Habari wana-Jf!!
Kuna hili suala kama linavyosomeka katika thread hapo Juu,.
Nimekuwa nikijiuliza mara nyingi bila kupata majibu maana asilimia 80% ya wahubiri ambao nimewahi kukutana nao shuleni, vyuoni na hata katika maisha ya kawaida wengi wao ni wenyeji wa mkoa wa Mbeya!
Wakati mwingine nafikia kusema mkoa wa Mbeya umebarikiwa kutoa wahubiri wa neno la Mungu kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mikoa mingine na wengi wao ni walokole na madhehebu mengine ya Kikristo.
Wakuu tuambiane na mkoa wako mmejaliwa kitu gani cha kipekee kama ilivyo kwa Mkoa wa Mbeya kujaliwa wahubiri wa neno la Mungu?
NB: Mimi siyo mwenyeji wa mkoa Mbeya!
Nawasilisha,...
mkoa wa mbeya kuna makanisa mengi sana alafu pia kuna wachawi wengi karibu kila kaya kuna mchawi.
mbeya mpk mageto makanisa,
Mwakasege Mwaitege Mwasabwite, Mwaipaja, Mwabukusi, Mwakyoma, Mwasote, Mwansasu, Mwisapile, Mwandosya, Mwakyembe Bukuku, Mwakaleli ........
una uzoefu. unatokea mbeya ?
Hahahahaa Mwapapu......... Duh!!!MWALYOYO,MWAMPASHI,MWALUKO,MWANDWELO,MWAKYAMBIKI,MWAIPOPO,MWAPAPUCHI,MWAFILIFILI,MWASANGA,....nakuja kuendelea
Asante mkuu kwa kuliona ilo,ila si ilo peke yake bali kuna mchele wa mbeya, maharage viazi na hivyo vimebarikiwa kuwepo ktk mkoa huo huo
mbeya mpk mageto makanisa,
Kuhubiri sio kufundisha na uwingi wa wahubiri sio kuwepo kwa IMANI. Pamoja na kwamba kuna wahubiri wengi MBEYA ina idadi kubwa sana ya matukio ya uhalifu kwa mfano mauaji yanayotokana na imani za kishirikina, ubakaji unaofanywa na wachungaji na uhalifu mwingine wa kutisha. Kila siku kwenye mahabusu za Mbeya lazima kuna mchungaji au mzee wa kanisa anayetuhumiwa kwa makosa ambayo hata si ya kiimani kama vile utapeli. Jiulize, kama ni kuhubiri neno la Mungu kwa nini akina Lusekelo wanahubiri mijini tu hususan Dar es salaam?Habari wana-Jf!!