Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,067
- 4,506
1. Kumekuwa na wahitimu katika vyuo mbali mbali nchini ambao wamekuwa wakijibainisha kuwa ni wahitimu wa vyama vya siasa hususani Chaso na Ccm!
2. Mtumishi wa umma (civil servant) au wa majeshi ya umma (millitary servant) hatakiwi kufungamana na itikadi ya chama cho chote cha siasa bali anatakiwa kutii mamlaka halali iliyowekwa na wananchi kupitia uchaguzi mkuu (chama kinachotawala). Hii ni kwa mjibu wa katiba ya nchi.
3. Kwa msingi huo wahitimu hawa waliojibainisha kuhitimu na kufanya mahafali ya kuhitimu ya vyama vya siasa wamejiondolea sifa ya kuajiriwa kwenye civil or millitary service vinginevyo itakuwa ni hatari na ni kinyume cha katiba.
4. Mamlaka za nchi zinapaswa kuwabaini wahitimu hawa ili wasije kuajiliwa katika utumishi wa umma. Waajiliwe kwenye vyama vyao vya siasa au kwingineko.
5. Wasiwasi wangu ni kuwa hawa vijana na wazazi wao sidhani kama wanalijua hili. Wanaingizwa mkenge na vyama hivi vya siasa. Watakuja kujuta mbeleni. Serikali ingepiga marufuku mtindo huo ili kuokoa vijana wetu kuingizwa mkenge at this tender age!!