wamesulubiwa mwili Pamoja na Mawazo yake mabaya Pamoja na tamaa zake." Wagalatia 5:24.

Ni wazi kwamba ikiwa tunataka kuwa wa Kristo tunahitaji kufanya hivi hasa: “Mkinipenda, mtazishika amri zangu.” Yohana 14:15.

Je, inawezekana kwenda na usitende dhambi tena?

Unapojaribu kuishi maisha haya ya kushinda dhambi utaona haraka kwamba si rahisi sana kufanya. Licha ya nia yetu nzuri tunaanguka na kuanguka na kuanguka tena.

“Basi nasema enendeni kwa roho wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.” Wagalatia 5:16. Ufunguo wa kuishi maisha ya ushindi ni kumwacha Roho aongoze maisha yako, au kama ilivyoandikwa katika tafsiri nyingine, kutembea katika Roho. Na hiyo inamaanisha kuwa mtiifu kwa Roho. Tukifanya hivi, basi imeandikwa kwamba hatutafanya kile ambacho asili yetu ya dhambi inataka tufanye. Na ikiwa hatufanyi kile asili yetu ya dhambi inataka tufanye - ikiwa hatutakubali tunapojaribiwa - basi hatujatenda dhambi!

Ni rahisi kuja na sababu nyingi kwa nini haiwezekani "kwenda na usitende dhambi tena". Unaweza kufikiri kwamba Yesu alikuwa anazungumza na mwanamke huyu maalum na hasa kuhusu uzinzi. Unaweza kusema kwamba Alisema hivyo ili tu kuwafundisha Mafarisayo somo na hata hakumaanisha kile Alichosema. Unaweza kusema kwamba Alimaanisha kwamba tunapaswa kujaribu tu kadiri tuwezavyo lakini kwa vyovyote vile baada ya muda tungeanguka.

Lakini ukweli ni kwamba Yesu hakusema lolote kati ya mambo hayo.

Alichosema ni, “Nenda na usitende dhambi tena.” Na Yesu alimaanisha kile alichosema.

Biblia haikusudiwi kugawanywa na kuchunguzwa na kufafanuliwa na kufasiriwa. Imekusudiwa kusomwa na kutii. Kinachosemwa ndicho kinamaanishwa. Biblia ni Neno la Mungu, lililoandikwa na watu wanaomcha Mungu walioongozwa na roho wa Mungu. Hakuna kitu hapo ambacho hakipaswi kuwa hapo. Mungu alijua alichokuwa akifanya.

Kwa hiyo Yesu aliposema, “Enenda zako na usitende dhambi tena,” alimaanisha twende na tusitende dhambi tena!
 
LEARN TO UNLEARN Ego is your enemy.
 

Attachments

  • images - 2026-03-15T201143.311.jpeg
    images - 2026-03-15T201143.311.jpeg
    16 KB · Views: 2
  • images - 2026-03-15T201017.535.jpeg
    images - 2026-03-15T201017.535.jpeg
    44 KB · Views: 3

Similar Discussions

Back
Top Bottom